Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Kuna wanaume ambao kwa kutokujua wanadhani mwanamke anachohitaji ni fidia baada ya kuvunjiwa heshima, hivyo huwa wanawavunjia heshima wake zao na baadae kujitoza fidia kwa kuwanunulia zawadi kubwakubwa wanawake hao.
Wanawake huwa wanapokea zawadi hizi, lakini hii haina maana kwamba ndoa itaendelea kuwa ya amani na upendo. Mwanamke hata kama atapewa dhahabu yote duniani, kama atajua kwamba mumewe hamheshimu, ni wazi kwamba hatakuwa na furaha ya ndoa. Miongoni mwa mambo sita ambayo mwanamke akiyakosa huhisi kutindikiwa na kukosa furaha ya uhusiano ni heshima.
Kama haki ya mwanamke hailindwi na mwanaume, hata kama kuna kitu gani, ndoa ni lazima itakuwa ni ya kubahatisha. Mwanume anapokuwa na uhusiano wa kipapenzi nje ya ndoa yake, mwanaume anapomzuia mkewe kuamua masuala yake mwenyewe ambayo ni haki yake, kamwe mwanamke hawezi kuridhishwa na hayo na hata kama ndoa imejaa watoto wazuri wenye afya na akili na fedha nyingi zimeipamba nyumba yake.
Kama mwanaume ataonyesha kutojali kuhusu matamanio au ndoto za mkewe kamwe mwanaume huyo asitarajie kuwa mkewe atakuwa na upendo naye. Mwanamke huwa anatamani sana kuona mumewe anajali na kuyapa uzito matamanio au ndoto za mkewe. Kwa mfano mwanamke anapoonyesha kwamba, angependa kuanzisha shughuli labda ya biashara au wangependa wapate mtoto na mwanaume akaonyesha kutojali kuhusu matamanio hayo, kamwe mwanamke hawezi kutulia na kuwa na amani.
Kuna vitu au mambo ambayo mwanamke anayahitaji maishani, mahitaji hayo ni mengi yakiwemo yale ya msingi katika maisha na yale ya kawaida. Inatosha kusema kwamba, mwanamke anapogundua kwamba mumewe hajali juu ya mahitaji yake huwa hajisikii vizuri.
Kwa ujumla tunaweza kusema kwamba mwanamke huhitaji heshima katika utashi na matamanio yake. Anapogundua kwamba utashi na matamanio yake havizingatiwi na mumewe hawezi hata mara moja kumkubali mume huyo. Kumkubali hapa ina maana ya kumkubali na kumtambua.