Tutofautishe kufunga na kubadili ratiba ya kula

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Kufunga ni Ibada ambao Mungu anakuwa karibu kujibu ombi na dua za mja wake
Kufunga ni kujinyima
Kufunga ni kutoa sadaka sana Kwa wahitaji
Kufunga ni Siri kati ya anae funga na Muumba
Kujitangaza na kujionyesha ati unafunga ni unafiki na dhambi

Unakuta mtu amefunga mchana anatembea na bakora kuwa hapa wasiofunga
Sasa huyu kafunga au unafiki?

Muda wa mfungo ndo unautumia kuhukumu wasiofunga

Mtu anafunga mchana, usiku anafungulia na kula kama panya

Anafungulia na kutumia sigara na pombe anakwambia Toka mchana sijavuta nilimfunga

Ukikuta anafuturu unatashangaa
Meza imejaa mavyakula ya mtu anakula kama anahamia Sudan

Meza ina uji, mtori, wali wa Nazi, pilau, nyama, samaki n.k yaani mavyakula mengi
Wakati Kuna mayatima hawajala

Kipindi cha mfungo hupaswi kula sana

Tuheshimu Ibada ya kufunga
 
Ni kweli ndo maana sisi wakristo huwa tunachagua kuacha kula chakula kimoja tu mimi kwaresma ya mwaka huu nafunga kula makande siku 40 ila vyakula vingine nakula kama mchwa.

Rafiki yangu mwaka jana alipata shida yeye alifunga kula nyama tukaalikwa sehemu tukaletewa sambusa za nyama akaanza kutoa zile nyama na akala maganda ya sambusa ili asiharibu funga yake.
 
Kuna wale wakifunga usiku unakuwa mchana wanafungulia na sigara

Au kujitoa mhanga
 
Ni kweli ndo maana sisi wakristo huwa hatufungi tunapumzika kula chakula kimoja kila mtu anachagua afunge nini, Demu wangu kachagua kufunga kula dagaa mchele hali dagaa mchele siku 40 ila vyakula vingine anakula kama kapewa tenda ya kufagia barabara ya SGR.

Wewe utafunga kula nini mkuu? Au utafunga kula uduvi hauli uduvi siku 40?
 
Nafunga kula dagaa nakula kitimoto ambayo ni tamu mno
 
Back
Top Bottom