Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Uwajibikaji utakuja wakati wa kuunda mifumo mipya, katiba mpya, nchi mpya.

Nyerere, JPM, Lissu kama binadamu kuna makosa walifanya na kuna mazuri mengi sana wamefanya.

Moja la kosa la Nyerere ni muundo wa huu Muungano na hii Katiba.

Moja la kosa la JPM ni kukubali Samia awe msaidizi wake, kuwaacha baadhi ya wanamtandao, kwenye nafasi nyeti.

Moja la kosa la Lissu ni kumkubali mwanamtandao Lowassa kuwa Mwenyekiti wa Chadema ni sawa na kumchukua Samia awe mwenyekiti wa Chadema mtu uliyetumia miaka kumi kumpinga na kumuita Fisadi au kukubali kila alichosema Mbowe hadi pale Mbowe alipotaka kumuweka Lissu pembeni ndio Lissu akashtuka.

Sina shaka Nyerere, JPM walikuwa wazalendo. Lissu, Polepole ni wazalendo na wana nia ya dhati kulikomboa hili Taifa kutoka kwa hiki kikundi cha wanamtandao.

Hii inaonyesha hakuna yoyote mkamilifu aliyewajibika kwenye nafasi yake huko nyuma kwa asilimia 100%. Watu wanajifunza kutokana na makosa yao. Lissu au Polepole wa miaka kumi iliyopita sio sawa na Lissu, Polepole wa leo.

Kwenda mbele nakubaliana na wewe tuweke misingi ya uwajibikaji, kama kuondoa kinga kwa wananchi wote including Rais. Mafisadi wote kufikishwa mahakamani na mali zote zilizopatikana kwa ufisadi kurudishwa kwenye mikono ya umma. Wezi, mafisadi, watekaji kuwekwa wazi na kufikishwa mahakamani na kupewa hukumu stahiki.
Kosa kubwa la Magufuli lililo zamisha nchi no kumteua Mama Samia awe Makamo wa Raisi, na Watoto wa Jpm nao sijui walikua wapi kumsanua Baba yao, Mimi nigekua Mtoto wa Magufuli ningemwambia amtumbue Samia na amateur Hussein Mwinyi kidogo tungepona, Sijui Magufuli alikua akai vikao na Watoto wake na Mke wake ili kupata Maoni yao, Kuna muda Mzazi lazima uweke kikao na familia mnakuta sitting room mnaongea na kuwasikiliza watoto maoni yao kuhusu Serikali yako na Wasaidizi wako.
 
Naunga Mkono hoja zako nyingi, lakini Mimi ni muumini wa serikali moja nchi moja. Ukweli siungi Mkono serikali Tatu!!!

Binafsi, kwa mtazamo wangu, kuidai Tanganyika ni kuvunja Muungano. Na hapo ni kutangara serikali mbili za nchi mbili. Hapa kikubwa tuelekee serikali moja Nchi moja!
Mkuu serikali ni Mbili na siyo Moja na Zanzibar wananufaika na Muungano kwa % 100 kama Rais akiwa Mzanzibar. Zanzibar wana bajeti yao nje ya Muungano na Kwasasa Mama Samia anachota pesa ana jenga Hospital na Mashule na Barabara kwakutumia pesa za Watanganyika. Yani Wizara ya Ujenzi ya Zanzibar inatengewa Bajeti yake kutuka kwa Mama Samia na inapewa pesa tena na Serikali ya Zanzibar, Ni sawa Mkoa wa Arusha uwe na Bajeti yake itokanayo na Makusanyo ya kodi na Mapato mengine ndani ya mkoa na iwe inapewa pesa kutoka Wizara ya fedha kwaajili ya Maendekeo.
 
BOOKMARK THIS: Ndugu Humphrey Polepole na Ndugu Tundu Lissu hawapikiki chungu kimoja. Kuanzia KIFIKRA, KIITIKADI na KIMALENGO. Atakapotoka nje, Tundu Lissu ambaye anataka kuitoa CCM madarakani ndiyo tutafahamu kwamba kweli Ndugu Polepole anataka nini.

