Je yupo mtu anaweza kuwatukana wazazi wake....!?
Mama zake wadogo...!? Mama zake wakubwa...!? Baba zake wadogo na wakubwa...!? Mashangazi na wajomba...!?
Kwa utamaduni wetu wa kitanzania,Hawa wote ni kundi la wazazi.Hata wanapokuwa wamekwenda kinyume Kuna namna ya kuwashitaki kwa staha na suluhisho likapatikana.
Je, viongozi wetu wa nchi tunawachukuliaje...!? Unajua kuwa Hawa pia ni kundi la wazazi...!? Unajua utabisha kwa sababu maadili yako na malezi hayako sawa na unaweza kusema nasumbuliwa na upungufu wa elimu,lakini fahamu kuwa elimu yangu pia ni ya chuo kikuu Kama ilivyo elimu ya vijana wengi wanaotukana viongozi wa nchi kwenye mitandao kwa kufikri kuwa wamepata ukombozi wa kielimu.
Mtu anayeweza kumtukana Rais ama viongozi wengine walioko juu yake anao pia uwezo wa kumtukana Baba yake na Mama yake maana hana maadili hata kidogo.
Ukitaka kujua msingi wa unachosoma hapa,rudi kijijini kwenu kajaribu kumtukana mwenyekiti wako wa kitongoji na hako ka diploma kako halafu ulete majibu hapa.
Vijana tubadilike! Vinginevyo tutabaki kulaumu watu bila mafanikio!