Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Kwa style hii itakuwa vigumu sana kuikomboa Tanganyika. Uvyama, ukabila, udini, huyu ni wa Lissu, huyu wa JPM.

Aliyofanya Mange, Maria Sarungi, Polepole huko nyuma yote inabidi yawekwe pembeni kwa sasa. Tuna adui mkubwa zaidi kwa sasa.
Kwa sasa wao ndio wanatuhabarisha wanaofanya ufisadi, mauaji, utekaji, ndio wanaompigania Lissu atoke. Kwa sasa waungwe mkono.

Watanzania wote wanatakiwa kuwa wamoja wapigane kuondoa huu uongozi dhalimu wa sasa, baada ya hapo serikali ya mpito ikijumuisha wadau wote, watapanga jinsi ya kupata katiba mpya, Tume mpya ya uchaguzi, mahakama huru.

Wanamtandao wanawatawala Watanzania sababu siku zote wanawagawanya na kuwaweka kwenye makundi. Siasa safi, katiba mpya, tume huru, mahakama huru utaletwa na umoja wa Watanzania wote wakiwemo wana-CCM, vyama vya upinzani, wasio na vyama, viongozi wa dini na wadau wengine.

Polepole kajitolea kuwapigania Watanzania akijua wakati wowote wanaweza kumuua. Anasema uchafu wote uliopo ndani ya serikali, wahusika, jinsi unavyofanywa ndani ya CCM na serikalini na jinsi ya kusafisha CCM, serikali, nchi.

Kuwapinga hawa wanaharakati inasaidia kuimarisha hii serikali dhalimu ya sasa, kuwapa nguvu wanamtandao, mafisadi, wauwaji na watekaji. Haisadii harakati za ukombozi wa Tanganyika. Haisaidii Chadema, haimsaidii Lissu.

Polepole ni shujaa wa Taifa. Kumpinga ni kudhoofisha, kukwamisha, kurudisha nyuma juhudi za ukombozi wa nchi hii.
Nakubaliana na wewe kwamba WATANGANYIKA inabidi TUUNGANE.

Kila mtu asimame kutetea nchi katika nafasi yake. Nathamini sana mchango wa Humphrey Polepole, nathamini sana mchango wa Maria Sarungi, nathamini sana mchango wa Mange Kimambi, nathamini sana mchango wa Evarist Chahali na nathamini michango ya watu mbalimbali mitandoani na kwenye vyama vya siasa.

Jambo moja tu ambalo sitalichanganya ni lile la kuamini kwasababu anazungumza kichagga basi ni lazima huyu atakuwa ni Mchagga. Tuna kasumba mbili kubwa kwenye siasa zetu. Mosi, kuamini kwamba kila anayezungumza lugha sawa na sisi au kufanana na sisi basi ni mwezetu. Hili lilimgharimu sana Mzee Nyerere hata kwenye diplomasia ya nchi. Hili limebaki hadi kwetu, WATANGANYIKA tunaamini kwamba kila mtu anawaza mema kama sisi na ana moyo mkunjufu kama sisi.

Huwa yanatukuta tukiwa tumeshachelewa mno, ndiyo tunazinduka usingizini kwamba kumbe huyu hakuwa mwenzetu.

Pili, ni kutopenda kuwajibika kisiasa hata pale ambapo ni dhahiri tumefanya makosa makubwa yanayoonekana. Tunakarisika kabisa tukiambiwa ukweli. Ndiyo maana hadi leo hii Mzee Nyerere alifanya makosa na wengi hatupendi kuyaanisha hayo makosa ili tujifunze, tunaishia kujificha kwenye kivuli cha NIA NJEMA. AU kisipokuwa hicho tutasema ni hujuma za MABEBERU. Nothing is ever our fault. Sasa huu utamaduni wa kutopenda KUWAJIBIKA usipojengwa hapa nchini, tutakuwa na hali mbaya hata kama wapinzani watachukua nchi.

Sasa basi mimi naungana na wote wanaosema ukweli. Lakini sitajiingiza kwenye dhambi ya kuamini kwamba wote wanaipenda TANGANYIKA wala kuiwazia mema. Umri nilio nao unatosha kunifundisha mengi kuhusu siasa za Tanzania.
​
 
UTANGULIZI:
Habari ndugu MTANGANYIKA, leo ni mambo mengi kweli ya kusema ambayo yanatatiza sana moyo wangu. Nimejaribu kuandika wiki kadhaa lakini naishia kufuta kila nikimaliza kuyaaandika. Mengine nikiyasema hadharani yanaweza kuwaumiza sana moyo na mkaishia kukata tu, tamaa. Ila itoshe kusema kwamba TANGANYIKA ISHAUZWA.

1.TANGANYIKA KUTETEWA NA WANAHARAKATI WALIOWAHI KUTUHUJUMU:
Ndugu Humphrey Polepole na pamoja na wanaharakati wengine wa mtandaoni kama Mange Kimambi na Maria Sarungi, watu ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kuwa wanufaika wa mfumo na hata kutumika kuhujumu wananchi. Mtu pekee ambaye amekuwa akisema ukweli siku zote ni kaka yangu Evarist Chahali (He has been very Consistent and Objective).

