Wandugu wana JF na wapenzi wa Tusker Lager, kuna kitu kinaniumiza kichwa kuhusu hii bia tamu ya tusker ambayo zamani TBL walikuwa wanazalisha under licence na sasa naona SBL.Je kipi kilitokea mpaka hawa SBL wawe ndio wanaimiliki au kuzalisha?. Kwa upande wangu sina imani sana na uwezo wa SBL kwenye kuzalisha bia. Kuna mwenye tetesi ya kilichotokea? :mad2:
.
Zemu hii issue ni ngumu kuielewa kwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe, inahitaji utaalamu japo kidogo kujua nini haswa kinaendelea, na kulikuwa na vita kwenye media, iliyoitwa Vita vya Bia 'Beer War'
Gemu lilianzia kama ifuatavyo, kwanza Tusker ni bia ya Kenya, ya Tanzania ni Ndovu. Kiwanda cha Kibo kule Moshi kilichokuwa kinamilikiwa na EABL ndio kilikuwa kinatengeneza Tusker, kulifanyika makubaliano fulani au hostile take over kati ya TBL na EABL kuwa kila nchi itengeneze bia ya mwenzake na kuiuza nchini kwake. Hawakuuziana kwa pesa bali waligawana kila kiwanda kimiliki asilimia 20% chenzake, yaani 20% EABL imilikiwe na TBL (SUB) nao wamiliki 20%, TBL watengeneze Tusker, EABL watengeneze Castle. Ndipo Ghafla TBL wakakifunga kiwanda cha Kibo na kuwamwaga wafanyakazi karibu wote wakapigwa chini, menejiment wakahamishiwa TBL. Mpaka hii leo sijui kilitokea nini, lakini Tusker ikazalishwa TBL.
EABL akahisi TBL inaihujumu brand yake ya Tusker na kupromot zaidi Safari na Kilimanjaro, ndipo wakafanya mazungumzo na SBL kuwapa tenda ya kutengeneza Tusker, TBL wakawakatalia EABL kujitoa ubia wao mpaka wakafikishana mbele ya vyombo vya sheria, tume ya Ushindani FCC hadi mahaka ya usuluhishi London. Wakati huo TBL ikakodi vijana kuyahujumu matangazo yoyote ya Tusker ikiwemo kuya vandalize na kuwalazimisha ma ajenti wao wasipokee Tusker, ilikuwa vita kweli, mastatement na mastatement yakitumwa magazetini.
Mwishowe EABL na SBL wakatoa statement vita imeisha kwa amani na hakuna vita yoyote baada ya kufikia makubaliano kwa amani. TBL nao wakatoa statement yao, hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa.
Kwa bahati mbaya mimi sinywi kabisa bia (haina maana sinywi pombe), sikujua kabisa hatima ya Tusker mpaka leo ulipouliza.
Huo ndio uelewa wangu mdogo.