Tutafakari hizi kauli mbiu za shule nyingine siyo

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,491
Reaction score
8,304
Salaam wapendwa.
Kila nikipita naona vibao vya fundi maiko vikielekeza shule zetu. Sasa najiuliza yale maneno wanayoweka pale yanawaumbia nini watoto wetu mioyoni mwao? Mie nimesoma shule isiyo na kibao wala ukuta.

Elimu Ni nuru,
Elimu Ni ufunguo wa maisha,
Elimu Ni urithi bora.
Elimu Ni mafanikio.

Mimi shuleni nilikuwa naenda tu ili kuepuka maswali ya kijinga ya mzee baba, maana alikuwa ananiuliza vitu ambavyo hata yeye hana majibu. Mfano akirudi anakuuliza kwanini mwewe kachukua vifaranga? Yule mbuzi alipokata kamba kaenda wapi? Mimi nitajuaje Sasa!!Bora nikashinde shuleni tu.
Shule ni kitu kingine na maisha ni kitu kingine.

Shuleni tunajifunza kuchanganyika na wengine na kuvumiliana tu, siyo kupeana funguo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hakika wewe ni mzarendo haswaaa.

Sent from my DUB-LX1 using Tapatalk
 
Huo ndio mwanzo wa watoto kuharibika.Ina maana hamna maisha nje ya Elimu wakati ni uongo uliopiliza.Sawa na na Sisi tulivyopata Uhuru na wimbo wa maadui watatu umasikini,ujinga na maradhi.Matokei yake tunaendelea kuwa wajinga,masikini na wagonjwa kadri siku zinavyozidi Kwenda mbele.
 
Au mzee anaweza kukuuliza 'mbona sijawahi kukuona na msichana' aise ni bora uende skonga tuu.
 
Huo ndio mwanzo wa watoto kuharibika.Ina maana hamna maisha nje ya Elimu wakati ni uongo uliopiliza.Sawa na na Sisi tulivyopata Uhuru na wimbo wa maadui watatu umasikini,ujinga na maradhi.Matokei yake tunaendelea kuwa wajinga,masikini na wagonjwa kadri siku zinavyozidi Kwenda mbele.
Tunawadanganya kweli mkuu. Anasoma weeeeeee!akitoka hapo ajira hapati na akiipata ni kwa masimango na kimshahara kidoooogo cha laki 5. Shule miaka 10 inamaana kila mwaka alisomea elfu 50 tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam wapendwa.
Kila nikipita naona vibao vya fundi maiko vikielekeza shule zetu. Sasa najiuliza yale maneno wanayoweka pale yanawaumbia nini watoto wetu mioyoni mwao? Mie nimesoma shule isiyo na kibao wala ukuta.

Elimu Ni nuru,
Elimu Ni ufunguo wa maisha,
Elimu Ni urithi bora.
Elimu Ni mafanikio.

Mimi shuleni nilikuwa naenda tu ili kuepuka maswali ya kijinga ya mzee baba, maana alikuwa ananiuliza vitu ambavyo hata yeye hana majibu. Mfano akirudi anakuuliza kwanini mwewe kachukua vifaranga? Yule mbuzi alipokata kamba kaenda wapi? Mimi nitajuaje Sasa!!Bora nikashinde shuleni tu.
Shule ni kitu kingine na maisha ni kitu kingine.

Shuleni tunajifunza kuchanganyika na wengine na kuvumiliana tu, siyo kupeana funguo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa, ndio maana wanasema elimu na akili ni vitu viwili tofauti.

Unaweza kuwa na akili lakini huna elimu au ukawa na elimu ukawa huwa akili (wengi wapo hapa).

NB: Kuna watu hawana vyote (elimu na akili) ila wana ubongo tu. [emoji3]
 
Back
Top Bottom