Nanukuu Morrison goli 0 msimu 1" mwisho wa kunukuu.
Naomba nizungumzie upande wa michezo ya kimataifa msimu wa 2021/2022 kwa upande wa Simba, ilibebwa pakubwa sana na mchezaji Morrison.
Mechi ya Galaxy vs Simba magoli mawili ya Simba yalipatikana kwa mchango wa Morrison.
Mechi ya marudiano kwa Mkapa Simba walipata goli moja lilipatikana kwa mchango wa Morrison.
Mechi iliyofuatia ilikuwa dhidi ya red arrow, Simba walipata ushindi wa magoli matatu yaliyotokana ya jitihada za Morrison.
Mechi za makundi, Simba walianza na Mimosa na Morrison alichangia ushindi wa Simba. Mechi ya Berkane na USGN kwa Mkapa ni Morrison pia anahusika kwenye magoli ya Simba.
Mechi ya away dhidi ya USGN bila goli alilosawazisha Morrison Simba wasingefuzu robo fainali kwasababu wangemaliza wakiwa na point 9 tu.
Halafu Biligumana hakusajiliwa Yanga kwaajili ya kufunga kwasababu sio striker bali kiungo mkabaji.