Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
TUSIPOTOSHE UMMA RAIS MAGUFULI YUPO TAYARI KWA MDAHALO, SI VINGINEVYO.
Wasalaam wana JF.
Natumia fursa hii kutoa ufafanuzi na maelezo yanayojitosheleza dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mgombea wa kiti cha urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa haogopi mdahalo wa aina yoyote na kwa namna yoyote ile, wanaojenga hoja hii ni wapotoshaji na wapuuzwe kabisa, najenga hoja hii kumtetea Rais kutokana na utendaji wake kuwa wazi na usio na shaka kwa Watanzania wote.
Dkt. Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa chama dola na amiri jeshi mkuu wa nchi, Chini ya Rais Magufuli serikali ya awamu ya tano imefanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo na kitekinolojia kwa Watanzania wanyonge ambao kwa muda mrefu ombi lao lilikuwa kumpata kiongozi mwenye maono mithili ya Magufuli, Sasa amepatikana kiongozi mwenye “Tumaini la Kweli” nongwa ya nini?
Aidha nimesikia ombi la Ndugu Tundu Lissu la kuomba uwepo wa mdahalo kati yake na Dkt. Magufuli, ni Jambo jema katika ustawi wa nchi na wala Lissu hajakosea, lakini kinachonipa shida ni dhana inayojengwa kwa sasa na “mtandao wa upinzani”, na wapambe wao kuwa mgombea wa CCM anaogopa mdahalo ni uongo na fitina za wapinzani wa Magufuli, Dkt. Magufuli anao uwezo wa kujibu hoja kwa hoja, kujenga hoja na kupangua kila hoja inayoweza kujitokeza mbele yake, ni kiongozi anayejiamini tofauti na Bwana Lissu anavyofikri.
Kifikra, Upeo, Medani za Ungozi kifalsafa uwezi kuwa linganisha Magufuli na Lissu, Lissu uongozwa na hoja za mihemko na vitisho, wakati Magufuli ujenga hoja zenye utamaduni wa kutatua matatizo ya watu, kwa ufupi Magufuli ana maono ya utatuzi wa matatizo ya watu na si mihemko ya kisiasa, Je kwa dhana hizi nani mwenye kuogopa mdahalo? Bila shaka jibu lipo wazi.
Uwezi kuwa na kiongozi mwenye serikali iliyofikia malengo kwa asilimia kubwa katika uwajibikaji kwa watu alafu ukasema anaogopa mdahalo, mdahalo kuna wadudu gani huko mpaka Magufuli aogope kujitokeza, ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa hofu ya Rais kuogopa mdahalo iondoke vichwani mwa wapinzani badala yake wasubiri wakati ukifika wenye dhamana na mamlaka watajitokeza kutoa maelekezo na ufafanuzi juu ya mdahalo lakini hoja za kuogopa mdahalo zife na zipuuzwe kwa namna yoyote ile.
Nawasilisha.
Deogratias Mutungi.