kijana wa mtaa
Member
- Mar 9, 2009
- 16
- 1
tusker wale majaji wote ni proffessional hakuna vihiyo ndo mana wasanii wetu walioenda kule wanavurunda kwasababu TANZANIA KILA KITU NI SIASA, JUMA NATURE ALISHAWAHI IMBA :NCHI IMESHAUZWA HII"
bila kupendelea, watanzania walioenda kutuwakilisha wanachemsha!!!
hata wangekuja BSs wangetolewa mapema tu!!
hawana sauti, hawako interesting, ili mradi tu si wasanii wa muziki kweli, tanzania tuna vipaji vingi tu, usanii sio lugha, mbona makeba aliimba malaika na ikauza?
Lakini kuna karembo hapo Ka Kenya, kanajiita Shrek or something, i think she has a great voice.
Thanks Haika......kwa kweli bila mapendeleo sioni hao warembo wa TZ wakienda mbali. kazi yao ku-tweng...mbona wana kizungu fresh sana tena chenye accent!!!! they are not star material. period! the ugandans deserve to win again!!! wote watatu!
Oh! poor smatta, you talk of warembo mbele ya watz, hujawaona wale wasichana wawili wakibongo, yaani carlo na mwenzie wanavyong'ara? hakika wale wasichana Mungu kawaumba aisee, hata wasiposhinda lakini wamewakilisha dada zetu wa kibongo. ni wazuri sana.
nilivyoona hata hivyo, mwaka huu Uganda watachukua tena, yule dada mwenye sura ya kiume anayeimba na sauti kama ya kisauz africa, hakika anaimba sana. atachukua hiii.
kelvin wa tz, nilikuwa napenda atoke siku ya kwanza tu alivyoenda, kwasababu alikuwa hajui anachofanya, alikuwa haonekani kama yuko kwenye mashindano, alikuwa hajui kimombo anajifanya kuongea cha kwenye miziki ya african americans...hahaha, alikuwa anatuaibisha. nilifurahi nilivyoona muda wa kuondoka umefika.
atakayefuata kuondoka, ni yule mtu wa majani wa Rwanda, hahaha, anaimba akinyata kama anavuta bangi.nilicheka hadi nilikaa chini.
atakayefuata kwa hapo, kama hatajirekebisha, ni Carlo, ni mzuri sana wa sura, anajua kimombo, lakini hatoi sauti na anaonekana kama ana hofu kidogo. labda kama atajitahidi, ndo ata watatangulia wale waimba rege wa Rwanda,pamoja na ka Nina.
that girl other than Carlo, anaweza akatuwakilisha kufika mbali. anaweza sana.
kuna kaschana kamoja hivi ka kikenya, ni kazuri lakini hakawazidi wabongo. kana imba vizuri lakini wiki iliyopita kalichemsha.
nikija kwa ng'ang'alito, atatoka, hajui anachofanya, anafanya utani tuuu, anafikiri anaigiza pale. anachekacheka kama kashoga fulani hivi.(nilisikia kenya mashoga wanataka haki kama south na wamejitokeza wanajulikana). I hope that young boy is innocent na kurembua kule hakutakuwa na matatizo kwake.watu wasije wakamuelewa vibaya. anatakiwa achague moja, kama ni comedy, comedy, kama kuimba aimbe, si kila mtu anapenda mwanaume anayerembuarembua.
hata mimi ilinishangaza, kuna bias sana katika hii competition, they failed terribly on the planning, uli notice kwa season 2 it was definate that a UG was to win, I am 101% sure that this time ni mtanzania ndie ataibeba, it doesnt matter if he has a talent or not.
Nimeona hata nyimbo za kiswahili wanaimba isipokuwa lugha inayotumika pale na majaji hata washiriki wenyewe ni Kiingereza. Nafikiri msimu mwingine kama ingewezekana wangehamisha venue isiwe nchi ya Kenya; waweke Uganda, Tz etc kuwaamsha watu wa nchi hizo. Ni maoni na mtazamo wanguKiongozi hapo hata mimi naku suport. Na kingine ni kuwa hawa wenzetu wanatumia zaidi lugha ya kiingereza na hiyo ni advantage kwao coz hata nyimbo zinazoimbwa pale ni kiingereza tu. Sisi mpaka ufikrie kwa kiswahili halfu utafsiri kwa kiingereza.
nathani iluminata na carol wameondolewa kwa kukosa wapigaji wa kura kutoka kwa watanzania hakuna anaehamasisha kwa kiasi fulani watanzania wapigie ma participant wetu that why wamekuwa wakiingia katika kinyan'ganyiro cha kuondolewa kwa kura za watazamaji na si jugdes ila nime prefer hasa kwa huyu iluminata ni realy good musician kama dada yake Rene lumira hata carol she was doing much great lakini kelvin bado hata Nyimbo nyingi alizoimba alikuwa si tu akikosea bali pia baadhi ya maneno hayakuwa akiyatamka inavyopaswa jifunze hata kwa nyimbo zingine si lazima utumie nyimbo za p-square pekee yake
Hi wajameni, nimekuwa najiuliza hii tusker project fame inakuwaje tuanze kwa kuvurunda wakati bongo flavor yetu inakubalika sana hapo jirani. Please assist me to think outside the box for i'm totally confused as to why we are not doing better on this.
Wadau tafadhali