SoC04 Tutumie rasilimali zetu tulizopewa na Mungu kukusanya pato la taifa kuliko kuwa na kodi na tozo kandamizi kwa wananchi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Inashangaza sana kuwa na taifa ambalo lina kila aina rasilimali ambazo zikitumiwa vizuri tunaweza kuwa na taifa ambalo lina pato kubwa la taifa.

Fikiria madini ya almasi, dhahabu, ruby au Tanzanite yakivunwa vyema na kisha kuuzwa taifa letu litanufaika na kuwa na pato kubwa.

Hivi hii nchi inashindwa kuwa na hata Mgodi mmoja dhahabu na kisha uvunaji ukifanyika dhahabu ziuzwe na kisha kupata fedha za kigeni?

Hivi kwa jinsi tulivyo na eneo kubwa la bahari ambalo likitumika vyema uvuvi kwenye bahari kuu unaweza kufanyika na kuleta manufaa. Kwa nini tusijinufaishe na uvuvi kama nchi Japan na Denmark zinavyonufaika?

Hii ni mifano tu.

Alafu bila aibu tunag'ag'ana kuwa na tozo kandamizi kila kona . Ukiweka umeme tozo, ukilipia maji tozo, wafanya biashara wadogo wanakandamizwa no tozo kibao. Wafanyabiashara wakubwa walia kila kona.
 
Upvote 6

Back
Top Bottom