Mpaka sasa nitaendelea kumsikiliza, maana baadhi ya mambo anayoyasema yana ukweli nusu-nusu. MOST OF YOU ARE NOT READY FOR THIS DEBATE.
​
Hapa ni wenye jicho la 3 pekee ndio watakuelewa na hii pia ni kete ya Wanamtandao kama wakiwahi mapema Lissu anaaminika na hana historia yenye makandokando kwenye siasa , Lissu ni kete ya turufu kwa Wanamtandao , Polepole na kundi lake pamoja na Wazalendo ndani ya mifumo ya nchi , kiufupi Lissu kaibeba nchi mabeganj
 
Uzuri wote wanaonitukana mpaka sasa hakuna anayekanusha kwamba nilichokisema kina UKWELI na UHALISIA. Ndiyo hapa narudi kwenye usemi ule-ule, WATANGANYIKA ni watu wepesi mno kuhadaiwa kisiasa. SHERIA na KANUNI ndiyo mwongozo mkuu wa msomi yoyote yule, hasahasa kwenye nyakati hatari kama hizi:

SULUHISHO LA NDUGU HUMPHREY POLEPOLE KWA MATATIZO YA NCHI:
CCM isimruhusu Samia Suluhu kugombea Uraisi a.k.a imwage Oil. CCM ifanye mjadala na CHADEMA na kumtoa Lissu gerezani ndipo tufanye uchaguzi mkuu. Polepole anaamini kwamba CCM kwanza nchi baadaye, yaleyale mawazo ya Mzee Nyerere kwamba TANZANIA IMARA= CCM IMARA

SULUHISHO LA NDUGU TUNDU LISSU KWA MATATIZO YA NCHI:
Tundu Lissu anaamini hivi, KATIBA IMARA = TANZANIA IMARA. Ambapo anasema kabla ya kufanya chochote kile ni lazima nchi ifanye mabadiliko makubwa kisheria na kimfumo.Turekebishe katiba, tuamue hatma ya muungano, tuwe na tume huru, kisha tukafanye uchaguzi mkuu.

HAYA MAWAZO NI MAWILI TOFAUTI, KISHERIA NA KIMATOKEO. Mtu yoyote yule mwenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo mtambuka kwa kina lazima ataona utofauti. Kuna wengine wanataka tu RAISI SAMIA atoke, akishatoka wao ni CCM kindakindaki. Kuna wengine wanataka RAISI SAMIA atoke, na CCM pia itoke, hawa ni wapinzani kindakindaki wanaotaka dola.

MIMI BINAFSI NAONA JAMBO JEMA NI HILI:
Mabadiliko ya kisheria lazima yafanyike. Wanasiasa wote (CCM + CHADEMA) ni lazima wadhibitiwe ili mambo haya yasije kujirudia hapa TANGANYIKA endapo hata siku CHADEMA wakachukua nchi. Kubwa zaidi, ili kuzuia uvunjifu mkubwa wa haki za raia, unadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ni lazima tuunde TRUTH COMMISSION, ambayo itachunguza maovu ya serikali tokea awamu ya kwanza na kuwajibisha watu.

TRUTH COMMISSION itatusaidia kufanya VICTIM REPARATIONS, jambo ambalo ndiyo msingi mkuu wa taifa lolote lile linalotaka amani ya kisiasa (Transional Justice). Kuna maelfu ya watanganyika wenzetu waliuwawa kikatili, waliwekwa kizuizini, walifutiwa uraia, wakafukuzwa nchi, wakafungwa, wakafilisiwa na hata kuuwawa na serikali chini ya mwamvuli wa UZALENDO. Hawa ni lazima wapewa haki yao, aidha wakiwa hai au wafu.

TRUTH COMMISSION pia itatusaidia kufanya INSTITUTIONAL REFORMS. Vyombo vya kiusalama vitatakiwa kufanyiwa marekebisho ili mwanasiasa yoyote, ikiwemo Tundu Lissu wasije wakajisahau endapo watakuwa ikulu na kugeuka MIUNGU WATU.

MTAZAMO WA MBALI KABISA: Tatizo siyo watu peke yake. Matatizo ya Tanzania hayawezi kumalizwa kwa UCHAGUZI NA TUME HURU peke yake. TATIZO LETU KUBWA ni SHERIA NA MFUMO mbovu uliozalisha TAMADUNI ZA HOVYO ZA KISIASA. Mzee Mkapa alikuwa kiongizi safi wakampa jina MR CLEAN, lakini alifanya mambo mabaya mangapi ???

IFIKE MAHALI TUWE WAELEWA
​
Umeandika vizuri sana lakini unasisitiza sheria na kanuni tuzifuate. Je, kwa unavyoona muelekeo wa nchi na viongozi tulionao kweli kuna sheria zitafuatwa??

Hebu weka solution ya kudumu ambayo itasaidia hao watu wafate kanuni ili hata siku chama chochote au mtu yeyote akikabidhiwa funguo za ikulu asiende kinyume na sheria na kanuni..!!
 
