SoC03 Tutokomeze majanga ya moto shuleni; Njia bora zaidi

SoC03 Tutokomeze majanga ya moto shuleni; Njia bora zaidi

Stories of Change - 2023 Competition

NACKO

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2022
Posts
1,298
Reaction score
2,514
Ni kwa muda sasa,WATANZANIA tumekuwa tukipitia maumivu makali ya Kupoteza Ndugu zetu wapendwa kwa ajali za moto mara kwa mara mashuleni..
Screenshot_20230613-202215.png

(picha kutoka JAMII FORUM)

Lakini je? ni kwanini basi licha ya kutuumiza vikali kiasi hiki,majanga haya bado yameendelea kujirudia mara kwa mara?...

VYANZO VIKUU VYA MAJANGA YA MOTO SHULENI;
A} UBOVU WA MIUNDOMBINU NA HITILAFU KATIKA MIFUMO YA UMEME.
Ubovu wa vifaa, shoti,kukatika katika hovyo kwa umeme,usanifu mbovu wa majengo,ukosefu wa vifaa vya kuzima moto,sio tu husababisha majanga haya mara kwa mara bali pia kuleta ATHARI kubwa zaidi mara majanga yatokeapo..

B} MOTO ULIOWASHWA KWA MAKUSUDIO FULANI...
Pia wanafunzi wanaweza kuchoma moto mabweni, madarasa na hata mali zinginezo za shule au walimu kwasababu mbalimbali kama vile, njama fulani tu, kuonyesha kuchukizwa zaidi na jambo fulani kama kero za muda mrefu na matatizo yasiyo tatuliwa kwa muda stahiki au kushikinikiza kukubaliwa kwa matakwa yao..
Screenshot_20230613-202406.png

(picha kutoka JAMII FORUM)

ATHARI ZA MAJANGA YA MOTO SHULENI
[a] Kupoteza maisha kwa WAATHIRIKA,ULEMAVU WA KUDUMU kwa waathirika pia matatizo ya KISAIKILOJIA.
Wanafunzi kukosa MASOMO yao kwa KUFUKUZWA SHULE au kwa kupisha shughuli za ukarabati miundombinu.
[c] HASARA ya pesa na upotevu wa mali..
[d] Wazazi kuwa HOFU muda wote juu usalama wa watoto wao wawapo shuleni.

JE NINI KIFANYIKE KUDHIBITI MAJANGA HAYA?.

A} ELIMU NA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA KUZIMA MOTO,
Shule nyingi bado hazina vifaa vya kuzimia moto wala utaratibu wa kutoa elimu ya majanga ya moto kwa wanafunzi,Ni vyema kwa kila shule iwe na vifaa vya kuzimia moto vya kutosha, Wanafunzi wafundishwe namna ya kuweza kupambana na majanga ya moto pindi ya yanapotokea ,wapewe ujuzi wa kutumia vifaa vya kuzima moto pia mbinu mbalimbali za kuweza KUJIOKOA kwa haraka pindi moto unapozuka ghafla.

B} UJENZI WA MAJENGO BORA NA YA KISASA..
Uwepo wa miundombinu isiyokidhi viwango, sio tu husababisha majanga ya moto kujirudia mara kwa mara, bali pia kuleta UGUMU ZAIDI wakati wa zoezi la UOKOAJI pale majanga yanapojitokeza..
Ili kurahisisha hili, ni vyema mabweni yakijengwa MAKUBWA bila VYUMBA, madirisha MAKUBWA,milango MINGI(angalau MITATU kwa bweni moja) MIKUBWA na yenye kufungukia nje,pia mabweni yakawekewa ALAMU ZA MOTO, na mifumo mizuri ya MAJI,..mfano(madumu makubwa ya kutunzia maji).

C} UBORESHAJI WA MIFUMO YA UMEME MASHULENI
Kwa kutambua hatari zinazoweza kujitokeza kwasababu ya hitilafu za umeme,ni vyema mifumo ya umeme IKASUKWA kwa UFANISI na TAHADHARI kubwa, pia kufanyiwa UCHUNGUZI na MAREKEKEBISHO mara kwa mara,..
mfano.,kwakua matumizi makubwa ya UMEME mabwenini ni kwa ajili ya MWANGA peke yake, hakuna haja tena ya KUNG'ANG'ANIA Matumizi ya umeme wa (VOLTI 230) MABWENINI ambao ni hatarishi, Kuna HAJA ya KUUCHAKATA na KUPUNGUZA VOLTI ZA UMEME kabla ya kuingia MABWENINI kutoka (VOLTI 230) hadi (VOLTI 12) ambao ni salama kiasi katika kusababisha MAJANGA YA MOTO ikilinganishwa na ule wa (VOLTI 230), pia kama umeme huu wa volti 12 ndio utakaotumika mabwenini bado waweza kutumika vyema na taa nyingi za kisasa zenye kutumia umeme MDOGO na kuwaka vyema.
IMG_20230709_095524_826_095800.jpg

