Tutiririke vitu vya msingi kuvijua unaposimamia ujenzi kama mmiliki, haya mafundi tuambieni ukweli 1 2 3

Tutiririke vitu vya msingi kuvijua unaposimamia ujenzi kama mmiliki, haya mafundi tuambieni ukweli 1 2 3

Thinker96

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2011
Posts
321
Reaction score
81
Habarini wakuu,

Kuna vitu ambavyo mafundi tunaomba watuambie katika kusimamia ujenzi tuvijue ili tupate nyumba kulingana na gharama iliyotumika kwa kuanzia:-

1-Mgawanyo wa hatua za Ujenzi kwa mgawanyo mkubwa na mgawanyo mdogo. Mfano Mgawanyo mkubwa ni Boma-Kuezeka-Kuhitimisha. Ila mgawanyo mdogo ndo una mambo mengi unawaze kuelezewa na wataalamu wenyewe kwamba ukiishia hapa kujenga unaweza kupumzika na kujikusanya na kuendelea wakati mwingine bila nyumba kudhurika.

2-Viwango vya malighafi na uchanganyaji wake kwa mfano saruji mchanga na kokoto kwa matumizi tofauti tofauti mfano saruji kwa ajili ya mtenganisho wa tofali na tofali kwa kozi huchanganywa na mchanga ndoo ndogo za lita kumi mfuko mmoja kwa ndoo 16/18/20 na vitu kama hivyo.

3-Mafundi na wataalam wa kada ya ujenzi mtaongezea pamoja na wasimamizi wazoefu mtatueleza mfano namna ya kwenda kutambua ubora wa malighafi kama tofali kipimo gani tutatumia na mambo mengine mengi ka,i kwenu wajuvi wa mambo uwanja ni wenu twende kazi 2025+ ni kazi bora tu sio kazi mbovu . . .
 
Ukitaka kwenda sambamba na mafundi wa kibongo usizoane nao!!! Siku za mwanzo mwanzo kabisa, tafuta kakosa kadogo tu wabomoreshe afu waambie next time watalipia gharama za materials.

Make sure unawalipa kidogo kuliko walichofanya na uwe active kwenye site. Jifunze mambo madogo madogo kama ratio, pima maji, angles nk.

Siku nyingine unaenda na fundi mwingine mzoefu mjanja mjanja ukifika site unamuita engineer (omba wasiwe wanamjua). Muombe engineer wa uongo akague jengo pia atembeze bit la kutosha kwa mafundi.
 
Du hii nimeipenda
 
Karibuni Nile house designs!!

kwa sasa tumeboresha huduma zetu Ili kukufikia mteja zaidi, tunatengeneza michoro na muonekano (3d) wa nyumba, majiko, sebule, bars, mandhari( landscape ) na huduma yoyote unayotaka kuanzisha,
Wasiliana nasi Leo tukupe huduma unayohitaji,

Call/Whatsapp 0715477041
 
Back
Top Bottom