Hapa ni wenye jicho la 3 pekee ndio watakuelewa na hii pia ni kete ya Wanamtandao kama wakiwahi mapema Lissu anaaminika na hana historia yenye makandokando kwenye siasa , Lissu ni kete ya turufu kwa Wanamtandao , Polepole na kundi lake pamoja na Wazalendo ndani ya mifumo ya nchi , kiufupi Lissu kaibeba nchi mabeganj
Kwenye Movie tunaita Stering
 
Ndio tatizo la kuajiri wasomi watupu eti wanaendana na tecnolojia. Ndio maana ule yzalendo nidhamu au woga wa kazi haupo .
Hivi leo hii mtu mwenye digree yake kitengoni umwambie ajifanye chizi au awe mfagia barabara ili tuu kukusaya data atakubali? Pamoja na hayo kwa sasa idara iliishia kwa kikwete ile inteku yake ya mwisho hawa wengine wanaoingia siku hizi wako kimaslahi sana hana mwaka kazini lakina kafurumusha majumba ya kupangisha magari kibao ya dhamani.
Kwa kifupi kwa sasa uzalendo hakuna
 
MAMBA HUWA ANA NGUVU AKIWEPO NDANI YA MAJI TU.

TAASISI zote za kiusalama duniani kote zina kitu kiitwacho INTEREPOLABILITY. Ambapo mafanikio ya kazi ya JASUSI X inategemea mafanikio ya kazi ya JASUSI Q, tena huenda hata hawafahamiani, wala hawaji kufahamiana. TAASISI haifanyi kazi ikitegemea MTU, bali watu ambao wakiwa wengi hutengeneza MFUMO ambao huwa unakuwa na lengo moja.

Wewe hata uwe JASON BOURNE, JAMES BOND au JACK RYANA usipokuwepo ndani ya MFUMO, huna utofauti wowote ule na MAMBA aliyepo nje ya MAJI. Ndiyo maana hata unapostaafu kuna baadhi ya SECURITY CLEARANCES unabaki nazo, kwasababu wewe umuhimu wako kwa MFUMO utaisha siku pale unapofariki tu.

Sasa wakitaka kukushughulikiwa, kwanza kabisa wanafanya REVOCATION OF SECURITY CLEARANCES, aidha kwa kukataza USIPEWE TAARIFA MUHIMU, au KUPANGARUA BAADHI YA IDARA kwa kuhamisha watu, kuwapa teuzi, kuziunganisha idara (Merger), kuiweka idara moja chini ya nyingine (Subordination) au kuua watu muhimu kwenye idara. Wakishakufumba macho hivi, aidha wanabana fedha zako au wanakuua.

Mataifa mengine, kama UCHINA na URUSI njia yao ni MOJA TU ambayo kwangu mimi naamini ITS THE MOST EFFECTIVE METHOD. Unawapa majasusi "The Scarlet Letter", ambayo itakuhakikishia A CLEAN SLATE, ya kuanza upya. Sema ndiyo hivyo hapa Afrika Mashariki aliyeweza kutoa The Scarlet Letter ni General Paul Kagame tu, ndiyo maana Rwanda mbali na ujinga wa UKABILA, mambo yanaenda.


====================================================
Kule Rumi ya Kale (Ancient Rome) vyombo vya usalama vilikuwa vina adhabu iitwayo DECIMATION, ambapo wanajeshi walikuwa wanagawiwa katika vikosi vya MAKUMI, MAMIA na MAELFU. Tatizo likitokea kwenye kikosi moja unamchukua kiongozi wao unamuambia awaambie wenzake wale tisa wamuue wa kumi. Au wale tisini wawau wale kumia. Au mia tisa wawaue wale mia.

Hili lilileta heshima mno kwa majeshi ya Warumi ambapo wakubwa wa vikosi walifahamu fika kabisa, tukileta uzembe tutaambiwa tuue wenzetu wa kikosi kimoja ambao bahati mbaya sana walikuwa ni watoto wao, wakwe wao au ndugu zao. Hata MONGOLS jeshi lao lilikuwa na nidhamu kwasababu ya adhabu ya DECIMATION.

Ukiisha ingia kwenye vyombo ya usalama ni lazima uwe na nidhamu. Nchi ambayo maafisa wake hawana nidhani huwa haidumu muda mrefu. Hawa watu huwa wanapewa mafunzo, wanafahamu siri na kudekezwa kama mayai kwa mishahara na marupurupu. Wanapoharibika na tamaa, hakuna njia ya kuwarudisha kwenye mstari zaidi ya kuwapeleka mapema ahera.

