Tusker Challenge Cup Updates

Tusker Challenge Cup Updates

Tumeshapigwa chini tayari! Kura za kihuni za kwenye bahasha, Yanga tumeokata iliyoandikwa OUT! Kila la kheri watani wetu. Ndipo pa kumalizia hasira hapo.

Mshaanza visingizio sijui kura za kihuni... fungu la kukosa la kukosa tu..
 
Dakika ya 3 Simba ( Mnyama mkali ) 1 watoza ushuru kutoka Uganda URA 0 he he he!
 
Tumeshapigwa chini tayari! Kura za kihuni za kwenye bahasha, Yanga tumeokata iliyoandikwa OUT! Kila la kheri watani wetu. Ndipo pa kumalizia hasira hapo.

Hii kanuni ya kura haiko fair, ni kheri hata ingepigwa penalti moja moja. 🙁
 
Hii kanuni ya kura haiko fair, ni kheri hata ingepigwa penalti moja moja. 🙁

Mkuu huwezi kupiga penati nje ya mchezo, labda ingefanyika replay....namaanisha timu haziwezi kuingia uwanjani na kupiga penati peke yake.
Hata hivyo Yanga walipaswa kushinda ili kuepuka ile kura.
BTW: Kanuni za kura zilikuwepo kabla hata ya mashindano haya kuanza.
Update: HT Simba 1 URA 1.
 
habari toka : Nifahamishe.com Habari za michezo za Tanzania
Simba yaangukia pua Tusker Cup, yatolewa nusu fainali

BAO la pili lililofungwa katika dakika ya 54 na Erick Obua wa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), lilitosha kuiwezesha timu hiyo kutinga fainali ya Kombe la Tusker na kuitupa Simba nje ya michuano hiyo.

Obua alifunga bao hilo la pili na hivyo kuifanya URA itoke uwanjani na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza kwa kasi, huku kila timu ikitafuta nafasi ya kufunga bao la haraka, lakini walikuwa Simba waliopata bao la mapema lililofungwa na kiungo Henry Joseph, katika dakika ya nne ya mchezo huo, baada ya kupokea pasi safi ya Ulimboka Mwakingwe.

Ikiwa imesalia dakika moja timu kwenda mapumziko, kosa lililofanywa na beki Ramadhan Wasso la kutoa pasi isiyokuwa na macho liliweza kuwapa bao la kusawazisha URA, lililofungwa na Mbiru Samson. Mpaka mapumziko timu hizo zilikuwa sawa kwa mabao 1-1.

URA itasubiri mshindi wa nusu fainali ya kesho itakayozikutanisha timu za Mtibwa Sugar ya Tanzania na Tusker ya Kenya.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kocha wa Simba, Talib Hilal, alisema amekubali matokeo, lakini alilalamikia uamuzi wa mchezo wa leo kwa kusema haukuwa mzuri.

Endapo Tusker itashinda mchezo wa leo, timu hiyo na URA zitaweka rekodi ya kucheza fainali kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miezi mitano katika ardhi ya Tanzania. Tusker na URA zilicheza fainali ya Kombe la Kagame mwaka huu, ambako Tusker ilitwaa ubingwa.

Simba: Deogratius Bonaventure, Salum Kanoni, Ramadhan Wasso, Meshack Abel, Kelvin Yondan, Henry Joseph, Haruna Moshi ‘Boban', Mohamed Banka, Mussa Hassan ‘Mgosi', Emeh Izuchukwu na Ulimboka Mwakingwe.

URA: Dhamira Abel, Mbiru Samson, Kyombe David, Owino Joseph, Karangwa John, Maweejje Tommy, Ochan Patrick, Kigozi Ismail, Muwanga Martin na Obua Erick.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=591898&&Cat=6
 
Simba yaangukia pua Tusker Cup, yatolewa nusu fainali

BAO la pili lililofungwa katika dakika ya 54 na Erick Obua wa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), lilitosha kuiwezesha timu hiyo kutinga fainali ya Kombe la Tusker na kuitupa Simba nje ya michuano hiyo.

Obua alifunga bao hilo la pili na hivyo kuifanya URA itoke uwanjani na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tunashukuru bwana. Kumbe Masatu ni shabiki na si mpenzi wa mpira. Kufungwa akaingia mitini..........
 
wowowo kidedea mpoo mpo mpompompompo wowowo kidedea.... mumeo akifa kwa ukimwi mke lazima ufuate alah... out kwa timu zote ah kumbe bado mtibwa asalaaale
 
Simba kwa njaa yaani kama mngewatangazia wale wachezaji kuwa wakishinda meschi ya fainali huo mshiko wa milioni arobaini wangegawana wao mmeona shiidaaaa, alafu timu inavurunda mnataka kupigana wenyewe kwa wenyewe dah kweli simba albadri yanga mpira bwana, thats y nimegundua mashabiki wa simba wanazeeka mapema maana sura zao zimekunjamana kama wazee wa miaka 90 kumbe ni vijana wa miaka 30-40 dah hiyo inatokana na kukasirika all the tym mnakunja sura tu once simba inapocheza,, yani furaha kidogo maudhi mengi hahahaha hamieni yanga bwana huku ni buruuuuuuudani
 
Back
Top Bottom