kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kutumia fursa ni elimu, kipaji au hulka ya mtu?. Wazungu wote sasa hivi wanapingana wenyewe kwa wenyewe hali inayopungaza uzalishaji na masoko yao kiuchumi. Lakini Ni ajabu kubwa kuona waafrika badala ya kutumia fursa hii kuungana na kuzalisha, kuuziana na kuwauzia wazungu tunawaza kutekana, kupigana na kuibiana kura kwenye chaguzi.
Tungeacha kila kitu na kutumia mwanya wa wazungu kupigana wenyewe kwa wenyewe katika kuzalisha zaidi ili kupunguza mwanya wa kiuchumi kati ya wazungu na Waafrika.
Huu ni wakati wa kuahilisha na kubadilisha vipaumbele vyetu kama vile Uchaguzi, Ujenzi na miradi mingine ambayo haileti matunda ya haraka Kiuchumi ili kuzalisha zaidi na kuwauzia wazungu chakula na nguo za kuvaa ili wapigane zaidi.
Natamani kusia hakuna Uchaguzi wala ujenzi wa sijui nini na fedha zote za uchaguzi na ujenzi zitatumika kwenye kununua na kugawa matrekta kila kijiji, kuchimba mabwawa ya umwagiliaji na kugawa pembejeo ili tuzalishe ngano, ndizi, pamba, kahawa, matunda nk kwa wingi na kusafirisha huko wanakopigana na kuwekeana vikwazo.
Lakiniii, loooh! utasikia Msigwa kahamia kule, jamaa anachochea Mamasai Ngorongoro, nani yule katekwa na kupigwa sana. TAMISEMI imetoa tarehe ya uchaguzi. badala ya kuwaza fursa. Shame!