comrade_kipepe
JF-Expert Member
- Jun 25, 2019
- 8,748
- 18,096
Jamiiforums ianze kutulipa sasa maana umeacha kazi zako umetumia week nzima kuandika uzi
Walichokifanya kina
Yes hilii.
Umkubali au umchukie, the guy is charismatic.
Press zake hata afanye nane Usiku, maelfu kama sio malaki ya Watanzania watamsikiliza.
Na yeye anasema vitu ambavyo vimekuwa vikiongelewa siko zote, anapigia tu mstari.
Na kama ukimfuatilia vizuri ni kuwa kuna pahala anataka tufike, na naamini tutafika.
Juzi nimekutana na binti mmoja ananiambia habari za Mtandao na upigaji unaoendelea. Jambo ambalo sikutegemea kuliskia kutoka kwake, kwa namna alivyo na maisha anayoishi.
So, Pole pole ana impact tena positive kabisa kwenye Ukombozi ( ambao naona hauko mbali)
Kazi nzuri sana. Bandiko zuri. Tunashkuru mno.Haya WAKUU, mimi NIWATAKIENI KILA LA KHERI
==================================================
Hatuna la zaidi ya kusema :Haya WAKUU, mimi NIWATAKIENI KILA LA KHERI
===================================================
Kwa maneno mengine Gwajima yuko sahihi lakini kwa kusema hivyo kanisa lake limefungwaMALCOM LUMUMBA Lord Denning ahsante kwa mjadala mzuri. Baada ya muda nimeingia na kusoma kitu.
Hata kama sikubaliani na baadhi ya hoja zenu, nakubaliana na ujenzi wenu wa hoja na kina cha mjadala
Nimefurahi , nililolieleza takribani miaka 10 hapa JF linaongelewa kwa ukubwa, yaani tatizo la Taasisi na mifumo yake.
Katika hili namlaumu Mwl. Nyerere kwa kuamini kwamba uzalendo na maadili waliokuwa nayo yangeheshimiwa na kuwa utamaduni. Mwalimu akatujengea mifumo na Taasisi zinazotegemea uadilifu badala ya kanuni, taratibu na sheria. Mwl alidhani Vijana wake na Wajukuu watakuwa kama yeye na wenzake. Mwl akatuachia;
1. Katiba ya Nchi isiyoweza kujitetea kwasababu haina mifumo inayoitetea kama Mahakama
2. Taasisi zinazotegemea Mtu au Watu badala ya Taasisi zinazojiendesha kwa sheria , kanuni na taratibu zake.
Niliwahi kutoa mfano wa Nchi ya India iliyokaa miezi 3 bila Waziri Mkuu kwasababu hakuna aliekuwa na majority.
UK (Uingereza) ilikaa wiki 3 bila Waziri Mkuu, hakuna aliyeweza kuunda serikali.
India na UK hazikutetereka mifumo ya Ulinzi, Usalama, Uchumi na siasa ilikuwa chini ya Taasisi, nchi haitegemei mtu.
Magufuli altusaidia kujua panapovuja. JK alianza kuvuruga Taasisi kimya kimya, pigo la mwisho lilikuwa la Magufuli.
Hizo Task force , kudhalilisha Mahakama,kuingiza vyombo vya ulinzi na usalama katika siasa, kuzifanya Taasisi ni mali ilianzia kwa JK kisha Magufuli. Tangu hapo Taasisi hazijasimama tena.
Hata Taasisi kama Jeshi hazijachwa salama , Mzee Warioba alithibitisha.
Tatizo letu si Taasisi moja moja ni jumla ya Taasisi zetu. Tunapaswa kuwa na mfumo unatengeneza Taasisi (Institutions) zinazojitegemea na zinazosimama kwa masilahi ya Nchi na si mtu wala Watu.
Taasisi haziwezi kufanikiwa isipokuwa kwa kufanya mageuzi yafuatayo
1. Kutengeneza sheria zinazolinda Taasisi- KATIBA
2. Kuwapa Wananchi nguvu ya kumiliki Taasisi (BUNGE)
3. Kulinda Wananchi na sheria za Nchi- MAHAKAMA
Haya yakifanikiwa mengine yatafuata mtawalia
JokaKuu
Huyu 48...KJ kiburi sana mkuu🤣🤣🤣So tunapaswa kuwa tumetumikia jeshi kama commissioned officers Ili tuelewe uzi wako?..
