Tutofautishe bei ya mazao, wingi wa mavuno na kuuza mazao nje ya nchi

Tutofautishe bei ya mazao, wingi wa mavuno na kuuza mazao nje ya nchi

Nnaona kuna upotoshwaji wa hali ya juu wa hali ya chakula nchini. Si kawaida yangu kuanzisha thread, ila hili imebidi nianzishie thread.

Kwanza kabisa ni declare interest, mimi ni mdau wa kilimo kwa miaka mingi, hivyo nnachoandika hapa ni kutokana na uzoefu wangu kwenye kilimo.

HOJA KUU
Watu wengi wanachanya bei za mazao kuwa juu na upatikanaji wa mazao nchini. Wengi wamejawa na hofu ya kutokea njaa, watu kukosa chakula hasa vijijini, etc....kubwa zaidi ni watu wa mjini kuogopa kununua chakula kwa bei ya juu.

Ikumbukwe mazao yanayolalamikiwa sana hapa ni mahindi na mpunga. Kwa kuwepo field, sioni kama kunaweza tokea njaa yoyote Tanzania, sababu watu walilima, na watu wanaendelea kuvuna.

Swala la kupanda bei lina pande mbili, kubwa ikiwa gharama kubwa za mbolea na mazao kiduchu yaliyotokana na wengu walioshindwa nunua mbolea.

Wengi mtawaza kwamba serikali izuie kuuza nje ili bei za vyakula zishuke, hiyo itakuwa kumuua mkulima at the expense ya walaji. Ikumbukwe mwaka jana mwishoni serikali ilinunua kwa wingi mahindi kwa wakulima na bado hawajaanza toa stock kwenye maghala yao. Hivyo mkulima aendelee uza kwa bei inayomlipa, popote kwenye soko, serikali ina stock ya kutosha kuuza ndani, muda ukifika itoe stock yake.
U mwongo na unapanga uongo. Sentensi zako mbili zinadhihiri. Hakutakuwa na njaa kwa sababu watu walilima na wana endelea kulima. Mazao yalipungua kwa sababu ya kupanda kwa bei ya mbolea na wakulima hawakumudu. Ukweli ni kuwa hakuna mazao ya kutosha kwa sababu ya kupungua kwa mvua na kupanda kwa mbolea. Kusafirisha mazao nje kutamshawishi mkulima kuuza yote na kuishiwa chakula. Watu wa mjini shamba lao ni mifuko yao, ongezeko la bei haliwasumbui na wafanya biashara wa kuleta chakula wapo. Tatizo ni wakulima watakao hitaji chakula na pesa hawana. Huna uthibitisho wa maghala ya serikali kuwa na akiba.
 
Ananufaika mkulima. Yani bei kubwa ipo shambani.
Ananufaika kwa muda, baadae anaenda kununua mjini mara mbili ya bei aliyo uzia. Mkulima wa Tanzania ana shida, anahitaji msaada. Mnufaika ni mfanya biashara.
 
Ananufaika kwa muda, baadae anaenda kununua mjini mara mbili ya bei aliyo uzia. Mkulima wa Tanzania ana shida, anahitaji msaada. Mnufaika ni mfanya biashara.
Aisee...sijui upo dunia gani....usikariri ndugu
Mkulima akivuna kitu cha kwanza anatoa mbegu za kupanda msimu ujao, mbili anatoa chakua kitachomtosha hadi mavuno yajayo, ndio anauza kinachobaki.
 
U mwongo na unapanga uongo. Sentensi zako mbili zinadhihiri. Hakutakuwa na njaa kwa sababu watu walilima na wana endelea kulima. Mazao yalipungua kwa sababu ya kupanda kwa bei ya mbolea na wakulima hawakumudu. Ukweli ni kuwa hakuna mazao ya kutosha kwa sababu ya kupungua kwa mvua na kupanda kwa mbolea. Kusafirisha mazao nje kutamshawishi mkulima kuuza yote na kuishiwa chakula. Watu wa mjini shamba lao ni mifuko yao, ongezeko la bei haliwasumbui na wafanya biashara wa kuleta chakula wapo. Tatizo ni wakulima watakao hitaji chakula na pesa hawana. Huna uthibitisho wa maghala ya serikali kuwa na akiba.
Hahahha usipaniki ndugu....
 
Back
Top Bottom