UTANGULIZI:
Habari ndugu MTANGANYIKA, leo ni mambo mengi kweli ya kusema ambayo yanatatiza sana moyo wangu. Nimejaribu kuandika wiki kadhaa lakini naishia kufuta kila nikimaliza kuyaaandika. Mengine nikiyasema hadharani yanaweza kuwaumiza sana moyo na mkaishia kukata tu, tamaa. Ila itoshe kusema kwamba TANGANYIKA ISHAUZWA.
1.TANGANYIKA KUTETEWA NA WANAHARAKATI WALIOWAHI KUTUHUJUMU:
Ndugu Humphrey Polepole na pamoja na wanaharakati wengine wa mtandaoni kama Mange Kimambi na Maria Sarungi, watu ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kuwa wanufaika wa mfumo na hata kutumika kuhujumu wananchi. Mtu pekee ambaye amekuwa akisema ukweli siku zote ni kaka yangu Evarist Chahali (He has been very Consistent and Objective).
Miundombinu mingi ambayo Samia anaitumia kututesa WATANGANYIKA, ilitengenezwa na Raisi John Pombe Magufuli. Humphrey Polepole na Dr.Bashiru Ali Kakurwa walikuwa ni wahandisi wakuu wa kisera. Ilifika kipindi hadi Dr. Bashiru alitamka wazi kwamba CCM inaweza kuvunja katiba ili kubaki madarakani kwasababu ndiyo imeshika dola.
Hawa wengine kama Maria Sarungi, na Mange Kimambi tunafahamu kwamba madai mengi yalianza kama maslahi binafsi. Hasahasa Binti Sarungi ugomvi wake mkubwa na JPM chanzo ni mambo ya kifamilia ambapo yeye kama munfaika wa mfumo alikutwa na SHOCK-THERAPY ya JPM. Alikuwa na mwenzake Fatma Binti Karume, ambaye mlimbatiza jina na kumwita Shangazi, lakini awamu hii rangi zake naye mshaziona.
Mange Kimambi, ni mamluki. Alishawahi kuwa upande wa CCM, baadaye dhidi ya Lowassa, baadaye upande wa Lowassa dhidi ya Magufuli. Baadaye kushangilia msimba wa Magufuli na kumnadi Samia, na saa hizi yuko dhidi ya Samia. WATANGANYIKA hatufahamu kesho atakuwa dhidi ya nani.
Hii dhambi naona inatafuna wengi mno hadi maafisa usalama ambao binafsi nawafahamu waliwahi kuwa mstari wa mbele kutetea kila ujinga unaofanywa na dola, ambapo mamia ya WATANGANYIKA walipoteza uhai, kuumizwa, kufungwa au kufilisiwa. Hata humu JF wengi nawafahamu, naona kabisa mwelekeo wao ni watu aliyepagawa na pepo au kapata wazimu.
WATANGANYIKA, ili kuepukana na kadhia hii ya kubebwa na kila aina ya upepo wa kimaslahi wa watu ni lazima WASOMI wajifunze kusimamia kitu kinachoitwa KANUNI (Principles). Hata pale ambapo mwanasiasa unayempenda anakosea, wewe inabidi uufunde moyo wako kusimamia KANUNI.
RAI YANGU KWA WATANGANYIKA, hasa WANAUSALAMA: Kwenye BIBLIA, Daudi alikuwa ni mtenda dhambi mkubwa kama sisi tu, lakini tunaambiwa ni moja kati ya watu walipata kibali kikubwa sana kwa MUNGU. MUNGU alisema wazi kabisa kwamba anampenda Daudi kwasababu MOYO WAKE HAUNA HILA. Daudi alikuwa ni mtu mwenye kusimamia KANUNI.
Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda amuue Daudi. Mara mbili Daudi alipata nafasi ya kumuua kabisa Sauli, kwa mambo aliyomtendea lakini Daudi alisimamia KANUNI. Alikataa kumuua na kusema HUYU NI MPAKWA MAFUTA WA MUNGU, atamalizana na MUNGU wake.
Daudi alikuwa ni KIONGOZI MKARIMU (Equittable). Kuna sehemu kwenye BIBLIA ilitokea vita, na baadhi ya askari wake walichoka wakashindwa kwenda vitani. Waliporudi na kupata ushindi mkubwa na mali nyingi, kuna baadhi ya askari wakasema hawa ambao hawakwenda na sisi vitani wasipewe chochote kile. Daudi aliwakemea na kusema aliyekwenda vitani, na aliyebaki kulinda mji wote watapata mali sawa. Akimaanisha kwamba kila mtu ana umuhimu ndani ya jamii.
Daudi alikuwa ni KIONGOZI MUUNGWA. Alikosea mno kwa kuiba mke wa mtu na kumpa mimba, huku akimuua mume wake. Baadaye alipofutwa na nabii Nathani kuambiwa ukweli, wala hakutafuta vijisababu, bali alikuwa mpole na kwenda kuomba msamaha mbele ya taifa zima. Hakusema kwamba yeye alikuwa na nia njema, ila alisema wazi kwamba amekosea.
SASA BASI: wale ambao mliwahi kuwakosea WATANGANYIKA, na kusababisha vifo, misiba, umasikinui na majeraha ombeni TOBA KWA MUNGU, OMBENI TOBA KWA WATANGANYIKA, lakini kubwa zaidi TOBA YA KWELI huambatana na mabadiliko ya moyo. Jaribuni kukaa kwenye viatu vya watu kama Wazazi wa Ben Saanane, Familia ya Gwanda, Familia ya Soka, Familia ya Akwilina na wengine kisha mtafahamu kwamba WENGI HAMKUISHI VIAPO VYENU.