Mfumo huu upo Sana kwenye system ya medical school. Watoto wakike wanajikuta hawana option Ila kutoa rushwa za aina hiyo.
Madaktari wanao fundisha wanamamlaka makubwa Sana juu ya hatima ya ufaulu wa wanafunzi wao.
Daktari anaekufundisha ndio anakutungia mtihani, mtihani ipo ya aina si chini ya tano, Insha ndefu, Insha fupi, ya kutambua vitu, ya kujieleza Kwa Mwalimu wako na ya kumpima mgonjwa Kwa vitendo mbele ya Mwalimu.
Hivo basi ukiangalia mitihani ya ainahii inapima ufahamu na haina ushahidi ukiachilia ile miwili ya mwanzo na Mwalimu akiamua kukufelisha ni rahisi Sana na huna cha kumfanya.
Ikumbukwe kua si tuu walimu huomba rushwa ya ngono Bali hata mabinti wasiojiweza huwahonga ngono walimu ili wafaulishwe na matokeo yake ni kupata madaktari wa hovyo.
Kwa sababu hiyo sidhani Kama PCCB watatatua tatizo hili la kimfumo .
Nadhani wizara ya afya na TCU wabuni mfumo rafiki Kwa madaktari wanafunzi wa kike.
Ningeshauri madaktari wanafunzi wakike watahiniwe na walimu wa kike tena kutoka chuo tofauti na kile wanachosomea. Hili litamaliza tatizo hasa madaktari hawa wakiwa na uhakika kua walimu wao wa kiume hawana mamlaka juu Yao Kwa kutahiniwa
Nasikitika kusema kua hili limechelewa kuja na kwavile limefikishwa hapa naomba tutambue kua watoto wetu wanaliwa hasa, na haishii hapo na wengine wanaambukizwa magonjwa, wengine wanaathiriw kisaikolojia Kwa kuhonga bikra zao na mengine mengi..... Hivo basi tuwaunge mkono watoto wetu
.