Basi Polepole yuko mbele ya wakati mkuu.What is Law ???
Professor John Austin defines law as "Commands of the sovereign backed by sanctions". Akimaanisha sheria ni amri zinazotolewa na mamlaka ya juu kwenda kwa watu wa chini ili kutekeleza jambo fulani zikisindikizwa na adhabu.
Professor John Austin anasema hata mtunge sheria, zisipokuwa na kitisho cha adhabu aidha kufungwa, kunyongwa au faini fahamu fika kwamba hizo siyo sheria bali maneno matupu. Hivyo ili sheria iwe sheria, ni lazima watu wafahamu fika kwamba endapo tutavunja kuna madhara huko mbele.
Watanganyika wanafanya ujinga kwasababu vikwazo vya uvunjwaji havijawahi kutekelezwa dhidi ya watawala wanaovunja sheria. Siku vikitekelezwa basi sheria itakuwa sheria haswa na hutaona hata katabia ka mazoe kakiendelea. Kule Ufaransa mwaka 1789 walinyonga Mfalme wao, na kuua watawala zaidi ya 30,000 kwa siku moja kisa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Baada ya pale viongozi waliofuata walikuwa na adabu sana.
Asante sana, Mkuu, kwa kunielewa na kutoa mapendekezo muhimu ya kutafuta muafaka. Hoja zako hapa ni za msingi sana. Hii model uliyopendekeza Ina mashiko kama local government za Sasa haziwajibiki ipasavyo kwa wananchi.Tatizo lenu kubwa ni hili, kutafuta suluhu rahisi kwenye majawabu magumu.
Mzee Nyerere aliposema Tanganyika itaimeza Zanzibar, hakuwa mkweli kwa asilimia 100%. Aidha alikuwa ni mwoga, alifikia ukomo wa kufikiri au alikuwa na ajenda yake ya siri. Jambo ambalo hatupendi kulisema ni kwamba kisheria neno SERIKALI lina maana kubwa sana. Tunaposema serikali ya Tanganyika hatumaanishi chombo kingine (A New Entity) ila kufahamika kwa Tanganyika pamoja na uwezo watu wake kusimamia mambo yao (Historical Identity and Ability to decide our affairs).
Serikali ya Tanganyika ikiwepo siyo lazima tuunde SHIRIKISHO (A Federation). Duniani kote neno serikali humaanisha vitu vikuu viwili: Serikali Kuu (The Central Government) ambayo huwa inatambulika kimataifa kama msimamizi mkuu na mdhibiti wa dola, na Serikali Ndogo (Local Government), ambazo huongoza jamii husika kuanzia ngazi ya kijiji, kitongoji, tarafa, wilaya hadi mkoa.
KAMA MNAOGOPA SERIKALI TATU BASI FANYENI HAYA YAFUATAYO:
Federate at Local Levels.
Tengenezeni majimbo maalumu ndani ya Tanganyika ambayo yatakuwa yanajisimamia yenyewe chini ya WIZARA MAALUMU YA TAMISEMI. Tanganyika haitakuwa na Raisi au Waziri Mkuu, bali itakuwa ina chombo maalumu chini ya TAMISEMI ambacho kitasaidia kuratibu sera mbalimbali chini ya Uangalizi wa WAZIRI MWENYE DHAMANA.
Haya majimbo yatakuwa na wawakilishi wake kwenye BUNGE LA JMT, huku yakiweza kuchagua na viongozi wao wa maeneo husika ambao watasimamia maslahi ya wananchi wao. Hili la kulazimisha kwamba kila kitu kifanywe na Serikali na Bunge halina afya na litaendelea kuleta maneno.
Waruhusuni Watanganyika wapewe serikali zao (Semi-Autonomous) walau kwenye ngazi za majimbo, ambazo watazichagua wao, na zitasimamiwa na chombo maalumu chini ya TAMISEMI.TAMISEMI siyo suala la MUUNGANO hivyo tuanzie hapa. Mambo ya msingi ya Tanganyika hayatakiwi hata yaamuliwe hata na serikali ya Tanganyika bali watu wenyewe kwenye serikali zao (Local Governments), huku wakishirikiana na serikali ya JMT.
