Tutaje sababu zinazoweza kusababisha gas ya kupikia kulipuka na kuleta maafa

Tutaje sababu zinazoweza kusababisha gas ya kupikia kulipuka na kuleta maafa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
1. Kubandika kitu na kukisahau halafu ukaenda dukani. Masufuria yetu yenyewe kwa sasa ni mepesi sana dakika kumi ukijisahau ukatoka unaweza kurudi kukuta chakula kimeungua chote. Sasa baada ya Chakula huwa ni zamu ya sufuria kuyeyuka na kisha kwenda pale kwenye pipe inapoungwa na kisha inalipuka..

2. Kingine ni ulevi, aisee kama unaishi ki bachelor na una jiko la single plate nakushauri acha kabisa kupasha chakula ikiwa umelewa acha kabisa kupika ukiwa umewaka Mapombe huko kwa vyumba vyetu vidogo Hivi gas sijui huwa inachochea kausingizi ukisema uegeshe tu umekwisha..

3. Pipe kukunjika na Hatimaye leakage.. Pipe inyoke vizuri hasa Kwa majiko ya plate mbili.. Pipe isijikunje.

4. Kuingia na jiko la mkaa au sigara karibu na jiko la gas..

Tuzidi kuwa makini.Hata Ka gas kadogo tu kakilipuka ukaonyeshwa vipande vilivyolitoboa bati ndo utaamini kwamba gas ni hatari mno.
 
Tangu nishuhudie nyumba imeungua sababu ya jiko la gesi la plate 2 sina hamu na majiko hayo,na bahati yao walipona wote,haya majiko mengi ya mchina hata hayaeleweki,bora lile la mtungi tu
 
kwa sasa hivi hakuna gesi yenye nguvu sana.ila kama nyumba yako ina madirisha ya vioo ni hatari kulipuka kama ina vuja
 
2.kingine ni ulevi, aisee kama unaishi ki bachelor na una jiko LA single plate nakushauri acha kabisa kupasha chakula ikiwa umelewa acha kabisa kupika ukiwa umewaka Mapombe huko Kwa vyumba vyetu vidogo Hivi gas sijui huwa inachochea kausingizi ukisema uegeshe tu umekwisha..
Hii point imenigusa sana nilienda kwa mangi nikaunga na bia. Uzuri sikufunga mlango jirani alihisi kitu kinaungua akaokoa.
 
kwa sasa hivi hakuna gesi yenye nguvu sana.ila kama nyumba yako ina madirisha ya vioo ni hatari kulipuka kama ina vuja
Username yako na ulichokoment naona vinaendana,Sina uhakika kama unatania au upo serious,kama upo serious hakuna gesi iliyopunguzwa nguvu gesi formula yake ni ile ile miaka yote
 
Hii ya kubandika sufuria halafu ukajisahau ishanitokea kama mara mbili.

Mara ya kwanza nilikaa nje harufu naisikia ila nikawa nahisi ni kwa jirani.
Niliporudi ndani nakuta samaki ashakuwa majivu.

Mara ya pili nilikuwa nina mafua sikusikia harufu kabisa.
Naingia jikoni nakuta maharage yanaungua tuu.
 
Username yako na ulichokoment naona vinaendana,Sina uhakika kama unatania au upo serious,kama upo serious hakuna gesi iliyopunguzwa nguvu gesi formula yake ni ile ile miaka yote
Gas imepunguzwa nguvu mjomba,gas ya 1990s siyo hii,hii ikitoka 40cm toka chanzo imeisha nguvu
 
Hii ya kubandika sufuria halafu ukajisahau ishanitokea kama mara mbili.

Mara ya kwanza nilikaa nje harufu naisikia ila nikawa nahisi ni kwa jirani.
Niliporudi ndani nakuta samaki ashakuwa majivu.

Mara ya pili nilikuwa nina mafua sikusikia harufu kabisa.
Naingia jikoni nakuta maharage yanaungua tuu.
Mkuu unachemsha marage kwenye gas
 
Back
Top Bottom