Tuulize chochote kuhusu mbao na changamoto zake

Tuulize chochote kuhusu mbao na changamoto zake

Mbao Tanzania

Senior Member
Joined
May 31, 2021
Posts
170
Reaction score
215
Heri ya mwezi mpya,

Sisi ni wataalamu wa mbao za aina mbalimbali zinazozalishwa nchini Tanzania. Tupo Dar es Salaam. Tunao ujuzi na uzoefu wa miaka mingi.

Kama inavyofahamika, shughuli za ujenzi wa majengo na baadhi ya miundombinu hapa kwetu kwa kiasi kikubwa bado hutegemea mbao kama mojawapo ya nyenzo muhimu.

Je, unawezaje kutambua mbao nzuri, imara na zinazofaa kwa mradi anuai?

Tumekuja JamiiForums kujuzana na kuepusha hasara ambayo wadau wa ujenzi hukumbana nazo, yakiwemo makampuni na watu binafsi kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha.

Tutajibu maswali yote tutakayoyamudu kwa wakati.

Karibuni sana.
 
Unawezaje kutofautisha mbao ambayo ni imepitia process zote kuwa treated (treated timber) na fake?
Mbao iliyopitia mchakato wa dawa (treated) huwa zinachemshwa na kubadilika rangi mpaka ndani ya mbao husika.

Mbao ambazo hazijawa treated mara nyingi huwa na muonekano wa rangi nyeupe angavu.
 
Mbao za mikaratusi zinafaa kutengenezea fremu za milango, madirisha na kadhalika.
Kwa nini zinapinda au kuachana na kuacha uwazi, zikitumiwa kutengeneza milango, je, ni mbao zipi zinafaa kutengeneza milango na samani mbalimbali kwa ubora zaidi ya mninga.
 
Mnaweza mkajua mbao zinazopatikana kwa wingi?

Mfano mkaratusi unapatikana wapi kwa wingi, mninga, mkongo, mtondoro mpodo, mvule, mkangazi,mkarati, msederea, na Bei zake huko zinakopatikana.

Pia vibali vya kununua kusafirisha na kuuza mbao mnaweza kujua namna vinavyopatikana? Natanguliza shukrani.
 
Kwa nini zinapinda au kuachana na kuacha uwazi, zikitumiwa kutengeneza milango, je, ni mbao zipi zinafaa kutengeneza milango na samani mbalimbali kwa ubora zaidi ya mninga..
Hapa na mimi ningependa kujua,na kama zina hii tabia zinawezaje kufaa kwa kutengenezea fremu za milango au madirisha...?
 
Tunaendelea kupitia maswali yote. Tutajibu kwa kadri itakavyowezekana. Asanteni sana.
 
Mnaweza mkajua mbao zinazopatikana kwa wingi?
Mfano mkaratusi unapatikana wapi kwa wingi, mninga, mkongo, mtondoro mpodo, mvule, mkangazi,mkarati, msederea, na Bei zake huko zinakopatikana.
Pia vibali vya kununua kusafirisha na kuuza mbao mnaweza kujua namna vinavyopatikana? Natanguliza shukrani.
Tutakuja na details za kutosha juu ya hili. Acha tukusanye data za uhakika ndugu, tutakujibu mapema iwezekanavyo.
 
Je naweza kuezeka Nyumba yangu kwa kutumia mbao za Mninga?

Kwa kuongezea hapa:

Mbao za mninga zinapendwa kwa sababu ni imara sana lakini gharama yake ipo juu hivyo ni mara chache hutumika kwa shughuli za kuezekea.

Kujibu swali lako, ndiyo unaweza kuezeka nyumba yako kwa kutumia mbao za mninga.

Asante.
 
Kwa nini zinapinda au kuachana na kuacha uwazi, zikitumiwa kutengeneza milango, je, ni mbao zipi zinafaa kutengeneza milango na samani mbalimbali kwa ubora zaidi ya mninga..
Ni kutokana na asili yake.

Ndiyo sababu ni nadra mikaratusi kutumika kutengenezea milango, makabati na samani na badala yake hutumika kama mistimu ya umeme, fremu na baadhi ya kingo/viambata vya madaraja n.k.

Bado mninga ndiyo mbao nzuri na bora kwa utengenezaji wa samani kuliko aina nyingine yoyote.
 
Back
Top Bottom