Tusisifie sana shule za private zinafanya vizuri

Tusisifie sana shule za private zinafanya vizuri

CHAZA

kaka hiyo ni kweli tupu kuna mshikaji nilisoma naye a level alipata one ya tano shule ya serikali kwenda UDSM alikimbiza balaa tenda sio kwa msuli Kihiivyo,hakuna mwenye one ya tatu wala ya nne
 
Last edited by a moderator:
Ahsante mdau wa elimu. Ulichoongea INAWEZEKANA kina ukweli kwa asilimia kubwa maana kuna watu nilisoma walitoka O'level hizo shule zinazoongoza. Kuja A'level ikawa tofauti sana.

Lakini pia ukiwa kama mdau wa Elimu jitahidi kuandika vizuri. Kuchanganya r nal, pa kuweka h,kukatisha sana maneno.....
Haya tumekuelewa,shule za kata ndio zinaongoza kwa kufanya vizuri!!!
 
enzi za mwalimu private walienda kusoma waliofeli. ilikuwa aibu kusema unasoma private, lakini leo.....!

Mkuu wewe ni wa kitambo...! Hata enzi za mwinyi tu kuanzia '87 mpaka '95 ukisema wewe unasoma private watu washajua hata reasoning ability yako itakuwa very low lakini siku hizi mtoto anachaguliwa kwenda Mzumbe anakataa afu anaenda Marian.

Siku hizi kuna watoto wengi tu wanasoma hizi special schools lkn kiukweli hawastahili kabisa.
NB: kuna hatua za lazima inabidi zichukuliwe kuokoa shule za serikali
 
Wadau si shule zote zinafanyaja hujuma katika eneo la mtihani.Mapungufu ya shule za serikali yanafahamika.Zinaweza kuwa zinapata matokeo mazuri ambayo si sitahiki.Mjue kuna ata mbinu chafu huwa zinatumika kwa baadhi ya shule

Hata baadhi ya shule za serikali wanafanya cheating kinamna. Inakuwaje mwaka huu, wanafunzi biology (A-level) wanafundishwa practical ya kupasua mende tu, na mtihani ukija mende yupo. Mwaka jana labda ilikuwa ni kupasua chura au panya, mtihani ulipokuja wakakutana na chura au panya!

Haya nilihakikishiwa miaka ya 89-90, na walimu na wanafunzi wa shule fulani inayoheshimika kule Moshi. Ambapo walimu walikuwa wanajua mtihani kabla ili waandae specimen kwa ajili ya final exam, na ikawa wakijua, wanawa-brush wanafunzi kuhusu specimen hiyo.

Kule shinyanga, miaka michache tu iliyopita kulikuwa na udanganyifu katika mitihani ya darasa la saba ambapo mpaka mkuu wa mkoa na ma-afisa Elimu walihusishwa, lengo ilikuwa ni kuuinua mkoa ambao ulikuwa unafanya vibaya kwa muda mrefu. Kwa hiyo lawama zisiangukie shule za private tu, sometimes serikali yenyewe inajihusisha na udanganyifu.

Hata hivyo ninaamni kuwa kasoro hizo zinaweza kuwa zipo katika shule chache tu za serikali na private.
 
Kachumbi,

Mimi sio mdau wa elimu lakini nimesomesha watoto wangu kwenye shule za binafsi hivyo ni vizuri nikueleze uzoefu nilioupata.
Watoto wangu watatu wamesoma kidato cha kwanza mpaka cha sita kwa nyakati tofauti katika shule binafsi zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki mkoani Kilimanjaro.

UTARATIBU NA MITIHANI YA KUJIUNGA.

> Fomu za maombi zinatolewa mapema sana mara nyingine hata watoto hawajafanya mitihani ya kumaliza darasa la saba na zinajazwa na wazazi na kuzirudisha kunakohusika.

> Watoto wanaitwa kufanya mitihani ya kuwapima uwezo mapema sana mara tu wanapomaliza mitihani ya darasa la saba.

> Matokeo ya mitihani hii hutoka mapema kabla ya ile ya kumaliza darasa la saba na alama zao za ufaulu huanzia 50% sio chini kama ile ya serikali kwa darasa la saba.

> Mzazi unatakiwa kuthibitisha kuwa mtoto wako aliyefaulu mitihani hiyo atajiunga na shule aliyochaguliwa kwa kulipa mara moja ada iliyopangwa kwa kidato cha kwanza. Haya yote yanafanyika kabla ya matokeo ya mitihani ya darasa la saba.

Kwa kuzingatia utaratibu huu, watoto wengi wenye uwezo mkubwa darasani wanachukuliwa na shule binafsi kwani matokeo ya darasa la saba yanapotoka, wenzao huwa wamemaliza mchezo wa kupata wanafunzi wa kujiunga kidato cha kwanza. Katika muda wote watoto wanaposoma kwenye shule hizo wanaelewa kuwa wasipofikia kiwango cha chini cha ufaulu cha 50%,

hawezi kuvushwa kwenda kidato kingine bali mzazi unaitwa na kupewa taarifa hiyo kuwa mtoto wako anastahili kurudia kidato husika na kama mzazi ukiweka pingamizi basi unakabidhiwa mtoto wako umpeleke shule nyingine yoyote utakayoona inafaa.