Miundombinu mingi ambayo Samia anaitumia kututesa WATANGANYIKA, ilitengenezwa na Raisi John Pombe Magufuli. Humphrey Polepole na Dr.Bashiru Ali Kakurwa walikuwa ni wahandisi wakuu wa kisera. Ilifika kipindi hadi Dr. Bashiru alitamka wazi kwamba CCM inaweza kuvunja katiba ili kubaki madarakani kwasababu ndiyo imeshika dola.

Hawa wengine kama Maria Sarungi, na Mange Kimambi tunafahamu kwamba madai mengi yalianza kama maslahi binafsi. Hasahasa Binti Sarungi ugomvi wake mkubwa na JPM chanzo ni mambo ya kifamilia ambapo yeye kama munfaika wa mfumo alikutwa na SHOCK-THERAPY ya JPM. Alikuwa na mwenzake Fatma Binti Karume, ambaye mlimbatiza jina na kumwita Shangazi, lakini awamu hii rangi zake naye mshaziona.

Mange Kimambi, ni mamluki. Alishawahi kuwa upande wa CCM, baadaye dhidi ya Lowassa, baadaye upande wa Lowassa dhidi ya Magufuli. Baadaye kushangilia msimba wa Magufuli na kumnadi Samia, na saa hizi yuko dhidi ya Samia. WATANGANYIKA hatufahamu kesho atakuwa dhidi ya nani.

Hii dhambi naona inatafuna wengi mno hadi maafisa usalama ambao binafsi nawafahamu waliwahi kuwa mstari wa mbele kutetea kila ujinga unaofanywa na dola, ambapo mamia ya WATANGANYIKA walipoteza uhai, kuumizwa, kufungwa au kufilisiwa. Hata humu JF wengi nawafahamu, naona kabisa mwelekeo wao ni watu aliyepagawa na pepo au kapata wazimu.

WATANGANYIKA, ili kuepukana na kadhia hii ya kubebwa na kila aina ya upepo wa kimaslahi wa watu ni lazima WASOMI wajifunze kusimamia kitu kinachoitwa KANUNI (Principles). Hata pale ambapo mwanasiasa unayempenda anakosea, wewe inabidi uufunde moyo wako kusimamia KANUNI.

RAI YANGU KWA WATANGANYIKA, hasa WANAUSALAMA: Kwenye BIBLIA, Daudi alikuwa ni mtenda dhambi mkubwa kama sisi tu, lakini tunaambiwa ni moja kati ya watu walipata kibali kikubwa sana kwa MUNGU. MUNGU alisema wazi kabisa kwamba anampenda Daudi kwasababu MOYO WAKE HAUNA HILA. Daudi alikuwa ni mtu mwenye kusimamia KANUNI.

Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda amuue Daudi. Mara mbili Daudi alipata nafasi ya kumuua kabisa Sauli, kwa mambo aliyomtendea lakini Daudi alisimamia KANUNI. Alikataa kumuua na kusema HUYU NI MPAKWA MAFUTA WA MUNGU, atamalizana na MUNGU wake.

Daudi alikuwa ni KIONGOZI MKARIMU (Equittable). Kuna sehemu kwenye BIBLIA ilitokea vita, na baadhi ya askari wake walichoka wakashindwa kwenda vitani. Waliporudi na kupata ushindi mkubwa na mali nyingi, kuna baadhi ya askari wakasema hawa ambao hawakwenda na sisi vitani wasipewe chochote kile. Daudi aliwakemea na kusema aliyekwenda vitani, na aliyebaki kulinda mji wote watapata mali sawa. Akimaanisha kwamba kila mtu ana umuhimu ndani ya jamii.

Daudi alikuwa ni KIONGOZI MUUNGWA. Alikosea mno kwa kuiba mke wa mtu na kumpa mimba, huku akimuua mume wake. Baadaye alipofutwa na nabii Nathani kuambiwa ukweli, wala hakutafuta vijisababu, bali alikuwa mpole na kwenda kuomba msamaha mbele ya taifa zima. Hakusema kwamba yeye alikuwa na nia njema, ila alisema wazi kwamba amekosea.

SASA BASI: wale ambao mliwahi kuwakosea WATANGANYIKA, na kusababisha vifo, misiba, umasikinui na majeraha ombeni TOBA KWA MUNGU, OMBENI TOBA KWA WATANGANYIKA, lakini kubwa zaidi TOBA YA KWELI huambatana na mabadiliko ya moyo. Jaribuni kukaa kwenye viatu vya watu kama Wazazi wa Ben Saanane, Familia ya Gwanda, Familia ya Soka, Familia ya Akwilina na wengine kisha mtafahamu kwamba WENGI HAMKUISHI VIAPO VYENU.
​
Tanganyika hii NYERERE mwenyewe aliiponda akaiuza kwa wazanzibar.

Malechela alitaka kuipiga chini Zanzibar na kuianzisha Tanganyika wakati wa Mwinyi, walipojitokeza wabunge 55 au G-55,, Nyerere akaja juu kuutetea muungano hadi akamtungia Malechela kitabu.

Wa kumlaumu ni Nyerere aliyeiua Tanganyika jumla.

Rais wa Zanzibar wakati huo Salmin Amour alikuwa na dharau kubwa sana, na akasababisha hasira kwa hao wabunge 55 walioazimia kuifufua Tanganyika mwaka 1993 wakati wa chama kimoja - (CCM)

Hawa ni miongoni mwa wabunge G-55, Kashemeza Kabuye, marehemu. Njelu Kasaka, marehemu,, Philip Marmo, Tuntemeke Sana, marehemu, and others.
 
