Tusitegemee makubwa zaidi kutoka kwa Aziz-Ki!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
Naomba kuweka wazi kwanza, mimi ni mwanachama kindaki ndaki wa Dar Young Africans.

Kadi ya uanachama namba: TZDAR03067119

Tusipoteze muda twende moja kwa moja kwenye suala la msingi.

Kwenye soka kuna kitu kimoja cha ajabu sana. Mchezaji anaweza kuwa anajua sana soka (skills & Intelligence) ikawa vizuri sana lakini anaweza kukosa tija Uwanjani.

Ninachomaanisha, kwenye majukumu yake asiweze kukupa namba nzuri (magoli & usaidizi).

Ili tuelewane ninachosema, kwanini tusitegemee makubwa kutoka kwa Aziz Ki, lazima tuangalie utendaji wake huko alikopita kwenye timu zote.

Amecheza timu zifuatazo;[emoji1484]

1. CD RAN ROQUE
Mechi: 24
Goals: 02

2. OMONIA NICOSIA
Mechi: 17
Goals: 0
Assists: 01

3. ASEC MIMOSAS
Mechi 30+
Goals: 04
Assists: 02

4. ARIS LIMASOL
Mechi 5
Goals 0
Assists 0

Wazungu wanasemaga, "Numbers don't lie".

Wakimaanisha ukiwa unafanya vizuri, takwimu zitakubeba na kudhihirisha ubora wako.

Je, wewe kama mwanasoka ambae unafuatilia soka vizuri, hizo namba za Azizi Ki hapo juu zimekuridhisha?

Je, hizo namba hapo juu zinaendana na ubora wake ambao tuliambiwa kabla hajaja?

Je, unadhani kama alishindwa kufanya vizuri kwenye timu zote alizocheza huko nyuma kwanini iwe Yanga ndiyo sehemu ataonyesha uwezo?

Nimeepuka kuongea kwa mihemko na nimeweka namba zake kama msingi wa kujenga hoja yangu kuwa Azizi Ki tusitegemee maajabu makubwa kutoka kwake kwa sababu hata huko alikotoka hakuwa bora kiasi hicho (kutokana na namba - michango, magoli & usaidizi)

Narudia tena kwa Aziz-Ki tuliaminishwa vibaya . Alikua amepaishwa sana kana kwamba ni mchezaji wa daraja la juu wakati kiuhalisia namba zake uwanjani hazionyeshi hilo.

Mimi binafsi, naamini mpaka sasa tulichokiona kwa Azizk Ki ndicho hicho pekee ambacho anaweza kufanya. Hakuna kipya zaidi ambacho ataonyesha. Hakuna suala la kumvumilia, hapo ndipo uwezo na ufanisi wake ulipoishia.

Sitotegemea usaidizi 6, au magoli zaidi ya 6 kutoka kwa Aziz Ki katika msimu huu akiwa Yanga.

Aziz Ki, akifikisha hizo takwimu mnitafute nimeweka laki mbili dau mezani.

Kama kuna mtu angependa kupinga hoja yangu, aje na ukweli mtupu nimekaa pale.[emoji117]
 
Aziz ki siyo forward, ni kiungo anatimiza mahitaji ya kukaba, kunyang'anya mipira na kupandisha timu ili strikers wafunge.

Ikitokea kapata nafasi ya kufunga ni sawa.
Kipa tu asipofunga ni suala la kawaida sio kiungo hata assist tu hamna, hata mabeki wanaendaga kupiga vichwa mipira ya kona msimu unaisha ana goli 7
 
Tatizo Utopolo wazee wa kudandia panton ferry yaani Mnyama asimtake mchezaji kwa ajili ya matumizi yake na wao wanadandia tu kama mabumunda kwa kukomoana
 
Naunga mkono hoja yako mleta uzi.

Hata mechi ya jana naamini kama Feisal angesogezwa juu alipokuwa anacheza Ki kidogo Yanga wangeweza kupata attempts nyingi zaidi kutokana na hulka ya Feisal kujaribu lango.
 
Wewe ni kocha? Unayajua majukumu anayotimiza uwanjani? Au unaangalia asist tu? Aziz ki anatimiza kile anachokitaka kocha atimize na sio kama unavyotaka wewe, anaweza asiasist lakini akatimiza majukumu ya kiufundi ndani ya uwanja kwa uwepo wake unalijua hilo? Wewe macho yako yanaangalia kutoa asist ndo aonekane bora kwako?Acheni mambo ya kipuuzi matokeo ya sare yamefanya kila mmoja awe kocha
 
Naunga mkono hoja yako mleta uzi.

Hata mechi ya jana naamini kama Feisal angesogezwa juu alipokuwa anacheza Ki kidogo Yanga wangeweza kupata attempts nyingi zaidi kutokana na hulka ya Feisal kujaribu lango.
Pamoja na feisal alikua chini kidogo mara chache alizosogea juu alijitahidi kupitisha mipira ya hatari kuliko aziz ambae alikua juu muda wote, aziz ki alitakiwa kupigwa sub mapema aingie nondo alafu bangala apige 6 na feisal asogee juu zaidi kwa namba 10 pale
 
Aziz ki ni namba 10 ilo eneo kazi yake ni kutengeneza nafasi zankufunga na kufunga ikitokea nafasi so far bado aziz ki hajaonyesha matarajio waliokua nayo watu kwake labda tuseme tumpe muda
 
Kila mchezaji sasa ndo ubora wake utaonekana kwenye haya mashindano.
 
Huyu ndo walikuwa wanasema yeye mmoja ni sawa na gunia moja la debe 8 lilojaa akina C.C. CHAMA.
Madhara yake uwanjani ni madogo sana.
Heri namba 10 aachiwe Fei kazi yake inapimika, anaweza amua matokeo ya mechi lakini kwa huyu KI aliyetulaza macho wiki nzima hakika ni mtumishi wa kawaida (hewa) kama Ambundo tu.
 
Acha utopolo aziza key ni kiungo mshambuliaji.....kufunga,,ku-assist n muhimu kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…