Tusipoweka utaratibu wa kuwawajibisha wanasiasa tumekwisha

Tusipoweka utaratibu wa kuwawajibisha wanasiasa tumekwisha

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Kusema kweli maamuzi wa Rais Magufuli kuvunja mikataba tuliyoingia b yanatugharimu sana kama Taifa. Na yatatugharimu sana kama Taifa.

Hizi kesi tunazoshtakiwa na sasa tunalipa mabilioni zinatuumiza sana na itachukua muda mrefu sana kama Taifa kuanza kuaminiwa.

Mbaya zaidi zinatufedheesha sana mbele ya dunia maana wataalamu wetu wanapekekwa kutetea vitu ambavyo nina uhakika wanajua kabisa kuwa having sawa.

Ifike kipindi tuweke utaratibu wa kuwadhibiti viongozi hasa wa kisiasa katika kufanya maamuzi. Ushauri wa wataalamu ndo uongoze maamuzi yao kisheria na sio wao ndo wawaelekeze wataalamu waamue nini.
 
Yaani unashindwa kumlaumu msoga gang kuingiza nchi kwenye mikataba mibovu huku yeye akichukua 20%, unakuja kumlaumu MZALENDO aliekataa huo wizi
 
Kuna siku atakuja rais auze baadhi ya mikoa kwa nchi jjirani
 
Sasa kwasababu huo utaratibu hakuuweka Nyerere, mbona humlaumu pia kwa hilo?

Nyie ni wanafiki mnaochezea akili za wajinga tu, huku mkijua wazi kila kitu kitaamuliwa na waliopo.
 
Waambie kwanza CCM wawaondolee kinga ya kutoshitakiwa viongozi wao.
 
Kusema kweli maamuzi wa Rais Magufuli kuvunja mikataba tuliyoingia b yanatugharimu sana kama Taifa. Na yatatugharimu sana kama Taifa.

Hizi kesi tunazoshtakiwa na sasa tunalipa mabilioni zinatuumiza sana na itachukua muda mrefu sana kama Taifa kuanza kuaminiwa.

Mbaya zaidi zinatufedheesha sana mbele ya dunia maana wataalamu wetu wanapekekwa kutetea vitu ambavyo nina uhakika wanajua kabisa kuwa having sawa.

Ifike kipindi tuweke utaratibu wa kuwadhibiti viongozi hasa wa kisiasa katika kufanya maamuzi. Ushauri wa wataalamu ndo uongoze maamuzi yao kisheria na sio wao ndo wawaelekeze wataalamu waamue nini.
Aliye wapa makali,hatimaye alikimbia kwa kuogopa makali ya bisu alilolichonga mwenyewe na tena kulihifadhi ndani ya alangumu.Hatima ye yupo nje ya nyumba na nje ya fensi anapayuka mlio ndani na nje ya nyumba,aliyendani anakisu kikali na amepanga Kuwa Chija mlio ndani na nje ya nyumba yake.🤔.Mtu huyu timieleweje😂
 
Back
Top Bottom