Wandugu,
Hii taarifa ya Raila Odinga kususia uchaguzi wa marudio Kenya unaotarajiwa kufanyika October 26 si habari njema kwa wakenya.
Ikumbukwe kuwa Rails na wenzake was NASA hawawezi kususia uchaguzi wa marudio bila kuwa na mbinu mbadala wa suala hili, na hali inajionyesha dhahiri kwamba wapo tayari kuwaamrisha wafuasi wao hata kufanya vurugu ili nchi isitawalike.
Natabiri vurugu zinaweza kuwa kubwa zaidi ya ilivyotokea mwaka 2007.
Raila si wa kupuuzwa hata kidogo na madai yake ya kutaka mabadiliko kwenye tume ya uchaguzi ni ya msingi kabisa. Jambo la ajabu sana hapa kwa nini hii tume iliyovuruga uchaguzi wa kwanza iendelee kung'ang'ania kuendesha uchaguzi wa marudio. Na ajabu zaidi tume hii inaungwa mkono kwa asilimia Mia moja na chama tawala cha Jubilee chini ya Uhuru Kenyatta. Kwa vyovyote vile NASA chini ya Odinga wapo sahihi kabisa kususia marudio ya huu uchaguzi vinginevyo watajitumbukiza kwenye mtego na watashindwa kujitegua.
Suluhisho pekee la kunusuru hali hii ya machafuko ambayo tunaitarajia kutokea ni kwa hii tume inayijiita isiyo na mipaka kujiuzulu, vinginevyo machafuko hayaepukiki. Halahala Wakenya, mti na macho.