Tusiwapishe viongozi wetu wakuu barabarani

Tusiwapishe viongozi wetu wakuu barabarani

Quemu

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2007
Posts
984
Reaction score
133
Pengine kwa sababu suala la utanuzi na uongezaji wa barabara jijini Dar haliko juu kwenye "to-do" list ya nchini yetu; na kwamba barabara chache zilizopo zimehelemewa na mafuriko ya magari yanayoingizwa nchini kila siku; basi hatuna budi kutoupisha msururu wa viongozi wetu wakuu wanapotaka kutumia barabara kiduchu hizi.

Nao hawana budi kuendesha bumper-to-bumper kama wakazi wengine....

Yaani jana nimekwama kwenye foleni iliyoganda, halafu mara kuna kiongozi akaja na squad yake, basi wengine wote tukasukumwa sukumwa kwenye mitaro kana kwamba sisi ni maji machafu. Ilimradi mheshimiwa apite ili awahi kwenda kufuturu. Kwani nasi si tumefunga pia...ebo!
 
Na kweli!! utafikiri wanamwahisha mgonjwa hospitali!!!
 
Kweli tusiwapishe. Mathalani jana nikitoka Arusha kuja Dar, magari yalisimamishwa barabarabi kwa dakika 45 hadi saa nzima kumpisha Jaji Mkuu aliyekuwa akiongoza msafara wa JK uliokuwa nyuma ya JM kwa takriban dakika 20. Kwa jinsi hii kweli tutaendelea. Kwani tukipishana nao kutakuwa kitu gani?
 
...barabara chache zilizopo zimehelemewa na mafuriko ya magari yanayoingizwa nchini kila siku;

Yaani jana nimekwama kwenye foleni ...

Mkuu, ulikuwa na gari lako au kwenye usafiri wa wengi?
 
Pengine kwa sababu suala la utanuzi na uongezaji wa barabara jijini Dar haliko juu kwenye "to-do" list ya nchini yetu; na kwamba barabara chache zilizopo zimehelemewa na mafuriko ya magari yanayoingizwa nchini kila siku; basi hatuna budi kutoupisha msururu wa viongozi wetu wakuu wanapotaka kutumia barabara kiduchu hizi.

Nao hawana budi kuendesha bumper-to-bumper kama wakazi wengine....

Yaani jana nimekwama kwenye foleni iliyoganda, halafu mara kuna kiongozi akaja na squad yake, basi wengine wote tukasukumwa sukumwa kwenye mitaro kana kwamba sisi ni maji machafu. Ilimradi mheshimiwa apite ili awahi kwenda kufuturu. Kwani nasi si tumefunga pia...ebo!

Jaribu wewe na sisi wote tutakuiga, tena kwa ushauri wangu wewe ukisikia king'ora wewe zima gari lako halafu kaa kimya ndani ya gari lako. mimi mhhhhhhh nafikiri watagwaya wenyewe.halafu tupe taarifa ilikuaje.kama itakua poa basi tutakuiga

radikali
 
Honk if you are angry! Wakipigiwa honi kote wanakopita wataelewa huu ujinga wao ni kero kubwa kwetu sisi walalahoi. Watanzania tumekuwa wapole mno kwa muda mrefu sasa tumegeuka mazezeta.
 
Back
Top Bottom