Umenena vema.
Kuna vitu JPM alikosea na vingine alifanya vema.
Lissu ana tabia fulani zinazo shabihiana na za JPM mojawapo kutodhibiti kauli zake. Na udikteta kwa mbali.
Anaamini yeye ni bora kuliko mtu yeyote kwenye kufikiri au kufanya maamuzi.
Wote JPM na Lissu wana tabia ya kupenda sifa.
Lissu ni mzuri sana kwenye mambo ya sheria lakini namuona siyo kiongozi mzuri sana.
Lissu ana tabia moja nzuri sana ya kusimamia hoja zake au itikadi fulani.
Kwa nje nje tu namuona Lissu siyo mtu wa rushwa.
Congratulations, you have escaped the matrix of intellectual lobotomy.

Kuna mtu aliwahi kusema humu ndani kwamba Tundu Lissu is an upgrade of John Pombe Magufuli with bugs fixed. Alikuwa sahihi mno. Lissu kama John, wote ni watu wenye akili nyingi mno (Highly Intelligent), wana tatizo la sifa (Egotistical), wote hawawezi kutawala hisia zao (Lack of Emotional Stamina), waropokaji (Loose lips) na hawana uwezo wa kupembua nyakati (Lack of discernment). Sina shaka na uzalendo wao hata chembe, wala utendaji kazi wao.

Tatizo ni kwamba kuwa kiongozi mzuri inahitaji zaidi ya kuwa BOOK-SMART. Inahitaji mtu uwe unaweza kusoma alama, nyakati na majira. Ni lazima ujifunze mambo ya msingi kuhusu utawala (State-Craft), kama ifuatavyo:

Mosi, kuna vita nyingine unashinda kwa kushindwa.
Pili, kunyamaza kimya saa nyingine siyo udhaifu bali ni busara na mkakati-vita.
Tatu, Vita zote kubwa duniani huwa zinapiganwa kwenye gizani kusipoonekana.

Ndiyo maana hata unapomfundisha mtoto kucheza CHESS ni lazima umwambie kwamba kuna sehemu lazima akubali PAWNS waliwe ili KING au KNIGHT aweza kuzunguka vizuri kwenye ubao. Ukishafahamu kwamba dunia hii inatawaliwa na watu waovu basi ni lazima utahitaji kuwa mtawala wa aina yake. KARATA ZOTE HAZIWEKWI JUU. Tanzanians are also not ready for this conversation.
​
 
2. UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA USALAMA WA TAIFA ILIVYOANZA
Idara za usalama duniani kote huongozwa na kitu kiitwacho COMPARTMENTALIZATION. Wanausalama wa chumba namba SABA hawatakiwi kufahamu kinachoendelea chumba namba MBILI. Wameenda mbali kabisa kwamba wanausalama wa chumba namba KUMI, hawatakiwi kuwafahamu wanausalama wa chuma namba NANE. Lengo zima ni kulinda usiri na weledi wa taasisi.

Baada ya MTANDAO kujipenyeza ndani ya CHAMA na SERIKALI, walivuruga utendaji kazi mzima wa taasisi za kiusalama hapa nchini. Taasisi kuu za kiusalama hapa nchini ziko tatu (PT, TISS na TPDF-The Cerberus of the State), hazikuwa zinafanya kazi kama inavyotakiwa.

Mwaka 2015, JPM amekuwa Raisi na kukuta wakubwa wengi ndani ya taasisi ni wale wa miaka kuanzia 1992, vijana wengi ni wale wa kuanzia 1996 na wapya wengi ni wale wa Jakaya. SHIDA YA TAASISI ZA KIUSALAMA, ni kwamba huwa mnaapishwa wote siku moja, na mnastaafu wote siku moja au mwaka mmoja, kama mtatofautiana basi ni miaka isiyozidi mitano.

Ndani ya TAASISI, huwa kuna IDARA MBALI-MBALI, kwasababu ni mwiko kuweka mayai yote ndani ya kapu moja(All Eggs in One Basket), maana yakivunjika inakula kwako. Afisa anapoenda kufanya oparesheni kubwa, ni lazima ajaze fomu na afanye utaratibu maalumu kwenda kuomba vifaa vya kufanyia kazi kutoka kwa watu wa IDARA NYINGINE, ambao wanavitunza.

Mfano, unatafuta kuua magaidi. Unafanya utaratibu wa kwenda kwenye IDARA yenye watu wenye mafunzo maalumu ya kijeshi, ambao hao watatakiwa kwenda kuomba silaha maalumu za kufanyia oparesheni kutoka kwenye IDARA nyingine inayotunza silaha. Kuna silaha kama SUMU (Chemical Weapons) huwa zinatunzwa kwenye ghala maalumu chini ya IDARA maalum SURVEILLANCE DEVICES, nazo zinakuwa chini ya watu wa IDARA nyingine.

Sasa operesheni inafanyika kwa kuunganisha idara hata zaidi ya tatu ndani ya TAASISI ya usalama. Mara nyingine tatizo likiwa kubwa sana hata PT, TPDF, MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS na MINISTRY OF FINANCE huhusishwa. Katika hili sasa ndipo MTANDAO walikuwa mbele ya Raisi JPM hatua tano zaidi. Kila akiratibu jambo kwa siri, taarifa zinavuja kutoka IDARA moja kwenda nyingine mwishowe zinafika kwa MTANDAO.

