Tusiwalaumu sana Polisi kuzuia mikutano ya kisiasa, tatizo kubwa ni wakuu wa Wilaya na mikoa

Tusiwalaumu sana Polisi kuzuia mikutano ya kisiasa, tatizo kubwa ni wakuu wa Wilaya na mikoa

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Hili binafsi ningeomba viongozi wa vyama vya siasa muelewe vizuri kabisa na hata kama mtahudhuria kikao chenu anachoitisha msajili wa vyama vya siasa na Polisi, mwambieni ukweli kuhusu hili.

Kwa bahati nzuri sana kabla ya kuikacha CCM na kuamua kubaki kufundisha kunoa vijana,nimewahi kua mjumbe wa kamati ya siasa ya chama wilaya na mkoa. Tatizo la kujaza mapolisi kwenye vyumba vya mikutano ni mashinikizo kutoka kwa Wakuu wa Wilaya na mikoa, RPCs, RCOs, OCDs na OC CID hawa wote hupokea maagizo kutoka kwa wanaojiita wenyeviti wa kama za ulinzi na usalama. Polisi wanaokaidi maagizo hayo hufanyiwa fitina kuhamishwa vituo ao kuondolewa kwenye uongozi. Kwa wapenda vyeo huona isiwe taabu wanatii maagizo ya wanasiasa hawa.

Wakuu wa Wilaya na mikoa wanaelewa kabisa kungekuwa na katiba mpya hivi sasa kusingekuwa na vyeoo hivyo, Ukuu wa Wilaya na mkoa ni nafasi za kikoloni enzi za chama kimoja ambao kazi yao ilikua kukilinda chama. Huwezi kua kada wa chama tawala halafu ukahudumia wananchi wote na wa vyama viingine kwa usawa, katiba ya Warioba ilitaka tubakiwe na makatibu tawala yaani RAS na DAS wawe wawe wawakilishi wa Rais maeneo husika na wasiwe Makada.

Hivyo kuona polisi wanakomaa sana kuzuia mikutano ya siasa ni mashinikizo ya wakuu wa wilaya na mikoa ambao nao wakati mwingine wanapewa taarifa na viongozi wa CCM ngazi za wilaya na mikoa. Nimefanya kazi za chama cha mapinduzi naelewa nini nasema.

Hivyo wakati mnakutanishwa na msajili wa vyama vya siasa msiache kuusema huu ukweli.
 
Lazima walaumiwe. Kwani hawana wabobezi wa sheria wa kuwaeleza hili ni sawa na hili sii sawa?
 
Polisi wanafundishwa na miongozi mingi tu juu ya majukumu yao,unafikiri Polisi akitumwa kufanya jambo ambalo linapingana na miongozo ya kazi yake na jambo hilo akakataa kulitenda au kulifanya atakuwa amefanya kosa ?
Je ikiwa atafukuzwa kwa kukataa kutenda hilo jambo ,sheria za nchi zinamlinda au hazimlindi ?
Hebu tuendeleze madai ya Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya inayoendana na wakati.
 
Siyo kweli, tatizo kubwa ni fikra mbovu za makamanda wa polisi.
Nani mwenye madaraka, uwezo na utaalam kwenye usalama wa nchi zaidi kati ya IGP na RC au DC?
 
Kuna polisi hawapendi usumbufu wa wanasiasa na ukute wakati mwingine hawajapewa chochote, hutii amri tu za wenyeviti wa kama za ulinzi na usalama
 
Siyo kweli, tatizo kubwa ni fikra mbovu za makamanda wa polisi.
Nani mwenye madaraka, uwezo na utaalam kwenye usalama wa nchi zaidi kati ya IGP na RC au DC?
Upolisi kazi ya lawama ndugu, ukiogopa lawama kutofanya kazi utaiacha.
 
Back
Top Bottom