Naona umekuja kivingine, nakubaliana sana na huo msimamo wako, lakini nauchukia pia kwa sababu unaambatana na kiburi, dharau na matusi.
Unakuwa kama huishi kwenye dunia hii, ambayo hata Bwana Yesu alisema Tunaishi kwa Neema sio kwa matendo ya sheria. Unakuwa kama vile wewe hujawahi kutenda dhambi, wala hutendi dhambi.
Ashukuriwe Mungu kwa sababu yeye haangalii kama mwanadamu anavyoangalia, Siku moja Mfalme daudi alimkosea Mungu, akasema ni afadhali kuangukia ktk mikono ya Mungu kuliko kwene mikono ya mwanadamu.
Napingana na uovu wa namna yoyote na ninamheshimu Mungu. Lakini sipendi mtu anaekemea dhambi kwa kiburi na matusi, zaidi hata ya Mungu mwenyewe anavyotuonya.
BARIKIWA