Tutakukumbuka Mzalendo ambaye hukupenda kusikia ukweli na hoja kinzani

Tutakukumbuka Mzalendo ambaye hukupenda kusikia ukweli na hoja kinzani

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Mwaka 2015 mara baada ya Mh. Rais kuapishwa, kila mwezi takwimu zenye kuvunja rekodi kuhusu makusanyo ya kodi zilikuwa zikitangazwa na watu wakiweka vifua mbele kwamba nchi yetu inaelekea kuwa donor country.

Muda ulivyozidi kwenda, tulishuhudia sekta mbalimbali zikisinyaa. Biashara za kati zilitoweka na Waziri wa Fedha wa wakati huo alikiri biashara kufungwa.

Taasisi na Jumuiya za Kimataifa zikajikuta zinalumbana na Serikali kwenye takwimu. Wizara ya Fedha ilikuwa ikitoa taarifa zenye kuonyesha uchumi unakuwa kwa kasi wakati Taasisi za Kimataifa zikionyesha kwa wakati fulani, uchumi ule ulikuwa haufiki hata asilimia 5%. Ikapita miswada ya kuzuia machapisho mbalimbali na asasi za kiraia zikafungwa midomo.

Hilo likiendelea, serikali ikazidi kujinadi kwenye usafiri wa anga kwamba inatengeneza faida kumbe hali ni tofauti. Kwenya huduma za Afya tukaambiwa Serikali tukaambiwa ilitenga fedha zaidi ya bil. 200 kwa ajili ya dawa mwaka, kumbe haikupeleka hata senti. Mapambio yakaendelea kufurahisha Watanzania.

Wakati watu wakistaajabu hayo, ukafika uchaguzi ambao haukuwa na hamasa na aliyekuwa Mh. Rais alipiga kampeni chache lakini yeye na Wabunge wake walishinda kwa kishindo. Itakumbukwa waliokuwa wasimamizi wa Uchaguzi walionywa, kama umepewa hiyo nafasi na mimi, ole wako ashinde mwingine.

Wale waliochagua upinzani miaka ya nyuma walitahadharishwa, wakichagua upinzani, maendeleo ni ndoto.

Ajira kwa vijana, hali ikawa mbaya zaidi. Watunga sheria na sera, waliwahimiza vijana kujiajiri lakini hawakuandaa mazingira ya kujiajiri.
Pamoja na haya, hofu ikatanda. Mitandao ikazimwa. Kukosoa kukakoma maana matokeo yalikuwa wazi. Mapato hayakutangazwa tena. Watu mitaani walinong'ona hali ilivyo. Wafanyabiashara wakubwa wakakodi vijana wawauzie mali zao maana maduka hayakuwa na maana tena.

Pamoja na hayo, JPM alikuwa Mzalendo wa aina yake.
 
Mimi huwa najiuliza kwanini picha za Ikulu ya Chato hazioneshwi? Inawezekana kuwa kwenda zake aliwakataza zisioneshwe?
 
Jpm alikuwa ni jizi, liongo, lenye hofu ya kukosolewa na aliyejivika kot la uzalendo..
ni wachache ndo walikuwa wanalijua ilo, na pia hao wachache walinyamazishwa kwa mkono wa mahakamamagufuli na wasio onekana.
 
Msingi wa sasa hivi, ni kuwa na Serikali inayokubali kusikiliza maoni ya wananchi na kuwepo na uwazi.

Tuondoke kwenye takwimu danganyifu.

Tujiridhishe hesabu kamili ya vijiji visivyo na umeme, vituo vya afya vilivyojengwa, uwepo wa dawa, upatikanaji wa maji Safi, hali ya shule zilivyo ili tusikurupuke kama ubungo maana ndio hali iliyopo kwa kiasi kikubwa, idadi ya walimu na madaktari maana ajira siku hizi ni za watendaji vijiji.

Turuhusu uwekezaji wenye tija na tutengeneze mazingira ya ukuaji wa sekta binafsi.
 
Wanasema atengewe siku maalumu kumkumbuka na aingizwe kwenye somo la historia na apewe topic nzima kuhusu yeye.

Kuna watu wanashindwa kusoma alama za nyakati waendelee kujinasibisha na huyo mzee tu.
 
Mwaka 2015 mara baada ya Mh. Rais kuapishwa, kila mwezi takwimu zenye kuvunja rekodi kuhusu makusanyo ya kodi zilikuwa zikitangazwa na watu wakiweka vifua mbele kwamba nchi yetu inaelekea kuwa donor country...
Oyaa imetosha sasa tuacheni apumzike.
 
Back
Top Bottom