===============================================================
Mkiamua mnaweza kuigeuza TAMISEMI leo kuiita THE TANGANYIKA OFFICE, ambayo itasajili serikali za majimbo ambazo ni (Semi-Autonomous) kupitia, A Special Charter/ Act of Parliament. Hili likifanyika kutakuwa na ufanisi mkubwa mno kwenye utendaji. Kwanza kabisa hata makelele ya CHADEMA hayatakuwepo maana watakuwa wametingwa huku na kuwaachia CCM Serikali Kuu.
Lakini, pia ufisadi mwingi unasababishwa na kukosa udhibiti imara wa serikali ndogo (Local Government). Hizi serikali zikisajiliwa na kuanza kujitegemea kuna mambo mengi mno kama rushwa na uzembe vitapungua kwa kasi, na watu hawatadirikia kufanya ujinga. Mtapata wasomi hadi kwenye ngazi za vijiji wakifanya kazi kwasababu serikali za majimbo zitakuwa zinaweza kusimamia mapato yake.
Hebu tujaribu hili, nimelifuatilia sana na kutafiti na kuona kwamba linaweza kuzaa matunda makubwa. Tunaweza kuendelea kulifanyia tafiti.
Huyu malcom anajifanya jasusi uchwara mwenye nia njema ya "kuikomboa" Tanganyika lakini nimegundua ana malengo fiche ambayo yako mbali sana na kuikomboa Tanganyika.Umefafanua vizuri sana...
Kila mtu amejua tatizo ni wanamtandao...
Lakini mwisho unamlalamikia mtu anayepambana na wana mtandao...
Badae unajaribu kuwagombanisha polepole na lissu, ambao wanaweza wasiwe chama kimoja ila wote ni maadui wa samia na mtandao...
Na badae tena unajaribu kufanya ramli, kwamba mmoja akitoka jela hawatoelewana...
Kipi ni kipi brother...
Kitu unachokosea, kuna namna humfahamu Lissu...
Lissu ni mweupe wa roho na yuko tayari kushirikiana na yeyote kupambana na adui...
Lissu sio mbowe, mbowe anatabia za chuki...
Lissu anaweza kufanya kazi na yeyote ili mradi ameonesha nia njema...
Humfahamu polepole...
Polepole amenyooka sana na ni rahisi kufanya kazi na watu walionyooka kama lissu...
Ndio maana alipewa ugali na kikwete ila hakuendana nae, amekuja kuendana na magufuli...
NB: nyinyi ndio mlimtengeneza shetani ndani ya magufuli...
kipindi magufuli anaanza kazi alikua na nia njema ya kushirikiana na kila mtu...
baadae mkaanza kutumika na mtandao, pamoja na usomi wenu...
kipindi cha magufuli ndio tuliona wasomi wa jf wakipinga miradi ya bwawa la mwalimu na sgr kwa kutumia sababu za watu wa ulaya na marekani...
eti pollution...
miradi ya daraja la busisi ikapingwa na wasomi wetu kwasababu za kikabila...
wengine tukajiuliza mwanza sio tanzania? mbona miradi mingi inaenda dar, arusha, pwani na dom watu hawalalamiki?
kwa jinsi watu wa mwanza walivyokua wanahangaika kuvuka pale ferry halafu msomi mmoja anakuja kukwambia daraja limejengwa kikabila, unashangaa!
kumbe ndugu zetu mnatumika mda huo, akili mmeweka kwenye mfuko...
yaani anaibuka msomi mmoja anakwambia mradi wa bwawa la mwalimu ndani ya mbuga utasababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira na dunia haitakua mahali salama...
unajiuliza huyu ni msomi kweli? kumbe mwenzako ameweka akili mfukoni, anatumika...
baada ya magufuli kuwagundua...
akaanza kutocheka na mtu...
mkajikuta mmemgeuza magufuli, na ikabaki historia...