Leo umetuma watu kuchukua SUMU, watu wa ile IDARA kwa akili ya haraka wanajiongeza kwamba, kama SUMU inachukuliwa basi ni lazima kuna POLITICAL ASSASSINATION, hivyo taarifa zinavuja kwamba kuna Dangerous Substance imetoka maabara, na imebebwa na watu wa IDARA fulani hivyo wafuatilieni mwanzo mwisho. AU kuna watu wanafuatiliwa na IDARA ya IT, simu zao zimeingiziwa PERGASUS, taarifa zinatoka tu.

Mzee JPM kazidiwa ujanja, SULUHISHO NI NINI ??? Unda TASKFORCE na fanya En-Masse Recruitment, wape vijana mafunzo (Voda-Fasta) halafu waingizwe mitaani. Anza mdogo-mdogo kuchomoa baadhi ya maofisa ndani ya TAASISI, ambao una uhakika walipenyezwa na watu, lakini zuia Rectruitment nyingine isifanyike bila wewe kujua. Hapa ndipo wakazaliwa WATU WASIOJULIKANA.

Kweli TASK-FORCES, zinasaidia USIRI. Tatizo ni kwamba hazifanyi kazi kwa kufuata sheria. Maana ndani ya TAASISI, kila oparesheni inayofanyika ni lazima itakuwa AUDITED tu. Operesheni nyingi na fedha zake ni lazima zipitishwe na utawala wa kiraia (Civilian Administration) ili kuhakikisha TAASISI hazifanyi mambo ya ajabu kama kutaka kupindua nchi, au kutumika na watu binafsi kufanya hujuma.

Hata kipindi cha JK, taarifa zilikuwa zinavuja kwasababu ya huu mlolongo nwa KIIDARA ambao uko kisheria. Mambo mengi yalikuwa yanamulikwa, ndiyo maana kuna mipaka hata yeye na UFISADI wake alikuwa anaogopa kuivuka. Mzee JPM, kaanzisha TASK-FORCE, zina watu lakini wengi siyo PROFESSIONAL and SEASONED-VETERANS. Tatizo ni kwamba ukiwataka PROFESSIONALS unakuja kuambiwa wengi wanafahamiana, au wengi walienda mafunzo kambi moja, au wengi walifanyiwa mafunzo na kuingizwa kwenye taasisi na WANAMTANDAO waliowahi kuwepo ndani TAASISI.

MATOKEO ni NINI ??? Oparesheni nyingi zinaanza kufanywa kiholela kwasababu kwanza kabisa hazina wataalamu ambao wengi wangeweza kuuliza maswali, kutoa ushauri wa kitaalamu, au hata kukataa kufanya mambo ya ajabu. Lakini pili, kwasababu hakuna sheria inayounda TASK-FORCE wala kuzisimamia kila kitu kinakuwa ni halali. Wengi wataua watu, watateka na kutesa watu bila hata sababu zisizo za msingi.

Chanzo chote cha haya ni MTANDAO ambao umevuruga nchi na kujipenyeza kila sehemu na kumsababishia Mzee JPM awe na hofu muda wote (Paranoia). JPM alikosea na kiukweli mbali na kufanyiwa hujuma, huyu Mzee wetu alikuwa ni mtu mwenye tabia ngumu tangu uwaziri. Tunaweza kusema kuna baadhi ya maadui aliwatengeneza bila ulazima wowote ule. Angekua ni mtu mwenye kutuliza kichwa, sidhani kama MTANDAO wangemshinda.

Kiufupi, alichokifanya Mzee JPM na TASK-FORCE zake, hakina utofauti sana na kile ambacho Marehemu Mzee Jiang Zemin wa Uchina alikifanya mwaka 1999 kwa kuanzisha OFFICE 610, ambapo alishawishi CHAMA CHA KIKOMUNISTI kwamba waruhusu ianzishwe ili kupambana na makundi hatari kama The Falun Gong, nje kabisa ya mfumo wa Guaonbu (THE MINISTY OF STATE SECURITY).

Katika hili alifanikiwa mno, sema tatizo ni kwamba OFFICE 610, ilianza kutumika vibaya na MTANDAO wa Jiang Zemin a.k.a The Shanghai Clique ambao ulikuwa umejaa watoto wa vigogo (Princelings) kama Bo Xilai ambao walitumia OFFICE 610 kupata Uraisi, hadi mwaka 2012 kudiriki kutaka kumzuia Raisi Xi Jinping asiapishwe kwa kusambaza vikosi vya majasusi zaidi ya 15000 na askari zaidi ya 80,000 waliopo Tibet na Xi Njian wakisingizia kufanya mazoezi.

Hivyo TASK-FORCE zinasaidia, lakini bila usimamizi mzuri chini ya watu aina ya Bashite na Mafwele zinaweza kuvuruga kabisa mchakata wa kiutawala ndani ya nchi hasahasa pale zinapokuwa tayari kubwa na zenye askari wengi na rasilimali nyingi. Tulipofika, haitakiwi TAASISI yoyote ya kiusalama kufanya jambo kubwa bila usimamizi wa kisiasa (Civilian Oversight).