TANZANIA ilipofika, ili kuokoa nchi ni lazima TUCHUKUE MAAMUZI MAGUMU bila kuonesha hata CHEMBE YA HURUMA, wala SONI. WEWE ambaye umesomeshwa kwa hela za walipa kodi, ukawa hadi Balozi, watoto wako wako International Schools halafu ukasaliti kiapo chako, ulitegemea kitokee nini ??? A Bullet at the back of your head or A Noose around your neck.
​
Samahani vichwa kama hivi halafu bado nchi Iko matopeni ni ajabu sana unaandika na kutoa majawabu hadi nakutamani , HONGERA SANA NDUGU
 
UTANGULIZI:
Habari ndugu MTANGANYIKA, leo ni mambo mengi kweli ya kusema ambayo yanatatiza sana moyo wangu. Nimejaribu kuandika wiki kadhaa lakini naishia kufuta kila nikimaliza kuyaaandika. Mengine nikiyasema hadharani yanaweza kuwaumiza sana moyo na mkaishia kukata tu, tamaa. Ila itoshe kusema kwamba TANGANYIKA ISHAUZWA.

1.TANGANYIKA KUTETEWA NA WANAHARAKATI WALIOWAHI KUTUHUJUMU:
Ndugu Humphrey Polepole na pamoja na wanaharakati wengine wa mtandaoni kama Mange Kimambi na Maria Sarungi, watu ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kuwa wanufaika wa mfumo na hata kutumika kuhujumu wananchi. Mtu pekee ambaye amekuwa akisema ukweli siku zote ni kaka yangu Evarist Chahali (He has been very Consistent and Objective).

Miundombinu mingi ambayo Samia anaitumia kututesa WATANGANYIKA, ilitengenezwa na Raisi John Pombe Magufuli. Humphrey Polepole na Dr.Bashiru Ali Kakurwa walikuwa ni wahandisi wakuu wa kisera. Ilifika kipindi hadi Dr. Bashiru alitamka wazi kwamba CCM inaweza kuvunja katiba ili kubaki madarakani kwasababu ndiyo imeshika dola.

Hawa wengine kama Maria Sarungi, na Mange Kimambi tunafahamu kwamba madai mengi yalianza kama maslahi binafsi. Hasahasa Binti Sarungi ugomvi wake mkubwa na JPM chanzo ni mambo ya kifamilia ambapo yeye kama munfaika wa mfumo alikutwa na SHOCK-THERAPY ya JPM. Alikuwa na mwenzake Fatma Binti Karume, ambaye mlimbatiza jina na kumwita Shangazi, lakini awamu hii rangi zake naye mshaziona.

Mange Kimambi, ni mamluki. Alishawahi kuwa upande wa CCM, baadaye dhidi ya Lowassa, baadaye upande wa Lowassa dhidi ya Magufuli. Baadaye kushangilia msimba wa Magufuli na kumnadi Samia, na saa hizi yuko dhidi ya Samia. WATANGANYIKA hatufahamu kesho atakuwa dhidi ya nani.

Hii dhambi naona inatafuna wengi mno hadi maafisa usalama ambao binafsi nawafahamu waliwahi kuwa mstari wa mbele kutetea kila ujinga unaofanywa na dola, ambapo mamia ya WATANGANYIKA walipoteza uhai, kuumizwa, kufungwa au kufilisiwa. Hata humu JF wengi nawafahamu, naona kabisa mwelekeo wao ni watu aliyepagawa na pepo au kapata wazimu.

WATANGANYIKA, ili kuepukana na kadhia hii ya kubebwa na kila aina ya upepo wa kimaslahi wa watu ni lazima WASOMI wajifunze kusimamia kitu kinachoitwa KANUNI (Principles). Hata pale ambapo mwanasiasa unayempenda anakosea, wewe inabidi uufunde moyo wako kusimamia KANUNI.

RAI YANGU KWA WATANGANYIKA, hasa WANAUSALAMA: Kwenye BIBLIA, Daudi alikuwa ni mtenda dhambi mkubwa kama sisi tu, lakini tunaambiwa ni moja kati ya watu walipata kibali kikubwa sana kwa MUNGU. MUNGU alisema wazi kabisa kwamba anampenda Daudi kwasababu MOYO WAKE HAUNA HILA. Daudi alikuwa ni mtu mwenye kusimamia KANUNI.

Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda amuue Daudi. Mara mbili Daudi alipata nafasi ya kumuua kabisa Sauli, kwa mambo aliyomtendea lakini Daudi alisimamia KANUNI. Alikataa kumuua na kusema HUYU NI MPAKWA MAFUTA WA MUNGU, atamalizana na MUNGU wake.