(picha; ikionyesha mfano wa maboresho ya mfumo wa umeme mashuleni)

D} MALEZI BORA, UWAJIBIKAJI,HAKI NA USAWA..
Kila mmoja wetu ana WAJIBU wake katika kuhakikisha tunatokomeza majanga haya ya moto kama ifuatavyo:-
1; SERIKALI
[a] Kuhakikisha kila shule ina miundombinu na mazingira bora kwa usalama wa Wanafunzi wawapo shuleni. Na shule ambazo miundombinu yake haijakidhi viwango vya ubora kufungwa ili kunusuru Wanafunzi wetu.

Kupitia jeshi la ZIMA MOTO, kuboresha UFANISI wa utendaji kazi wa jeshi katika kupambana na majanga ya moto na pia kuendelea kutoa ELIMU kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla juu ya kupambana na majanga ya moto.

[c] Kupitia (TANESCO) kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa kutosha na uliotulia,.hivi karibuni tumeshuhudia umeme kukatika katika hovyo na kuto kutulia pindi ulidipo,jambo ambalo linaweza kuzua hatari ya moto shuleni hata majumbani mwetu pia....

2;WALIMU
[a] kutoa elimu na malezi bora kwa wanafunzi ili kuwajengea ujuzi wanafunzi wa kutatua changamoto mbalimbali kwa kutumia busara na hekima bila jeuri au kuvunja sheria kwa namna yeyote ile...

Kusikiliza, kujibu vyema hoja na kutatua kero za wanafunzi,. imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya shule zetu walimu kupuuza baadhi ya hoja au kero zinazowakabili wanafunzi, jambo ambalo huwaachia Wanafunzi dukuduku na hasira kwa muda mrefu inayoweza sababisha wanafunzi kuleta machafuko shuleni ikiwa watapata tu USHAWISHI..mfano wa kero maarufu shuleni zimekuwa ni UBOVU au UCHACHE WA CHAKULA. Pia ADHABU KALI kwa wanafunzi....

3; WAZAZI/WALEZI

[a] kuwalea watoto wao katika maadili mema,ili kuwawezesha kutoshiriki vitendo hatarishi.

kuangalia vyema ubora wa miundombinu ya shule husika kabla ya kuwapeleka watoto wao..mfano kumekuwa na Wazazi wengi ambao hawajawahi hata kuyaona MABWENI ambayo watoto wao wanaishi wawapo shuleni, jambo ambalo si vyema sana kwa usalama wa watoto..

[c] Kusikiliza na kuwasaidia watoto wao kutatua kero mbalimbali zinazo wakabili wawapo shuleni na sio kupuuza wajulishwapo...

4; WANAFUNZI
[a] Kutunza vyema miundombinu ya shule
kuwa na nidhamu,busara na hekima wakati wote.
[c] Kuacha kabisa vitendo vya jeuri na hatarishi vinavyoweza hatarisha usalama wao...mfano KUCHUBUA nyaya za umeme mabwenini ili kuweza kuchaji SIMU au REDIO.

5;JAMII NA WADAU WA ELIMU
[a] Kupinga vikali vitendo vya UKATILI dhidi ya Wanafunzi.

Pia Kama ilivyo kawaida kutolewa kwa misaada mbalimbali mashuleni, MISAADA hiyo pia iangazie namna ya kupambana na majanga ya moto.. mfano kurahisisha UPATIKANAJI na UTUNZAJI wa MAJI na vifaa vinginevyo vya kupambana na majanga ya moto..

[c] Kupiga vita vitendo vya UZEMBE vinavyofanywa na mamlaka mbalimbali katika kuangazia usalama wa Wanafunzi dhidi ya majanga ya moto.

[d] Kushirikiana sote katika kuwajenga vyema Wanafunzi kimaadili na kisaikolojia,pia kuwasaidia katika changamoto mbalimbali zinazowakabili....

WOTE KATIKA UJENZI WA TAIFA LETU...ASANTE:
 
Upvote 2
Haya matukio yamekuwa yakijirudiarudia hivyo yanapoendelea ni uzembe.
Kuna kipindi wizara ilitoa waraka kwa shule kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kudetect moto lakini wamekuwa wazembe kufanya ukaguzi kujua kama hivyo vifaa vipi my havipo
 
Back
Top Bottom