Quemu
JF-Expert Member
- Jun 27, 2007
- 984
- 133
Pengine kwa sababu suala la utanuzi na uongezaji wa barabara jijini Dar haliko juu kwenye "to-do" list ya nchini yetu; na kwamba barabara chache zilizopo zimehelemewa na mafuriko ya magari yanayoingizwa nchini kila siku; basi hatuna budi kutoupisha msururu wa viongozi wetu wakuu wanapotaka kutumia barabara kiduchu hizi.
Nao hawana budi kuendesha bumper-to-bumper kama wakazi wengine....
Yaani jana nimekwama kwenye foleni iliyoganda, halafu mara kuna kiongozi akaja na squad yake, basi wengine wote tukasukumwa sukumwa kwenye mitaro kana kwamba sisi ni maji machafu. Ilimradi mheshimiwa apite ili awahi kwenda kufuturu. Kwani nasi si tumefunga pia...ebo!