The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 9,436
- 10,944
Serikali imetoa mapendekezo ya Bajeti yake Kwa mwaka 2024/25 yenye zaidi ya Shilingi Trilioni 49.3 na kuainisha vyanzo vya pesa hiyo na matumizi yake.
Ni vyema Sasa Wananchi na wadau tujikite kutoa maoni ambayo yatasaidia mjadala wa Bajeti Ili kama Kuna tozo unaona haiko sawa uibainishe na njia Mbadala.
Binafsi Kwa sehemu kubwa Bajeti ya Serikali nimeona Iko vizuri isipokuwa kasoro ndogo ndogo.
Mojawapo ya tozo iliyopendekezwa na ambayo haijabainishwa wazi jinsi gani itatozwa na watatozwa kina nani ni hii inaitwa tozo ya miundombinu (infrastructure levy).Waziri anasema itaingia mfuko wa Dharura Ili kupata hela za ku deal na majanga lakini haijabainishwa wazi kama itatozwa kwenye Mafuta,au Kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri au Kwa utaratibu gani.
Wakati wa mjadala ni vyema ielezwe itakuwa kiasi gani na watakaotozwa ni kina nani.
Aidha account hiyo in case pesa haijatumika usalama wa pesa hizo itakuaje? Na nani watakuwa na amri ya kutoa hizo hela? Na Je tunaweza kufahamishwa ni kiasi gani kinatarajiwa kupatikana?
Kimsingi maswali ni mengi maana isijekuwa ni account ya kupigia pesa zetu Kwa sababu Nchi hii Viongozi Kwa sehemu kubwa hawaaminiki.
Naomba kutoa hoja 👇👇