Halafu wakishahudhuria ndio shida za wafanyakazi zitatatuliwa?
Acheni mizaha na wafanyakazi, jibuni hoja za CHADEMA na sio hizi blah blah za kuhudhuria.
CHADEMA wameshasema wakishika madaraka watapandisha mishahara na kwa kuanzia watafidia malimbikizo ya nyongeza ya mishahara yote ambayo wafanyakazi waliyopunjwa na serikali ya Magufuli toka 2015-2020. Wafanyakazi wamesikia hilo, wamelielewa na watafanya maumizi sahihi siku ya kupiga kura.
Sasa, CCM imebakia na propaganda za kale badala ya kuja na sera mbadala ya madhubuti.