Katika mazingira haya, wanafunzi wanaosoma shule za binafsi wanakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne na cha sita pasipo kuingiza rushwa na mambo mengine yanayofanana na hilo, mimi sina uzoefu na hilo ulilozungumzia.
 
Last edited by a moderator:
Udanganyifu upo tu sana, uzuri wanatumia mbinu nyingi kuhakikisha hamuelewi kinachoendelea, biashara ya shule ina faida sana hizo milioni 2, 3 na 4

Mnazolipa nadhani msingekuwa tayari kupokea matokeo mabaya ndio maana inafanyika kila namna matokeo yawe mazuri ila ukweli ni kwamba cheating zipo kwa sana ila si shule zote.
 
Kachumbi

Mleta hoja siungi mkono hoja yako hata kwa asilimia ndogo.mimi ni mwalimu wa goverment school.Through my experiance kinachohitajika hapa ni mambo mawili yafuatayo:

(1) Huduma nzuri kwa walimu.

(2)Nature ya wanafunzi wanaoenda kujiunga na shule hizi (je walipata elimu ya msingi kutoka wapi?)

Nijuavyo wenzetu wa private schools wanapokea wale tu wanaostahili kuwa form one kwa mchujo mkali.wakati shule za serikali wanalundika wajinga kwa hoja za kisiasa.

Hivi unategemea mtoto akiyeenda form one na alama 100/250 afanye miujiza?Alama less than 50 does he/she deserve to be in form one? Achilia mbali kutowajali walimu unategemea nini?
 
CHAZA

Jaribu ku focus! Wakifika chuo kikuu wanakuwa wa kawaida kwa sababu walikuwa wanabanwa na ghafla wanakuwa huru .Chini wanajituma kwa vile they always anxious extremely from teachers as well as their parents.
 
Last edited by a moderator:
born again pagan

Mie siwaelewi! Hizo hatua za kuokoa shule za serikali labda uwe mpango wa maendeleo wa miaka 40 (The next forty years) na hatua zianzie chini sio juu.mnatibu majani ugonjwa uko kwenye mizizi.Eleweni cream yote wanachukua private.

The rest wanaenda shule za kata.sidhani kama una uwezo na mtoto wako unamwona kichwa utampeleka akateketee shule za kata.Tambueni pia nyakati hizi mifumo ya kiuchumi na kisiasa imebadilika.Nchi ina matabaka.

Nina 46yrs of age nimesoma goverment school (Mawenzi sec 1988) mabadiliko yote yametokea naona. so nothing more nothing less hoja hapa ni mabadiliko ya mfumo kulingana na wakati.

Shule za kata kimfumo zipo ili kudanganya tabaka la chini only that na ndo maana mfumo wa alama umebadilika. Distinction, merit credit, Pass and fail kundi kubwa hapa linaangukia pass and fail haya utailaumuje serikali kama mwanao kaandikiwa pass?
 
Last edited by a moderator:
Ighombe

Ndugu mwalimu ulichosema ni kweli lakini bado haufuti ukweli wa kwamba kuna shule za private zinafanya udanganyifu kupamba biashara zao.

Hata mkibisha ila pesa ndo zinaongea.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu mwalimu ulichosema ni kweli lakini bado haufuti ukweli wa kwamba kuna shule za private zinafanya udanganyifu kupamba biashara zao. Hata mkibisha ila pesa ndo zinaongea.

Ndio nchi hii ni kubwa hatuwezi ku match uniformly from Mtwara to Kagera. but in private school qualitatevely ukweli unabaki pale pale.
 
Wewe kama ulishndwa wewe ulishndwa tu, huwez kunambia juhud za ufundshaj private na serikal unalingana,
 
Wewe kama ulishndwa wewe ulishndwa tu, huwez kunambia juhud za ufundshaj private na serikal unalingana,
 
Ufaulu mzuri wa shule za private ni artifical. Ukifuatilia sana utakuta wanaoingia form one ni 160 lakini wanaofanya mtihani wa form four ni 90. Wengine wanalazimishwa kufanya mtihani kama private candidates.
Ni kweli waalimu wanalipwa na wanafanya kazi katika mazingira mazuri.
Katika shule (za Private), waalimu wana sign performance bond.
 
Ukweli unaouma ni kuwa shule nyingi za private na baadhi za serikali wanafunzi wanawezeshwa majibu siku za mitihani ili waweze kufaulu vyema.1.Wasimamizi hupewa maagizo kutoka kwa maafisa elimu waliopewa chochote ili kuwafaulisha 2.Wasimamizi hupewa fungu kuwapatia majibu wanafunzi 3.Wasimamizi kukarimiwa kwa vinywaji na vyakula ili kuwapa ahueni wanafunzi 4.Wanafunzi kujichangisha na kuwapa wasimamizi 5.Wazazi (wenye vyeo vya juu) kutoa maelekezo ama kujichangisha kuwapa wasimamizi ama maafisa elimu.MATOKEO YA KIDATO CHA SITA NA VYUO HUWA YA KUSIKITISHA!
 
Back
Top Bottom