Bahati mbaya sana sasa, Raisi Samia kaingia Ikulu na amegundua kwamba kuanzisha FORCE-WITHIN A FORCE a.k.a TASK FORCE zina manufaa mengi kisiasa hasahasa pale unapotaka mambo yake yaende haraka, bila usimamizi wowote ule wa kisheria (Legal Scrutiny) na ushahidi (Incriminating Evidence). Mbali na NIDA+CCM+NEC kuwa na hatihati ya kumnufaisha Raisi Samia, hiyo mifumo ya FORCE-WITHIN A FORCE a.k.a TASK FORCE ambao ulianzishwa na Mzee JPM kupambana na MTANDAO, leo hii unatumiwa na MTANDAO kupambana na WATANGANYIKA.

RAI YANGU: Watanzania tusikubali TAASISI za kiusalama zitumike kisiasa bila kuwawajibisha viongozi wanaofanya hivyo. Lazima tufuate KANUNI, ili kuzuia madhira kama haya yanayolikumba hili taifa letu. Leo hii kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaweza wakakuchukia tu, na wakaamua kupiga simu moja tu kwa hawa watu wa TASK-FORCE na tusikuone tena mtaani.

Pia mara nyingine unaweza ukalaumu Polisi, Maafisi na Wanajeshi kwamba kwanini mnafanya mambo kinyemelea na kihuni bila weledi wowote ule, bila kufahamu ukweli ni kwamba ndani ya taasisi zao kuna vikosi maalumu (TASK-FORCES) zinazofanya kazi za wanasiasa bila kuwa CIVILIAN AUDITED, tena vimejaa maofisa ambao hawana ujuzi wala uzoefu mkubwa.
​
Makosa yalifanyika kipindi Cha Magufuli na lengo lake hakutaka process. Mzee alipenda sana short na kiukweli alifanya hii section (Security Unit) ikawa dhaifu kwa sababu aliamini Kila kitu kutoka kwenye Task force yake of which hawakuwa na experience ya kutosha maana wengi wao ni wale Juniors waliopata kazi kipindi chake.

So tunatokaje Mkuu hujasema?
 
Utofauti mkubwa uliopo baina yangu na wewe, ni ule uliokuwepo baina ya CICERO na MARK ANTHONY. Cicero aliamini katika Rumi kama Jamhuri ambayo inaongozwa kwa katiba, taratibu na bunge. Mark Anthony akiwa mfuasi mkubwa wa Julius Ceaser aliamini katika mtu, siyo katiba, taratibu na bunge, kwamba mtu maadamu ni Benevolent Dictator basi aachwe afanye chochote kile bila kuangalia madhara kwa vizazi vijavyo.

Jean Monnet aliwahi kusema hivi "For things to work, we need people" but "For things to last we need institutions". Mzee John Pombe Magufuli alipofanya mazuri nilimsifia, na alipokosea nilimsema waziwazi. Kwenye suala zima la MAKINIKIA na STIEGLER's GORGE mpaka siku ya kufa kwangu nikasema kwamba Mzee JPM alipatia sana na historia itamtetea.

Ila hili la kuamini kwamba alipatia kila kitu, na kwamba baadhi ya tabia zake za kidikteta zilianza punde baada ya kuwa Raisi na kuonewa na WANAMTANDAO limenishangaza sana. Ni kweli MTANDAO ulimhujumu Raisi Magufuli, Ni kweli MTANDAO ulimfanyia vibaya, lakini tabia zake nyingi alitoka nazo chini. Hivi kilichomtuma Raisi Magufuli na watu wake kumshambulia Lissu kilikuwa ni MTANDAO au hulka binafsi ??? Vipi kuhusu Ben Saanane, do you think he deserved that ???

Kuhusu Lissu, binafsi nazifahamu hulka zake tokea Ilboru na hawa waliosoma naye Magroup ya WhatsApp huzungumza mengi. Binafsi kuna tabia zake huwa sizikubali kabisa, tena nachelea kusema kwamba kama akiwa Raisi kwa katiba kama hii, yeye naye lazima atateleza tu. SISI NI BINADAMU, we are not GOD who is beyond reproach.

UNAAMINI WANASIASA ??? Good for you, kila la kheri.
​
Nyinyi wazee bhana...

Story nyingi ila mnashindwa kuutumia usomi wenu wakati sahihi...
 
Makosa yalifanyika kipindi Cha Magufuli na lengo lake hakutaka process. Mzee alipenda sana short na kiukweli alifanya hii section (Security Unit) ikawa dhaifu kwa sababu aliamini Kila kitu kutoka kwenye Task force yake of which hawakuwa na experience ya kutosha maana wengi wao ni wale Juniors waliopata kazi kipindi chake.

So tunatokaje Mkuu hujasema?
Tanganyikans are not ready for this type of conversation/discourse. YET​
 
3. MABADILIKO YA KIHUNI YA SHERIA YA USALAMA WA TAIFA MWAKA 2023
Raisi Samia na Saidi Massoro (DGIS) walipitisha mabadiliko makubwa ya sheria ya TISS. Sheria haikujadiliwa na ilipitishwa saa kumi na moja jioni mwaka 2023 kihuni-huni tu. Wengi hatufahamu madhara ya yale mabadiliko na nini kilipekea kuwa hivyo.

Kama nilivyosema hapo awali, kwamba taasisi za kiusalama zina COMPARTMENTALIZATIO na CIVILIAN OVERSIGHT. Hapa kwetu mabadiliko makubwa yalifanyika mwaka 1996 na wengi walidhani na kuboresha taasisi, lakini ukweli wengi tunaufahamu chanzo kilikuwa nini.