Daudi alikuwa ni KIONGOZI MKARIMU (Equittable). Kuna sehemu kwenye BIBLIA ilitokea vita, na baadhi ya askari wake walichoka wakashindwa kwenda vitani. Waliporudi na kupata ushindi mkubwa na mali nyingi, kuna baadhi ya askari wakasema hawa ambao hawakwenda na sisi vitani wasipewe chochote kile. Daudi aliwakemea na kusema aliyekwenda vitani, na aliyebaki kulinda mji wote watapata mali sawa. Akimaanisha kwamba kila mtu ana umuhimu ndani ya jamii.

Daudi alikuwa ni KIONGOZI MUUNGWA. Alikosea mno kwa kuiba mke wa mtu na kumpa mimba, huku akimuua mume wake. Baadaye alipofutwa na nabii Nathani kuambiwa ukweli, wala hakutafuta vijisababu, bali alikuwa mpole na kwenda kuomba msamaha mbele ya taifa zima. Hakusema kwamba yeye alikuwa na nia njema, ila alisema wazi kwamba amekosea.

SASA BASI: wale ambao mliwahi kuwakosea WATANGANYIKA, na kusababisha vifo, misiba, umasikinui na majeraha ombeni TOBA KWA MUNGU, OMBENI TOBA KWA WATANGANYIKA, lakini kubwa zaidi TOBA YA KWELI huambatana na mabadiliko ya moyo. Jaribuni kukaa kwenye viatu vya watu kama Wazazi wa Ben Saanane, Familia ya Gwanda, Familia ya Soka, Familia ya Akwilina na wengine kisha mtafahamu kwamba WENGI HAMKUISHI VIAPO VYENU.
​
Ulikuwa na hoja kwenye bandiko lako, lakini limepoteza mantiki baada ya kuingiza aya za Dini!

naamini unaweza kujenga hoja pasipo kuihusisha dini....tusiomini katika dini...andiko lako linapoteza maana!
 
BOOKMARK THIS: Siku Tundu Lissu anatolewa nje, Amin Amin nawaambia, tutafahamu madhambi mengi ya Ndugu Humphrey Polepole ambayo aliwahi kuyafanya. Pia sidhani kama atakuwa na uwezo wa kujibu hoja za Lissu. Wakati hili linatokea, WATANGANYIKA wengi watakuwa washachagua upande kati ya Lissu au Polepole. SUBIRI UONE
polepole ni scammer hili lipo wazi --- TAL atakuja kuwapa mchakamchaka sana
 
Nakubaliana na wewe kwamba WATANGANYIKA inabidi TUUNGANE.

Kila mtu asimame kutetea nchi katika nafasi yake. Nathamini sana mchango wa Humphrey Polepole, nathamini sana mchango wa Maria Sarungi, nathamini sana mchango wa Mange Kimambi, nathamini sana mchango wa Evarist Chahali na nathamini michango ya watu mbalimbali mitandoani na kwenye vyama vya siasa.

Jambo moja tu ambalo sitalichanganya ni lile la kuamini kwasababu anazungumza kichagga basi ni lazima huyu atakuwa ni Mchagga. Tuna kasumba mbili kubwa kwenye siasa zetu. Mosi, kuamini kwamba kila anayezungumza lugha sawa na sisi au kufanana na sisi basi ni mwezetu. Hili lilimgharimu sana Mzee Nyerere hata kwenye diplomasia ya nchi. Hili limebaki hadi kwetu, WATANGANYIKA tunaamini kwamba kila mtu anawaza mema kama sisi na ana moyo mkunjufu kama sisi.

Huwa yanatukuta tukiwa tumeshachelewa mno, ndiyo tunazinduka usingizini kwamba kumbe huyu hakuwa mwenzetu.

Pili, ni kutopenda kuwajibika kisiasa hata pale ambapo ni dhahiri tumefanya makosa makubwa yanayoonekana. Tunakarisika kabisa tukiambiwa ukweli. Ndiyo maana hadi leo hii Mzee Nyerere alifanya makosa na wengi hatupendi kuyaanisha hayo makosa ili tujifunze, tunaishia kujificha kwenye kivuli cha NIA NJEMA. AU kisipokuwa hicho tutasema ni hujuma za MABEBERU. Nothing is ever our fault. Sasa huu utamaduni wa kutopenda KUWAJIBIKA usipojengwa hapa nchini, tutakuwa na hali mbaya hata kama wapinzani watachukua nchi.

