888I
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 472
- 581
Katika taifa ambalo mgombea kama Boniface Mwabukusi — sasa ni Rais wa TLS — anasimulia jinsi kura zake zilivyokusanywa, kupuuzwa, na mwisho kuchomwa moto huku akiambiwa “nenda ukalalamike popote,” mtu yeyote anayesema atalinda kura 2025 bila kutanguliza mabadiliko ya sheria na mfumo, ama anajidanganya ama anatufanya wajinga.
Na hapa ndipo napata wasiwasi mkubwa na kauli za vyama kama ACT-Wazalendo kusema kwamba mwaka 2025 “tutalinda kura.”
Swali: 👉🏾 Mwaka 2020 mlilinda kura? Kama ndiyo, mbona wabunge wenu walinyang’anywa ushindi waziwazi na bado mlikaa kimya?
👉🏾 Kama hamkulinda kura 2020, je, nini kimebadilika leo mnavyoahidi kwamba mtaweza 2025?
Ulinzi wa kura siyo kiapo cha usiku wa kampeni. Ni matokeo ya:
1.Tume huru ya uchaguzi.
2.Mahakama zisizotisha kwa gharama.
3.Sheria zinazoruhusu scrutinizing ya matokeo bila pingamizi za kiutawala.
Kama haya hayajafanyiwa kazi kabla ya Uchaguzi, basi ulinzi wa kura ni kiapo tu kinachopotea hewani siku ya matokeo na hamtafanya kitu labda kama mmeahidiwa na watawala ili kuonesha kuna Uchaguzi.
Mfumo Huu Hauwezi Kulinda Kura
-Returning Officer anaweza kukataa matokeo yako na kusema “tayari nina matokeo” — hakuna wa kumgusa.
-Mahakama inakuambia ulete milioni 12 ndiyo usikilizwe.
-Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasema “hatuhusiki, una kesi mahakamani.”
Katika mazingira haya, kura haziwezi kulindwa kwa mabango wala mikutano ya kampeni.
Kama Hatufanyi Mabadiliko Kabla ya Uchaguzi — Tutarudia Historia
Vyama vyote vya siasa vya upinzani vina wajibu wa kuacha ndoto za kushinda kwenye uwanja wa majeruhi, halafu waje kulalamika baadaye.
-Hakuna maana ya kuandaa timu ya mpira wakati refa anachezea timu pinzani.
Tunachotaka Kusikia ni Hiki:
1.Tume huru ya uchaguzi (Huru kweli kweli).
2.Mfumo huru wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura mnajitahidi hapa kidogo..
3.Uwazi wa matokeo kuanzia kituo hadi Taifa.
4.Sheria mpya za uchaguzi kabla ya Uchaguzi.
5.Na mchakato wa kweli wa Katiba Mpya.
Kama haya hayajafanyika, mtu yeyote atakayesema atalinda kura 2025 hana tofauti na tapeli wa kisiasa.
Kura hazilindwi kwa ujasiri wa maneno. Zinalindwa kwa mfumo na sheria.
✍🏾