Tutarajie nini matokeo kidato cha nne 2013?

Tutarajie nini matokeo kidato cha nne 2013?

Wana JF,

Mwenye taarifa sahihi naomba anifahamishe lini matokeo ya kidato cha nne (IV) yatatolewa? ili niweze kuondokana na shinikizo la kuwaza pasipokujua siku wala saa.

Wasalaam

Mdau
 
Vumilia, nilisikia wiki hii, kama sivyo basi jitahidi mpaka wiki ijayo, si unajua wabongo mpaka wachakachue kwanza
 
Pole kuwa tu mpole jipe moyo kwa matokeo yeyote uyakubali uajipa ugonjwa bureee
 
Zilizopo Form 6 kabla hawajapiga Pper lazma yatoke,tunaskizia kesho.(Ukipanda Mchicha unavuna Matembele)
 
Sio matokeo...
Sema Madudu ya 4m 4 lini...?!
Ijumaa ndugu mambo hazarani,,lazima tumtafute mchawi tena nawambia..
Ngoja niwe mtabiri hapa:
zero aka sufuli aka point 34 na 35 ni 47%..
Div 4 aka wapata vyeti visiofaa kitu ni 32%..
2ngoje kesho...
 
Waboreshe malipo kwa walimu pamoja na shule za serikali mana ndo zinaongoza kwakuwa na matokeo mabaya
 
Tayari yako kitaa...una div 4 pts 34..ni pm mkubwa
 
Hivi wewe Magwero mbona una roho mbaya kiasi hiki?Unatoa utabiri wa watu kufaulu na sifuri unadhani unayoyasema ni mazuri?Badala ya kujiuliza hao watanzania wenzetu "watakaofeli" tuwasaidiaje wewe unawawazia mabaya?

Magwero mind your manners please!
 
Kwa mujibu wa baraza la mithiani kama mambo yataenda kama yalivyopangwa...kesho matokeo ya kidato cha nne yatatoka na kwa taarifa za awali wasichana wameng'ara zaidi ya wavulana wakati huo huo shule za private zimezidi kuwa juu kuliko zile za serikali tena za kata...!
 
Haitusaidii taarifa kama hii, ungesubiri yatoke ndo utuhabarishe
 
Haitusaidii taarifa kama hii, ungesubiri yatoke ndo utuhabarishe

sio haikusaidii tu bt huenda pia haikuhusu that y haikushughulishi na haitakua hivyo bt ni muhimu kwa yule inayomuhusu
 
Back
Top Bottom