Sasa basi mimi naungana na wote wanaosema ukweli. Lakini sitajiingiza kwenye dhambi ya kuamini kwamba wote wanaipenda TANGANYIKA wala kuiwazia mema. Umri nilio nao unatosha kunifundisha mengi kuhusu siasa za Tanzania.
​
unachokisema ni nje ya solution
Kinachofanyika ni mwanzo wa solution
Kuunga mkono mwanza huo ni Kuruhusu solution itokee
Criminal never die, but current crime need urgent solution.
Hivyo sio lazima kuanzia mwanzo hadi sasa inaweza kuwa vice versa
Remember some are good evils
 
2. UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA USALAMA WA TAIFA ILIVYOANZA
Idara za usalama duniani kote huongozwa na kitu kiitwacho COMPARTMENTALIZATION. Wanausalama wa chumba namba SABA hawatakiwi kufahamu kinachoendelea chumba namba MBILI. Wameenda mbali kabisa kwamba wanausalama wa chumba namba KUMI, hawatakiwi kuwafahamu wanausalama wa chuma namba NANE. Lengo zima ni kulinda usiri na weledi wa taasisi.

Baada ya MTANDAO kujipenyeza ndani ya CHAMA na SERIKALI, walivuruga utendaji kazi mzima wa taasisi za kiusalama hapa nchini. Taasisi kuu za kiusalama hapa nchini ziko tatu (PT, TISS na TPDF-The Cerberus of the State), hazikuwa zinafanya kazi kama inavyotakiwa.

Mwaka 2015, JPM amekuwa Raisi na kukuta wakubwa wengi ndani ya taasisi ni wale wa miaka kuanzia 1992, vijana wengi ni wale wa kuanzia 1996 na wapya wengi ni wale wa Jakaya. SHIDA YA TAASISI ZA KIUSALAMA, ni kwamba huwa mnaapishwa wote siku moja, na mnastaafu wote siku moja au mwaka mmoja, kama mtatofautiana basi ni miaka isiyozidi mitano.

Ndani ya TAASISI, huwa kuna IDARA MBALI-MBALI, kwasababu ni mwiko kuweka mayai yote ndani ya kapu moja(All Eggs in One Basket), maana yakivunjika inakula kwako. Afisa anapoenda kufanya oparesheni kubwa, ni lazima ajaze fomu na afanye utaratibu maalumu kwenda kuomba vifaa vya kufanyia kazi kutoka kwa watu wa IDARA NYINGINE, ambao wanavitunza.

Mfano, unatafuta kuua magaidi. Unafanya utaratibu wa kwenda kwenye IDARA yenye watu wenye mafunzo maalumu ya kijeshi, ambao hao watatakiwa kwenda kuomba silaha maalumu za kufanyia oparesheni kutoka kwenye IDARA nyingine inayotunza silaha. Kuna silaha kama SUMU (Chemical Weapons) huwa zinatunzwa kwenye ghala maalumu chini ya IDARA maalum SURVEILLANCE DEVICES, nazo zinakuwa chini ya watu wa IDARA nyingine.

Sasa operesheni inafanyika kwa kuunganisha idara hata zaidi ya tatu ndani ya TAASISI ya usalama. Mara nyingine tatizo likiwa kubwa sana hata PT, TPDF, MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS na MINISTRY OF FINANCE huhusishwa. Katika hili sasa ndipo MTANDAO walikuwa mbele ya Raisi JPM hatua tano zaidi. Kila akiratibu jambo kwa siri, taarifa zinavuja kutoka IDARA moja kwenda nyingine mwishowe zinafika kwa MTANDAO.

Leo umetuma watu kuchukua SUMU, watu wa ile IDARA kwa akili ya haraka wanajiongeza kwamba, kama SUMU inachukuliwa basi ni lazima kuna POLITICAL ASSASSINATION, hivyo taarifa zinavuja kwamba kuna Dangerous Substance imetoka maabara, na imebebwa na watu wa IDARA fulani hivyo wafuatilieni mwanzo mwisho. AU kuna watu wanafuatiliwa na IDARA ya IT, simu zao zimeingiziwa PERGASUS, taarifa zinatoka tu.

Mzee JPM kazidiwa ujanja, SULUHISHO NI NINI ??? Unda TASKFORCE na fanya En-Masse Recruitment, wape vijana mafunzo (Voda-Fasta) halafu waingizwe mitaani. Anza mdogo-mdogo kuchomoa baadhi ya maofisa ndani ya TAASISI, ambao una uhakika walipenyezwa na watu, lakini zuia Rectruitment nyingine isifanyike bila wewe kujua. Hapa ndipo wakazaliwa WATU WASIOJULIKANA.

