MALCOM LUMUMBA Lord Denning ahsante kwa mjadala mzuri. Baada ya muda nimeingia na kusoma kitu.
Hata kama sikubaliani na baadhi ya hoja zenu, nakubaliana na ujenzi wenu wa hoja na kina cha mjadala
Nimefurahi , nililolieleza takribani miaka 10 hapa JF linaongelewa kwa ukubwa, yaani tatizo la Taasisi na mifumo yake.
Katika hili namlaumu Mwl. Nyerere kwa kuamini kwamba uzalendo na maadili waliokuwa nayo yangeheshimiwa na kuwa utamaduni. Mwalimu akatujengea mifumo na Taasisi zinazotegemea uadilifu badala ya kanuni, taratibu na sheria. Mwl alidhani Vijana wake na Wajukuu watakuwa kama yeye na wenzake. Mwl akatuachia;
1. Katiba ya Nchi isiyoweza kujitetea kwasababu haina mifumo inayoitetea kama Mahakama
2. Taasisi zinazotegemea Mtu au Watu badala ya Taasisi zinazojiendesha kwa sheria , kanuni na taratibu zake.
Niliwahi kutoa mfano wa Nchi ya India iliyokaa miezi 3 bila Waziri Mkuu kwasababu hakuna aliekuwa na majority.
UK (Uingereza) ilikaa wiki 3 bila Waziri Mkuu, hakuna aliyeweza kuunda serikali.
India na UK hazikutetereka mifumo ya Ulinzi, Usalama, Uchumi na siasa ilikuwa chini ya Taasisi, nchi haitegemei mtu.
Magufuli altusaidia kujua panapovuja. JK alianza kuvuruga Taasisi kimya kimya, pigo la mwisho lilikuwa la Magufuli.
Hizo Task force , kudhalilisha Mahakama,kuingiza vyombo vya ulinzi na usalama katika siasa, kuzifanya Taasisi ni mali ilianzia kwa JK kisha Magufuli. Tangu hapo Taasisi hazijasimama tena.
Hata Taasisi kama Jeshi hazijachwa salama , Mzee Warioba alithibitisha.
Tatizo letu si Taasisi moja moja ni jumla ya Taasisi zetu. Tunapaswa kuwa na mfumo unatengeneza Taasisi (Institutions) zinazojitegemea na zinazosimama kwa masilahi ya Nchi na si mtu wala Watu.
Taasisi haziwezi kufanikiwa isipokuwa kwa kufanya mageuzi yafuatayo
1. Kutengeneza sheria zinazolinda Taasisi- KATIBA
2. Kuwapa Wananchi nguvu ya kumiliki Taasisi (BUNGE)
3. Kulinda Wananchi na sheria za Nchi- MAHAKAMA
Haya yakifanikiwa mengine yatafuata mtawalia
JokaKuu