TISS ACT 1996, inatoa CIVILIAN OVERSIGHT kwamba, TAASISI itakuwa chini ya WAZIRI WA NCHI MWENYE DHAMANA YA OFISI YA RAISI. Lengo hili ni zuri kabisa kwamba hata kama TAASISI ni chombo cha kiusalama ni lazima wawakilishi wa wananchi wasimamie (Supervisory Role) ili kuweza kujenga daraja baina ya UTAWALA WA KIRAIA na WATENDAJI WA KIUSALAMA.

Uratibu wa mikakati yote ni lazima ufanywe na WAZIRI, KATIBU MKUU KIONGOZI na MKURUGENZI wanafanya kazi kwa pamoja katika kusimamia TAASISI, hasahasa kwenye mambo ya utekelezaji wa majukumu na utekelezwaji wa sera. Hawa WATATU ndiyo WASHAURI WAKUBWA WA RAISI, mbali na BARAZA LA USALAMA.

Ila sheria ya TISS 2023, inawaondoa WAZIRI na KATIBU MKUU KIONGOZI (KMK) na kumuacha DGIS na PRESIDENT tu kama waratibu wakuu wa utendaji wa majukumu wa TAASISI, pamoja na utekelezwaji wa sera. HILI NI JAMBO LA HATARI MNO. Ila wengi wetu pia tunafahamu kwamba pamoja na sababu nyingine luluki, tunamuondoa KMK ambaye ndiye MWAJIRI MKUU WA SERIKALI kwenye UTUMISHI WA UMMA kwasababu ya yale yaliyotokea 2021.

Kiukweli, jambo ambalo WATANGANYIKA wengi huenda walikuwa hawalifahamu KISHERIA ni kwamba KATIBU MKUU KIONGOZI ana nguvu kuliko MAKAMU WA RAISI na WAZIRI MKUU (De Facto). Ni nafasi ambayo miaka mingi ilikuwa haionekani sana, lakini baada ya Mzee JPM kufariki, ndiyo watu wakafahamu kwamba, oooh kumbe KMK ndiye De Facto President.

Baada ya msiba wa Mzee JPM, kama tungekuwa na KMK mwenye hulka ya watu kama Benard Membe, sidhani kama leo hii Raisi Samia angekuwa hata ni Raisi. AU nchi ingekuwa imeingia kwenye machafuko tayari. Dr. Bashiru Kakurwa mbali na udhaifu wake mwingi alienda taratibu. Ninapishana na Bashiru kwenye mengi, lakini katika hili nachelea kusema angekuwa mtu mwingine nina uhakika tungekuwa tunazungumza mengine. NDIYO MAANA MZEE KIJAZI alitangulia mbele ya haki mapema kabisa.

KATIBU MKUU KIONGOZI, hapo zamani alikuwa na kazi za kusimamia utakerezaji wa shughuli za TAASISI kwasababu yeye ndiye MWAJIRI MKUU UTUMISHI WA UMMA. TAASISI iko chini ya OFISI YA RAISI hivyo wao ni WATUMISHI WA UMMA. KMK alihusika na masuala yao mazima ya mishahara na fedha za oparesheni, akishirikiana na WAZIRI na MKURUGENZI. Kiuhalisia hata leo WAZIRI MKUU amfukuze kazi mtumishi wa umma, KMK akimrudisha WAZIRI MKUU hawezi kufanya lolote lile.

Kubwa zaidi, KMK ndiyo CHIEF COORDINATOR-STATE HOUSE, maana yeye ndiyo KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI , lakini pia ndiyo CHAIRPERSON OF INTER-MINISTERIAL TECHNICAL COMMITEE, chombo kinachotumika kuandaa miswada yote muhimu kabla ya kwenda BARAZA LA MAWAZIRI na BUNGENI. Nafasi hii inamsaidia kufahamu wapi panahitaji usimamizi wa haraka (Security Intervention) ya TAASISI. Hili litasaidia kuhakikisha kwamba TAASISI ZA KIUSALAMA zinafanya kazi kutokana na uhitaji tu na malengo ya kitaifa.

Kumuondolea nguvu KMK kisa kuogopa kutokea kwa Dr. Bashiru Mwingine endepo Raisi atakuwa hayupo ni jambo la hatari na linaturudisha kulekule kwa kabla ya 1996 ambapo TAASISI ilikuwa ni IDARA ndani ya OFISI YA RAISI. Ambapo watu waliilalamikia mno kwa kuendeshwa kihuni kwasababu ilikuwa inawajibika kwa Raisi tu, na haina uangalizi wowote ule. Sasa baada ya taharuki za General Imran Kombe na CCM ikabidi ipitishwe Sheria 1996 kuwadhibiti.

Hii sheria ya TISS 2023, inaturudisha nyuma tena. DGIS na PRESIDENT ndiyo waamuzi wa kila kitu. Hivi kiukweli unaamini TAASISI ambayo imeshakuwa kubwa vile, isipokuwa chini ya usiamimizi wa walau watu wawili mtapata matatizo. DGIS na watu wake wa TISS wanaweza wakawa na taarifa nyingi za kiserikali lakini siyo katika ngazi ya kuweledi. KMK yupo kwenye BARAZA, BUNGE, na UTUMISHI WA UMMA hivyo yeye ni lazima atakuwa na nafasi nzuri ya usimamizi kuliko RAISI, WAZIRI na MKURUGENZI.

