Katiba zipo lkn zinakiukwa makusudi.
Mzee Mtei alifata katiba ya chama akakaa vipindi viwili vya miaka mitano mitano kama inavyosema katiba ya chama akatoka.
Akaja Bob Makani na yeye akafuata katiba kwa kukaa pia vipindi viwili vya miaka mitano mitano kama Mtei akatoka. Na hiyo ya kina mzee Mtei na hayati Bob Makani ndio demokrasia iliyosababisha chama kiitwe "Chama cha demokrasia na maendeleo".
Sasa huyu mfanyabiashara anawaona wenzake waliomtangulia wote ni kanyaboya. Ndomaana kaamua kung'ang'ania kitini bila kufuata katiba.
So acha wale wanaoona kuwa katiba ya chama inasiginwa makusudi waende mahakamani.