Naomba kuweka wazi kwanza, mimi ni mwanachama kindaki ndaki wa Dar Young Africans.
Kadi ya uanachama namba: TZDAR03067119
Tusipoteze muda twende moja kwa moja kwenye suala la msingi.
Kwenye soka kuna kitu kimoja cha ajabu sana. Mchezaji anaweza kuwa anajua sana soka (skills & Intelligence) ikawa vizuri sana lakini anaweza kukosa
tija Uwanjani.
Ninachomaanisha, kwenye majukumu yake asiweze kukupa namba nzuri (magoli & usaidizi).
Ili tuelewane ninachosema, kwanini tusitegemee makubwa kutoka kwa Aziz Ki, lazima tuangalie utendaji wake huko alikopita kwenye timu zote.
Amecheza timu zifuatazo;[emoji1484]
1. CD RAN ROQUE
Mechi: 24
Goals: 02
2. OMONIA NICOSIA
Mechi: 17
Goals: 0
Assists: 01
3. ASEC MIMOSAS
Mechi 30+
Goals: 04
Assists: 02
4. ARIS LIMASOL
Mechi 5
Goals 0
Assists 0
Wazungu wanasemaga, "Numbers don't lie".
Wakimaanisha ukiwa unafanya vizuri, takwimu zitakubeba na kudhihirisha ubora wako.
Je, wewe kama mwanasoka ambae unafuatilia soka vizuri, hizo namba za Azizi Ki hapo juu zimekuridhisha?
Je, hizo namba hapo juu zinaendana na ubora wake ambao tuliambiwa kabla hajaja?
Je, unadhani kama alishindwa kufanya vizuri kwenye timu zote alizocheza huko nyuma kwanini iwe Yanga ndiyo sehemu ataonyesha uwezo?
Nimeepuka kuongea kwa mihemko na nimeweka namba zake kama msingi wa kujenga hoja yangu kuwa Azizi Ki tusitegemee maajabu makubwa kutoka kwake kwa sababu hata huko alikotoka hakuwa bora kiasi hicho (kutokana na namba - michango, magoli & usaidizi)
Narudia tena kwa Aziz-Ki
tuliaminishwa vibaya . Alikua amepaishwa sana kana kwamba ni mchezaji wa
daraja la juu wakati kiuhalisia namba zake uwanjani hazionyeshi hilo.
Mimi binafsi, naamini mpaka sasa tulichokiona kwa Azizk Ki ndicho hicho pekee ambacho anaweza kufanya. Hakuna kipya zaidi ambacho ataonyesha. Hakuna suala la kumvumilia, hapo ndipo uwezo na ufanisi wake ulipoishia.
Sitotegemea usaidizi 6, au magoli zaidi ya 6 kutoka kwa Aziz Ki katika msimu huu akiwa Yanga.
Aziz Ki, akifikisha hizo takwimu mnitafute nimeweka
laki mbili dau mezani.
Kama kuna mtu angependa kupinga hoja yangu, aje na ukweli mtupu nimekaa pale.[emoji117]
View attachment 2381780View attachment 2381782