Soka Ndio Maisha Yangu
Member
- Nov 27, 2024
- 43
- 127
Mpira wa Tanzania ni mgumu sana, mpira wetu ni wa kikwetu kikwetu, wakati mwingine unapowaambia watu kuwa mpira wa Tanzania hauangalia uwezo wa makocha watu wanabisha, mfano mzuri moira unaochezwa na timu yangu ya Simba utasema kuna kocha mle?
Au gusa achie twende kwao kuna mpira pale? Mpira unachezwa sana nje, kocha ni kisingizio tu hapa bongo.
Hapa bongo hata umlete mchezaji gani kutoka Ligi Kuu ya Uingereza au Hispania, wazee wa timu hizi za jadi wakishajua jina lake, jina la mama wa mchezaji huyo, wakachukua jasho la jezi, wakachukua nyasi au mchanga alipokanyaga mchezaji huyo basi amekwisha.
Mifano iko mingi sana, Simba ilimleta Dejan mshambuliaji mzungu ambaye analijua goli sawa sawa, huko alikotoka alikuwa anapachika mabao sio kawaida, amekuja bongo hata dana dana ameshindwa kupiga mzungu yule.
Kituko kingine ni hiki, Simba ilimsajili Leonel Ateba, huyu ni bull striker kweli kweli, alianza kwa kasi sana ya kupachika mabao, lakini kadri siku zinavvyozidi kwenda Ateba Mbida akawa joka la kibisa.Kila akiletewa ndani ya 18 anakosa ama anajigonga mwenyewe.Kuna mtu hapa JF aliwahi kuwaomba viongozi wa simba waangalie Ateba ameshapigwa misumari.
Yanga nako kuna yule Prince Dube, huyu ni striker haswaaa, haihitaji kumwelezea sana kwa sababu Simba na Yanga wote wanamjua.Alipokuwa Azam ameshawafanya vibaya wote hao tena mabao ya kimataifa.
Dube naye akakanyaga, wenzake wanagusa wanaachia wanakwenda kwao akipewa yeye anaanguka, Gusa Achia Twende Kwao ikifika kwa Dube kapokonywa au kaanguka.
Ateba na Dube wajanja waliona hiyo wakawapeleka kwenye upako na mitandao ya kijamii ikawaonyesha mtu mmoja huyo huyo ndio kawafanyia upako Ateba na Dube, ina maana simba na Yanga wanajuana.Kwa sababu aliyewafanyia dawa ni mtu mmoja.
Matokeo ya upako ni nini? Ateba akatumbukiza mawili na alikuwa aondoke na mpira ile juzi basi tu ndio mambo ya mpira, ghafla Dube alianzia kule Congo na sasa hivi kaondoka na mpira jana vs Mashujaa.
Huu ni ushahidi tosha kuwa mpira wa TAnzania una mambo ya hatari sana kuliko tunavyodhania, watu wanaumizana ili waonekane koko, Clatous Chama naye amekwisha kabisa, hana lolote zaidi ya kujivunja mkono apumzike.Matarajio ya Yanga kwake yamepotea kabisa, wengine wanadiriki kusema wamrudishe alikotoka.
Kutokana na hili nina wasiwasi sana wachezaji kama Joshua Mutale, Jean Charles Ahoua, Augustine Okajepha, Mavambo, Mukwara na Kijri watakuwa wameingia katika mfumo wa washirikina, washirikana hawa aidha wanatoka ndani ya timu ama nje ya timu.
Wewe, Joshua Mutale namna anavyocheza sasa hivi ni kituko kabisa uwanjani, Mutale sio SGR tena, Mutale na nyavu anapaisha? Hapana.
Huenda hata Elie Mpanzu akaingia katika kikaango kile kile.Simba iangalieni hilo.