Kweli TASK-FORCES, zinasaidia USIRI. Tatizo ni kwamba hazifanyi kazi kwa kufuata sheria. Maana ndani ya TAASISI, kila oparesheni inayofanyika ni lazima itakuwa AUDITED tu. Operesheni nyingi na fedha zake ni lazima zipitishwe na utawala wa kiraia (Civilian Administration) ili kuhakikisha TAASISI hazifanyi mambo ya ajabu kama kutaka kupindua nchi, au kutumika na watu binafsi kufanya hujuma.

Hata kipindi cha JK, taarifa zilikuwa zinavuja kwasababu ya huu mlolongo nwa KIIDARA ambao uko kisheria. Mambo mengi yalikuwa yanamulikwa, ndiyo maana kuna mipaka hata yeye na UFISADI wake alikuwa anaogopa kuivuka. Mzee JPM, kaanzisha TASK-FORCE, zina watu lakini wengi siyo PROFESSIONAL and SEASONED-VETERANS. Tatizo ni kwamba ukiwataka PROFESSIONALS unakuja kuambiwa wengi wanafahamiana, au wengi walienda mafunzo kambi moja, au wengi walifanyiwa mafunzo na kuingizwa kwenye taasisi na WANAMTANDAO waliowahi kuwepo ndani TAASISI.

MATOKEO ni NINI ??? Oparesheni nyingi zinaanza kufanywa kiholela kwasababu kwanza kabisa hazina wataalamu ambao wengi wangeweza kuuliza maswali, kutoa ushauri wa kitaalamu, au hata kukataa kufanya mambo ya ajabu. Lakini pili, kwasababu hakuna sheria inayounda TASK-FORCE wala kuzisimamia kila kitu kinakuwa ni halali. Wengi wataua watu, watateka na kutesa watu bila hata sababu zisizo za msingi.

Chanzo chote cha haya ni MTANDAO ambao umevuruga nchi na kujipenyeza kila sehemu na kumsababishia Mzee JPM awe na hofu muda wote (Paranoia). JPM alikosea na kiukweli mbali na kufanyiwa hujuma, huyu Mzee wetu alikuwa ni mtu mwenye tabia ngumu tangu uwaziri. Tunaweza kusema kuna baadhi ya maadui aliwatengeneza bila ulazima wowote ule. Angekua ni mtu mwenye kutuliza kichwa, sidhani kama MTANDAO wangemshinda.

Kiufupi, alichokifanya Mzee JPM na TASK-FORCE zake, hakina utofauti sana na kile ambacho Marehemu Mzee Jiang Zemin wa Uchina alikifanya mwaka 1999 kwa kuanzisha OFFICE 610, ambapo alishawishi CHAMA CHA KIKOMUNISTI kwamba waruhusu ianzishwe ili kupambana na makundi hatari kama The Falun Gong, nje kabisa ya mfumo wa Guaonbu (THE MINISTY OF STATE SECURITY).

Katika hili alifanikiwa mno, sema tatizo ni kwamba OFFICE 610, ilianza kutumika vibaya na MTANDAO wa Jiang Zemin a.k.a The Shanghai Clique ambao ulikuwa umejaa watoto wa vigogo (Princelings) kama Bo Xilai ambao walitumia OFFICE 610 kupata Uraisi, hadi mwaka 2012 kudiriki kutaka kumzuia Raisi Xi Jinping asiapishwe kwa kusambaza vikosi vya majasusi zaidi ya 15000 na askari zaidi ya 80,000 waliopo Tibet na Xi Njian wakisingizia kufanya mazoezi.

Hivyo TASK-FORCE zinasaidia, lakini bila usimamizi mzuri chini ya watu aina ya Bashite na Mafwele zinaweza kuvuruga kabisa mchakata wa kiutawala ndani ya nchi hasahasa pale zinapokuwa tayari kubwa na zenye askari wengi na rasilimali nyingi. Tulipofika, haitakiwi TAASISI yoyote ya kiusalama kufanya jambo kubwa bila usimamizi wa kisiasa (Civilian Oversight).