Pointi kubwa kwa sasa ni namba 2 hapo juu.MALCOM LUMUMBA Lord Denning ahsante kwa mjadala mzuri. Baada ya muda nimeingia na kusoma kitu.
Hata kama sikubaliani na baadhi ya hoja zenu, nakubaliana na ujenzi wenu wa hoja na kina cha mjadala
Nimefurahi , nililolieleza takribani miaka 10 hapa JF linaongelewa kwa ukubwa, yaani tatizo la Taasisi na mifumo yake.
Katika hili namlaumu Mwl. Nyerere kwa kuamini kwamba uzalendo na maadili waliokuwa nayo yangeheshimiwa na kuwa utamaduni. Mwalimu akatujengea mifumo na Taasisi zinazotegemea uadilifu badala ya kanuni, taratibu na sheria. Mwl alidhani Vijana wake na Wajukuu watakuwa kama yeye na wenzake. Mwl akatuachia;
1. Katiba ya Nchi isiyoweza kujitetea kwasababu haina mifumo inayoitetea kama Mahakama
2. Taasisi zinazotegemea Mtu au Watu badala ya Taasisi zinazojiendesha kwa sheria , kanuni na taratibu zake.
Niliwahi kutoa mfano wa Nchi ya India iliyokaa miezi 3 bila Waziri Mkuu kwasababu hakuna aliekuwa na majority.
UK (Uingereza) ilikaa wiki 3 bila Waziri Mkuu, hakuna aliyeweza kuunda serikali.
India na UK hazikutetereka mifumo ya Ulinzi, Usalama, Uchumi na siasa ilikuwa chini ya Taasisi, nchi haitegemei mtu.
Magufuli altusaidia kujua panapovuja. JK alianza kuvuruga Taasisi kimya kimya, pigo la mwisho lilikuwa la Magufuli.
Hizo Task force , kudhalilisha Mahakama,kuingiza vyombo vya ulinzi na usalama katika siasa, kuzifanya Taasisi ni mali ilianzia kwa JK kisha Magufuli. Tangu hapo Taasisi hazijasimama tena.
Hata Taasisi kama Jeshi hazijachwa salama , Mzee Warioba alithibitisha.
Tatizo letu si Taasisi moja moja ni jumla ya Taasisi zetu. Tunapaswa kuwa na mfumo unatengeneza Taasisi (Institutions) zinazojitegemea na zinazosimama kwa masilahi ya Nchi na si mtu wala Watu.
Taasisi haziwezi kufanikiwa isipokuwa kwa kufanya mageuzi yafuatayo
1. Kutengeneza sheria zinazolinda Taasisi- KATIBA
2. Kuwapa Wananchi nguvu ya kumiliki Taasisi (BUNGE)
3. Kulinda Wananchi na sheria za Nchi- MAHAKAMA
Haya yakifanikiwa mengine yatafuata mtawalia
JokaKuu
Umeona vizuri mkuu.Huyu malcom anajifanya jasusi uchwara mwenye nia njema ya "kuikomboa" Tanganyika lakini nimegundua ana malengo fiche ambayo yako mbali sana na kuikomboa Tanganyika.
Hili ni boksi. Garasa.
Sana. Analeta mastori yake ya kijinga ya kutulaghai kumbe ana malengo tofauti kabisa.Malcom wewe ni msomi mzuri ila una matatizo mawili...
Unafiki...
Kutumika...
Huyo ni close minded , amefungwa na uchawa hivyo ni ngumu kuelewana yeye anachojua ni kupiga mapambio ya SAMIA na CCM , hana kingine anachokifahamu utqjichosha bure hata kumjibuUmewahi kutumikia jeshi kama Commissioned Officer ???
Bila kuwa Commissioned Officer hata nikikupa mifano lukuki huwezi kuelewa.
Saa tatu asubuhi mkuu.Unasema sheria mpya ya Usalama ya 2023 ilipitishwa sasa kumi na moja jioni. Ilitakiwa ipitishwe saa ngapi ?
Hapo wote wako sahihi kabisa mkuu.Lissu sioni akiungana na Polepole kwa sababu wanaamini katika vitu tofauti. CCM imara = Nchi imara Vs Bila CCM = nchi imara.