Kachumbi,
Mimi sio mdau wa elimu lakini nimesomesha watoto wangu kwenye shule za binafsi hivyo ni vizuri nikueleze uzoefu nilioupata.
Watoto wangu watatu wamesoma kidato cha kwanza mpaka cha sita kwa nyakati tofauti katika shule binafsi zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki mkoani Kilimanjaro.
UTARATIBU NA MITIHANI YA KUJIUNGA.
> Fomu za maombi zinatolewa mapema sana mara nyingine hata watoto hawajafanya mitihani ya kumaliza darasa la saba na zinajazwa na wazazi na kuzirudisha kunakohusika.
> Watoto wanaitwa kufanya mitihani ya kuwapima uwezo mapema sana mara tu wanapomaliza mitihani ya darasa la saba.
> Matokeo ya mitihani hii hutoka mapema kabla ya ile ya kumaliza darasa la saba na alama zao za ufaulu huanzia 50% sio chini kama ile ya serikali kwa darasa la saba.
> Mzazi unatakiwa kuthibitisha kuwa mtoto wako aliyefaulu mitihani hiyo atajiunga na shule aliyochaguliwa kwa kulipa mara moja ada iliyopangwa kwa kidato cha kwanza. Haya yote yanafanyika kabla ya matokeo ya mitihani ya darasa la saba.
Kwa kuzingatia utaratibu huu, watoto wengi wenye uwezo mkubwa darasani wanachukuliwa na shule binafsi kwani matokeo ya darasa la saba yanapotoka, wenzao huwa wamemaliza mchezo wa kupata wanafunzi wa kujiunga kidato cha kwanza. Katika muda wote watoto wanaposoma kwenye shule hizo wanaelewa kuwa wasipofikia kiwango cha chini cha ufaulu cha 50%,
hawezi kuvushwa kwenda kidato kingine bali mzazi unaitwa na kupewa taarifa hiyo kuwa mtoto wako anastahili kurudia kidato husika na kama mzazi ukiweka pingamizi basi unakabidhiwa mtoto wako umpeleke shule nyingine yoyote utakayoona inafaa.
Katika mazingira haya, wanafunzi wanaosoma shule za binafsi wanakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kufanya vizuri katika mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne na cha sita pasipo kuingiza rushwa na mambo mengine yanayofanana na hilo, mimi sina uzoefu na hilo ulilozungumzia.