Haya mambo ya miundombinu ya nchi kupewa majina ya watu binafsi naona kama ni ushirikina na kuabudu mizimu tu.
Mbona siku za nyuma haya mambo hayakuwepo? Mfano hapa Dar es Salaam Uwanja wa ndege uliitwa tu Dar es Salaam,barabara iliitwa pugu rd,ya mandela iliitwa port access lakini leo kila kitu Nyerere, Mkapa,Kikwete sijui Magufuli,kumbuka siku zote sifa ndiyo inaleta jina na wala siyo jina linaloleta sifa maana yake watu watakukumbuka na kuendelea kukutaja kwa yale uliyoyatenda.