Bahati mbaya sana sasa, Raisi Samia kaingia Ikulu na amegundua kwamba kuanzisha FORCE-WITHIN A FORCE a.k.a TASK FORCE zina manufaa mengi kisiasa hasahasa pale unapotaka mambo yake yaende haraka, bila usimamizi wowote ule wa kisheria (Legal Scrutiny) na ushahidi (Incriminating Evidence). Mbali na NIDA+CCM+NEC kuwa na hatihati ya kumnufaisha Raisi Samia, hiyo mifumo ya FORCE-WITHIN A FORCE a.k.a TASK FORCE ambao ulianzishwa na Mzee JPM kupambana na MTANDAO, leo hii unatumiwa na MTANDAO kupambana na WATANGANYIKA.

RAI YANGU: Watanzania tusikubali TAASISI za kiusalama zitumike kisiasa bila kuwawajibisha viongozi wanaofanya hivyo. Lazima tufuate KANUNI, ili kuzuia madhira kama haya yanayolikumba hili taifa letu. Leo hii kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaweza wakakuchukia tu, na wakaamua kupiga simu moja tu kwa hawa watu wa TASK-FORCE na tusikuone tena mtaani.

Pia mara nyingine unaweza ukalaumu Polisi, Maafisi na Wanajeshi kwamba kwanini mnafanya mambo kinyemelea na kihuni bila weledi wowote ule, bila kufahamu ukweli ni kwamba ndani ya taasisi zao kuna vikosi maalumu (TASK-FORCES) zinazofanya kazi za wanasiasa bila kuwa CIVILIAN AUDITED, tena vimejaa maofisa ambao hawana ujuzi wala uzoefu mkubwa.
​
HILI NDILO ANDIKO BORA LA MWAKA HUMU JF
NARUDIA TENA KUSEMA

HILI NDILO ANDIKO BORA LA MWAKA HUMU JF
 
Mwaka 1975, baada ya IDARA kufanya mauaji makubwa na kuonea raia wake kule kanda ya ziwa, Mzee Nyerere alichukua maamuzi magumu mno. Alifukuza kazi MAAFISA USALAMA kuanzia wakurugenzi waandamizi, WAZIRI OFISI YA RAISI na WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, hadi POLISI.

Mzee Nyerere kurudisha heshima alivunja kabisa IDARA, na kuteua MKURUGENZI msomi DR. Laurent GAMA aiongoze. Tofauti na ule utaratibu wa zamani wa kujaza TANU YOUTH LEAGUE ambao wengi walionekana kuwa THUGGISH and SADDISTIC, kina Dr. Gama waliaenda kufanya En Masse Recruitment mashuleni na vyuo vikuu.

Rucruitment ya 1975, ndiyo ilileta watu kama Membe, Mizengo na wengine ambao binafsi nawafahamu walioenda kupata mafunzo ya kinidhamu nje ya nchi. Walau IDARA iliendeshwa kiheshima, hasahasa baada ya kuona Mzee Emilio Mzena na Mzee Peter Siyovelwa ambao waligeuza IDARA kama mali yao binafsi wametimuliwa. Huyu Siyovelwa siku maafisa wameitwa Ikulu kwenye kikao aliinuka na kuanza kumtolea Mzee Nyerere maneno ya kashfa akimnyooshea kidole na kumwambia "Wewe Julius unahisi hii nchi ni yako peke yako"

Huyu Peter Siyovelwa alikuwa kama mungu-mtu. Ukimuona kwa nje-nje hivi unaweza ukasema ni mtu mwenye bashasha lakini ni moja kati ya watu waliochochea ugomvi baina ya Mzee Nyerere na Mzee Kambona. Ilifika hadi kipindui pale Iringa wakiteua WAKUU WA MIKOA wanawake alikuwa anapiga simu kwa Raisi au Waziri Mkuu, akisema hataki. A Megalomaniac Per Excellance.

SASA WATU AINA HII, ambao wanadhani wanaweza kutoa uhai wa binadamu mwenzao bila kuwajibika ndiyo wamejazana CCM, TISS, TPDF na PT. Wengine hujiita ni WAZALENDO. Ila ukweli ni kwamba MWANADAMU asipowekewa mipaka ndiyo kinatokea kile kilichotokea mwaka 2017 kwa Tundu Lissu.

BOOKMARK THIS: Siku Tundu Lissu anatolewa nje, Amin Amin nawaambia, tutafahamu madhambi mengi ya Ndugu Humphrey Polepole ambayo aliwahi kuyafanya. Pia sidhani kama atakuwa na uwezo wa kujibu hoja za Lissu. Wakati hili linatokea, WATANGANYIKA wengi watakuwa washachagua upande kati ya Lissu au Polepole. SUBIRI UONE
​
Kwamba Polepole atagombea dhidi ya Tundu Lissu.

Hili sipingi.
 
Back
Top Bottom