Tusipojua tunataka nini kwenye elimu yetu, tutakuja kupangiwa na watu wa nje

Tusipojua tunataka nini kwenye elimu yetu, tutakuja kupangiwa na watu wa nje

Mimi ukiniuliza mabadiliko kwenye elimu yetu, basi nitapendekeza Lugha ya Kiingereza itumike kufundishia elimu ya msingi hadi chuo kikuu.

Nakuunga mkono mkuu,sisi sio taifa kubwa na linalojitegemea kama China, Urusi sijui wapi.....tunahitaji Kingereza zaidi ya kiswahili..
 
Naona kama kwenye education system bado tumelala sana. Hivi huwa najiuliza. Wananchi wa tanzania wanataka watoto wao waelimishwe kuhusu nn. Elimu bora imefafanuliwa vipi kwa wazazi.

Tuna mpango endelevu kweli wa kujua watoto wetu wanahitaji kujua nn mashuleni utakao husisha kubadilishwa kwa syllubus.

Je, wanahitaji kujua kingereza kizuri?
Je, wanahitaji kujifunza juu ya uzalendo wa afrika?
Je, wanahitaji kujifunza discipline?
Je, wanahitaji kujifunza technology?
Je, wanataka ipad na sio chaki?

Lakini swali linabaki palepale, watoto wetu wanataka nini?

Naongea hivi kwa sababu tukishindwa kujua watoto wetu wanataka nn. Kuna mtu atatokea sehemu, inaweza kua ulaya au sehemu yoyote na kutuletea chochote kwa watoto wetu na atadai kuwa hicho alichokileta ndo kinafaa kwa watoto wetu.

Watu wataniuliza, kwanini watu watoke nje watuletee sisi elimu ya watoto wetu na kutuelekeza jinsi ya kuwalea. Je, kuna kitu wanafaidika?

Of course yes, kwenye kila move inayofanywa na mtu ambae ni tofauti na jamii yetu lazima kuwe na ufaidikaji. Inaweza kua ni long term plan ya ku miseducate watoto.s

Ndo maana nauliza tena, wana community wa Tanzania. Je, tunataka watoto wetu wapate nn mashuleni? Tuna sababu zozote za kubadili syllubus. Na kama zipo, tunampango gani za ku-implement. Maana zao la watanzania tulionao na matatizo yaliyopo limechangia sana na impact ya elimu yenye makosa mengi.

Tunahitaji elimu ambayo ni environment-specific...tuangalie mazingira yetu yana nini/resources ndipo tutunge syllabus!...namaanisha tufundishe watoto fursa zilizopo kwenye mazingira yetu na jinsi ya kuzi exploit, wakimaliza wana confidence ya kuexplore opportunities(employment/self -employment), kwenye mazingira yaliyopo Tanzania...

Tunahitaji change kwenye syllabus ndio ila sio ku copy everything from the west, wao wana challenges zao kutokana na mazingira yao wanazojaribu kutafuta solutions., Tunachoweza kujifunza kwao ni jinsi wanavyotumia Education to solve challenges ndani ya jamii yao...

I believe Technology, English,ni masomo ambayo kila mtoto wa Tanzania afundishwe nayo tangia mdogo, sisi sio kisiwa every other country wanainvest in these two subjects, Technology inarahisisha mambo saves times and English ina facilitate communication between borders....Plus somo ambalo naona liongezwe ni Kilimo, we have large arable land as an asset...
 
Back
Top Bottom