Nikupe mfano: Taifa la Uchina lina taasisi ya UJASUSI iitwayo GUOANBU (MINISTRY OF STATE SECURITY). Hii taasisi tofauti na kwetu siyo shirika au idara, bali ni WIZARA kama nyingine na ina WAZIRI WAKE. Mbali na huu ukubwa, hadi Central Inelligency Agency (CIA) na Secret Intelligence Service (SIS/MI6) wanasema ni moja kati ya taasisi TOO PROFESSIONAL hapa duniani.

Usimamizi wa GUOANBU haufanywi na WAZIRI tu, ambaye pia ndiyo MKURUGENZI, bali taasisi ina WAKURUGENZI WAWILI. Mkurugenzi wa kwanza ndiyo TECHNICAL DIRECTOR, anayesimamia shughuli za siku kwa siku za WIZARA. Mkurugenzi wa pili ni POLITICAL COMMISSAR anayehakikisha kwamba GUOANBU inafuata sera na malengo ya CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA UCHINA.

Mbali na hawa wawili, GUOANBU iko chini ya BARAZA LA MAWAZI kwasabubu nayo ni WIZARA. Huu URASIMU unaweza kuonakana hauna maana, lakini unasaidia taasisi za kiusalama za UCHINA kutumika kihuni na kikundi fulani kwa malengo yao binafsi kinyume na nchi.

SWALI LA KUJIULIZA: Ni kwanini WANAMTANDAO waling'aka sana baada Mzee Mkapa kumteua Marehemu Mzee Hassy Kitine kuwa WAZIRI OFISI YA RAISI anayesimamia IDARA YA USALAMA ??? Kweli alitumia fedha vibaya, lakini kwanini kina Benard Membe walilishadadia sana lile suala ??? Jibu, ni rahisi tu. Angeendelea kuwepo hadi 2005, ingekuwa ni nguvu kwa MTANDAO kuchezea TAASISI wanavyojitakia.

KWAHIYO SASA: Tuna TASK-FORCE inayofanya kazi nje ya usimamizi wa kawaida, ambapo hata baada ya haya mambo, hakuna ushahidi wowote wa utekwaji, uuaji na matumizi mabaya ya madaraka. Ila kubwa zaidi DGIS na RAISI ndiyo wanaamua kila jambo kuhusu UJASUSI bila kuwajibika kwa mtu yoyote yule. Kiufupi, TAASISI inaongozwa na DGIS peke yake tu ambaye anaweza kujiamulia lolote lile kwenye bajeti na mwelekeo wa TAASISI na asiambiwe lolote lile.

Mkipata mtu mbaya hapa, ambaye anatumika na MTANDAO au watu wasiolitakia mema taifa letu, TAIFA NDIYO KWAHERI hivyo. Sasa jiulize tu, kama Raisi hawezi kuamrisha TPDF au POLISI TANZANIA bila ruhusu ya BUNGE, kwanini aachiwe atumie TISS ambalo kiuhalisia ni jeshi, bila idhini ya BUNGE pia ???? TAFAKARI SANA...

ZINGATIA HILI: TISS ACT, 2023 imewapa maafisa kinga (IMMUNITY FROM PROSECUTION) hivyo hata wakituumiza WATANGANYIKA hawafanywi lolote lile. Ila jambo baya zaidi ni uwezo wa kutembea na silaha (Fire Arms) moja kwa moja, jambo ambalo nalo ntalizungumzia siku ingine panapo majaaliwa.
​
Umetumia neno Tanganyika lakini kwenye segments zote 1 mpaka 3 umeshindwa kuiweka bayana Tanganyika!
Wahuni wanapenda Tanganyika ipotee ili watumie rasilimali zake kujineemesha!
 
Nakubaliana na wewe kwamba WATANGANYIKA inabidi TUUNGANE.

Kila mtu asimame kutetea nchi katika nafasi yake. Nathamini sana mchango wa Humphrey Polepole, nathamini sana mchango wa Maria Sarungi, nathamini sana mchango wa Mange Kimambi, nathamini sana mchango wa Evarist Chahali na nathamini michango ya watu mbalimbali mitandoani na kwenye vyama vya siasa.

Jambo moja tu ambalo sitalichanganya ni lile la kuamini kwasababu anazungumza kichagga basi ni lazima huyu atakuwa ni Mchagga. Tuna kasumba mbili kubwa kwenye siasa zetu. Mosi, kuamini kwamba kila anayezungumza lugha sawa na sisi au kufanana na sisi basi ni mwezetu. Hili lilimgharimu sana Mzee Nyerere hata kwenye diplomasia ya nchi. Hili limebaki hadi kwetu, WATANGANYIKA tunaamini kwamba kila mtu anawaza mema kama sisi na ana moyo mkunjufu kama sisi.

Huwa yanatukuta tukiwa tumeshachelewa mno, ndiyo tunazinduka usingizini kwamba kumbe huyu hakuwa mwenzetu.

