Hili tulitarajie, mahakama ya juu kabisa ikiwa na majaji saba ilitengua maamuzi ya tume huru isiyo na mipaka ya Kenya iliyomtangaza Uhuru Kenyatta mshindi. Mahakama iliona mapungufu katika mchakato mzima wa uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kukiuka katiba ya Kenya. Mbaya zaidi maafisa wa tume walishindwa kuithibitishia mahakama juu ya kuonyesha tena idadi halisi ya kura zilizopigwa.
Tatizo kubwa lipo kwenye tume ya uchaguzi ambayo kwa vyovyote vile ndio iliyohusika kuvuruga uchaguzi.
Kwa hakika tume hii ilipaswa kujiuzulu bila kusubiri kushinikizwa kwa sababu upande wa upinzani wa NASA ukiongozwa na Raila, umeshasema hauna imani na tume hii na imeorodhesha majina ya watendaji walio ndani ya tume hii ambao hawana imani nao, ajabu ni kwamba chama tawala cha Jubilee kinaunga mkono tume hii iendelee kusimamia uchaguzi.
NASA wako sahihi kabisa kuikataa hii tume na watakuwa wajinga sana Kama wataingia kwenye uchaguzi kwa kusimamiwa na tume hii.
Inakuwaje refaree aliyevuruga mchezo apewe tena mechi ya marudio? Hii ni ajabu.
Tume hii ya Kenya kama itasimamia tena uchaguzi wa marudio, amani itatoweka Kenya sababu upande wowote utakaoshindwa hautakubaliana na matokeo. Kwa vyovyote vile NASA watasema hawakubaliani na matokeo kwa kuwa tume ilithibitika mahakamani kuwa haikuwa na uwezo wa kusimsmia uchaguzi, Jubilee wao watasema tume ilitishwa na wafuasi wa upinzani.
Cha muhimu hapa ni atafutwe refaree mwingine baaasi.