Tuulize chochote kuhusu mbao na changamoto zake

Mbao za mikaratusi zina changamoto ya kupinda na kuliwa na mchwa. Pia wakati wa mvua zinavimba hivyo milango haifungi
Ndio maana hazipendekezwi sana japo zinafaa. Ni chache zilizopandwa vizuri tangu zikiwa mbegu ndio zinaweza kutoa matokeo chanya.
 
Nin ddawa ya mdudu anayekuka mbao na kuacha unga unga?
 
Je, naweza kuezeka Nyumba yangu kwa kutumia mbao za Mninga?
Bila kujali gharama ya mninga, mbao ngumu (hardwood) hazitumiki kuezekea kwa sababu mbili kubwa:
1. Ni fupi (ni ngumu kupata mninga ulionyooka kwa zaidi futi 12, hivyo hufanya mbao zake nyingi kukatwa kwenye vipimo vya futi 8 au zaidi kidogo tu)
2. Ni nzito (inafanya paa liwe zito sana, utahitaji ujenge kuta/nguzo imara zaidi ili kuhimili uzito wa paa)
 
Uzuri wake ni upi zaidi ya mkongo?
 
Nin ddawa ya mdudu anayekuka mbao na kuacha unga unga?
Ni kupulizia au kupaka dawa mbao husika. Kuna aina mbalimbali za dawa ambazo unaweza kutumia.

Aidha tunashauri wakati mwingine utumie mbao zilizochemshwa na dawa kama tulizonazo.
 
Ni kupulizia au kupaka dawa mbao husika. Kuna aina mbalimbali za dawa ambazo unaweza kutumia.

Aidha tunashauri wakati mwingine utumie mbao zilizochemshwa na dawa kama tulizonazo.
Kuna wengine niliona wanatumia machine ya vacuum ili kupenyeza dawa kwenye mbao.
Zinakaa saa 24
 
Utajuaje ile dawa ya kutreat mbao ni fake ama sio fake..ile ya kijan..maana naskia mchezo huo upo sana bugurun pale
 
Kwa wataalam naomba mnisaidie, Mbao za mti wa muembe(mango tree) zinafaa kuezekea au kutengeneza fremu?
 
Mkuu wangu Mbao Tanzania tafadhali nipe elimu kuhusu mbao ya Mkangazi, je inafaa kwenye furniture za kitanda? Maana nataka nichukue kitanda cha mkangazi nimeambiwa ni kizuri na mbao yake ni bei ghari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…