Omary - Msamalia
JF-Expert Member
- Jan 19, 2020
- 2,079
- 4,521
Huu sio utabiri ila ndio suluhu ya mwisho ya yanayoendelea huko jikoni.
Inasemekana Hayati Magufuli alikuwa tayari amekubali kuuanza upya mchakato wa kuunda katiba ya Wananchi na hili alipata ushauri wa Kina kutoka kwa Mshauri na Mlezi wake Hayati Benjamini, moja ya mependekezo makubwa ya Magufuli ilikuwa ni kurekebisha Sheria zinazohusu Rushwa na ubadhilifu ikiwemo kurekebisha kipengele kiwahusuho viongozi wakuu wastaafu na ulinzi wanaoupata wakiwa madarakani, na jambo zito zaidi lilikuwa ni Juu ya muundo na mustakabali wa Muungano wetu.
Hata siku zake za mwisho aliwahi kukutana na Hayati Mzee Sharif Hamad na Hussein Mwinyi kuhusu maendeleo na mustakabali wetu kama Nchi.
Kuhusu mpasuko ndani ya CCM ni kuwa yametokea makundi makuu mawili kiitikadi moja linataka CCM ambayo inafuata Ujamaa Mamboleo na moja inataka CCM yote Iwe chama cha kibepari kamili na hata wabadili sheria za ardhi waruhusu wageni wapate Ardhi kwa namna yoyote ile, wanataka njia kuu za kiuchumi zimilikiwe na watu wachache na wengine wapewe ajira tu, Pia kuna Kundi ambalo linataka CCM ibaki kama ilivoasisiwa na wananchi wote waendelee sawa sawia.
Kwa sasa haya makundi yanatengeneza ushawishi wao ndani ya taasisi nyeti za serikali na vyombo vyetu vya dola, na pengine kundi moja linaweza kushawishi umma kusimam dhidi ya Serikali na kujaribu mapinduzi kama yaliyotokea Sudan na Afrika Magharibi ambapo majeshi yaliyowaunga mkono wanaoipinga serikali.
Mwisho kwa vyama pinzani vya siasa, msitumike kama eneo la kukimbilia endapo wafuasi wa kundi moja wataamua kuwapisha wengine, ila muwaache wapambane hadi mwisho, vita vyao vinaafya kwa mustakabali wa taifa