Tusishangilie sana kwani leo tumecheza na Zesco B ila ile Zesco yenyewe inatusubiri Levy Mwanawasa Stadium tarehe 26 Septemba

Tusishangilie sana kwani leo tumecheza na Zesco B ila ile Zesco yenyewe inatusubiri Levy Mwanawasa Stadium tarehe 26 Septemba

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Wana Yanga SC wenzangu wala tusishangalie sana kwani kumbe tunacheza na Zesco B ( Kikosi cha Pili ) cha Zesco na cha Kushangaza bado wanatusumbua tu na haka ' Kagoli ' ketu Kamoja ka Kupewa na Mwamuzi. Wana Yanga SC Wenzangu tusikubali Kuyumbishwa na hawa Viongozi wetu kwani hawana la maana zaidi tu ya Kuwahonga Waamuzi ili Yanga SC ishinde lakini ukweli ni kwamba hatuna Timu ya Kufika mbali.

Kwa mfano Mimi sioni kwanini Yanga SC imesajili hawa Wachezaji wabaya kama akina Sibomana, Balinya, Balama, Lamine na Tshishimbi ambao ndiyo wanaongoza kwa Kucheza vibaya dhidi ya Zesco United leo. Hawa Wachezaji waondoke na kama Yanga SC tutaweza basi tuwaombe Simba SC baadhi ya Wachezaji wao ili watusaidie na tutafika mbali.

Wana Yanga SC tusiukubali huu Uongozi wa sasa kwani hauna Malengo mema na Timu yetu na nasikia wote kumbe ni Simba na mara nyingi sana huwa wanakuwa na Viongozi wa Simba SC hapa mjini. Na kama tutaendelea Kuwa nao hawa hadi January 2020 pale tutakapokuwa tunacheza na Simba SC basi natabiri tunaweza Kufungwa Goli 7 au hata 9 kwani hawa Viongozi watakuwa ' Wametuuza ' kwa Simba SC ambao ndiko Wanakokushabikia tokea walipokuwa Watoto.

Msipokubaliana na Mimi mwana Yanga SC mwenzenu An Eagle basi nahama Yanga SC na naenda Simba SC kwa Hasira.
 
Wewe Popoma toka lini ukawa Yanga au umebadili ID na team
 
Wewe Popoma toka lini ukawa Yanga au umebadili ID na team

Sina ID nyingine zaidi ya hii ya An Eagle na nashangaa mpaka leo hujui kuwa Mimi ni mwana Yanga SC lia lia kabisa Ndugu.
 
Ishia zako huko! Yanga gani wewe, si useme tu ukweli?

Nikupe Ushahidi gani kamilifu ili ujue kuwa Mimi ni mwana Yanga SC Mwenzako? Members wote wa JF hapa wanalijua hilo / hili.
 
Nhahahaa kwisha kazi!

Walaumiwe Kipa Metacha Mnata, Makame na Beki mwingine ambao kwa ' Upumbavu ' wao kwa Makusudi kabisa waliamua Kupoteza muda wakati walikuwa na uwezo wa Kucheza mpira na hata Kuongeza Goli la Pili ila Wao walijua wanawakomoa Zesco United ambao wanajua sana Mpira.

Nahamia rasmi Simba SC sitaki huu Ujinga na Upumbavu kabisa.
 
Karibu Simba tumejipanga kwa ubingwa na Kurudi tena Afrika
 
Karibu Simba tumejipanga kwa ubingwa na Kurudi tena Afrika

Na nyie Simba SC mkinizingua tu nahamia rasmi KMC ( Kinondoni ) au Namungo FC ( Lindi ) kabisa kama siyo hata Biashara United ( Mara )
 
Back
Top Bottom