Nadhani tunachojifunza ni kuwa Waafrika bado tuna mawazo duni, ukabila udini na wakati mweingine ujinga ujinga tu!
Mzee Madiba kumpa tafu JZuma ni katika kupunguza speed ya kuvunjika kwa ANC, basically alishaona kuwa aking'ang'ania principle zake ANC itamegeka megeka, ingawa binafsi haafiki ya JZ, bado aliona ni lazima kumuunga mkono ili chama kiendelee kutawala na pia Sauzi kusijekuwa na machafuko ya aina yeyote.
Si mnakumbuka mzee JKambarage alivyompiga madongo ya nguvu Mzee Malecela baada ya kufahamu ni tishio wa changuzi lake?- Hizo ndo siasa za kiafrika! Na milele tutaendelea kuwa ombaomba na vidampa wa wazungu na wengineo, hadi hapo akili zetu zitakapo kaa sawa.