Pili, ni kutopenda kuwajibika kisiasa hata pale ambapo ni dhahiri tumefanya makosa makubwa yanayoonekana. Tunakarisika kabisa tukiambiwa ukweli. Ndiyo maana hadi leo hii Mzee Nyerere alifanya makosa na wengi hatupendi kuyaanisha hayo makosa ili tujifunze, tunaishia kujificha kwenye kivuli cha NIA NJEMA. AU kisipokuwa hicho tutasema ni hujuma za MABEBERU. Nothing is ever our fault. Sasa huu utamaduni wa kutopenda KUWAJIBIKA usipojengwa hapa nchini, tutakuwa na hali mbaya hata kama wapinzani watachukua nchi.

Sasa basi mimi naungana na wote wanaosema ukweli. Lakini sitajiingiza kwenye dhambi ya kuamini kwamba wote wanaipenda TANGANYIKA wala kuiwazia mema. Umri nilio nao unatosha kunifundisha mengi kuhusu siasa za Tanzania.
​
Uwajibikaji utakuja wakati wa kuunda mifumo mipya, katiba mpya, nchi mpya.

Nyerere, JPM, Lissu kama binadamu kuna makosa walifanya na kuna mazuri mengi sana wamefanya.

Moja la kosa la Nyerere ni muundo wa huu Muungano na hii Katiba.

Moja la kosa la JPM ni kukubali Samia awe msaidizi wake, kuwaacha baadhi ya wanamtandao, kwenye nafasi nyeti.

Moja la kosa la Lissu ni kumkubali mwanamtandao Lowassa kuwa Mwenyekiti wa Chadema ni sawa na kumchukua Samia awe mwenyekiti wa Chadema mtu uliyetumia miaka kumi kumpinga na kumuita Fisadi au kukubali kila alichosema Mbowe hadi pale Mbowe alipotaka kumuweka Lissu pembeni ndio Lissu akashtuka.

Sina shaka Nyerere, JPM walikuwa wazalendo. Lissu, Polepole ni wazalendo na wana nia ya dhati kulikomboa hili Taifa kutoka kwa hiki kikundi cha wanamtandao.

Hii inaonyesha hakuna yoyote mkamilifu aliyewajibika kwenye nafasi yake huko nyuma kwa asilimia 100%. Watu wanajifunza kutokana na makosa yao. Lissu au Polepole wa miaka kumi iliyopita sio sawa na Lissu, Polepole wa leo.

Kwenda mbele nakubaliana na wewe tuweke misingi ya uwajibikaji, kama kuondoa kinga kwa wananchi wote including Rais. Mafisadi wote kufikishwa mahakamani na mali zote zilizopatikana kwa ufisadi kurudishwa kwenye mikono ya umma. Wezi, mafisadi, watekaji kuwekwa wazi na kufikishwa mahakamani na kupewa hukumu stahiki.
 
Kwa sisi tuliosaiti walalahoi na ndiyo waliowengi hawajui nini kinachoendelea nchini na wala hawajui Tanganyika na Zanzibar zimeungana.
Mawazo yangu bila Traole wa Tanzania kizazi chetu kitaondoka tutaacha hakuna mabadiliko
 
Ila sheria ya TISS 2023, inawaondoa WAZIRI na KATIBU MKUU KIONGOZI (KMK) na kumuacha DGIS na PRESIDENT tu kama waratibu wakuu wa utendaji wa majukumu wa TAASISI, pamoja na utekelezwaji wa sera. HILI NI JAMBO LA HATARI MNO.
Aisee, hii sikuwa naijua. Nilijua nikulinda wanataasisi dhidi ya madhara yatokanayo na Kazi zao.
 
Congratulations, you have escaped the matrix of intellectual lobotomy.

Kuna mtu aliwahi kusema humu ndani kwamba Tundu Lissu is an upgrade of John Pombe Magufuli with bugs fixed. Alikuwa sahihi mno. Lissu kama John, wote ni watu wenye akili nyingi mno (Highly Intelligent), wana tatizo la sifa (Egotistical), wote hawawezi kutawala hisia zao (Lack of Emotional Stamina), waropokaji (Loose lips) na hawana uwezo wa kupembua nyakati (Lack of discernment). Sina shaka na uzalendo wao hata chembe, wala utendaji kazi wao.

Tatizo ni kwamba kuwa kiongozi mzuri inahitaji zaidi ya kuwa BOOK-SMART. Inahitaji mtu uwe unaweza kusoma alama, nyakati na majira. Ni lazima ujifunze mambo ya msingi kuhusu utawala (State-Craft), kama ifuatavyo:

Mosi, kuna vita nyingine unashinda kwa kushindwa.
Pili, kunyamaza kimya saa nyingine siyo udhaifu bali ni busara na mkakati-vita.
Tatu, Vita zote kubwa duniani huwa zinapiganwa kwenye gizani kusipoonekana.

Ndiyo maana hata unapomfundisha mtoto kucheza CHESS ni lazima umwambie kwamba kuna sehemu lazima akubali PAWNS waliwe ili KING au KNIGHT aweza kuzunguka vizuri kwenye ubao. Ukishafahamu kwamba dunia hii inatawaliwa na watu waovu basi ni lazima utahitaji kuwa mtawala wa aina yake. KARATA ZOTE HAZIWEKWI JUU. Tanzanians are also not ready for this conversation.
​
Kuhusu Lissu kuwa mropokaji hilo nakataaa. Tena Lissu anamzidi sana Magufuli kwa sababu Lissu anapenda mapambano ya hoja. Lissu ni mwanademokrasia kweli na haamini kwenye kumuumiza mtu ili hoja yake ipate nguvu.
 
Back
Top Bottom