Ninamuona Magufuli aliyepambana na CCM yake mwenyewe kwa machozi. Haikuwa kazi rahisi kupambana na watu wa nyumbani mwake mwenyewe. CCM kama familia ndio waliofukuza machinga na mama ntilie kama mbwa katika nchi yao wenyewe, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake.
Madereva walikunywa viloba, ajali zikaua sana, tukasema Freemason wanatoa sadaka, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Yaliuzwa majenereta kwà kila duka, na wenyewe majereta wakauziwa mafuta, umeme ukachezewa, yakaundwa makampuni ya kuiuzia umeme TANESCO. Watu walipiga ela, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Wanasiasa waligawana maeneo mahekali kwa mahekali, waligawana maeneo ya madini, maeneo ya mbuga za wanyama, vyura walisafirishwa, walishindana kumiliki fukwe za bahari. Masikini hawakuwa na thamani. Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Mafuta yalipita bandarini bila kulipiwa kodi, makampuni yakabinafsishwa kwa bei chee. Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Leo hospitali za serikali zinajaa vijana wanaotibiwa baada ya kuathirika na madawa ya kulevya, kutokana tabia za watawala, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Sarafu za shilingi mia tano mia tano zilisafirishwa kwenda china, na biashara ilifanywa na watanzania, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Nchi nyingi zilipata sifa ya kuuza madini ya Tanzania, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Ndugu watanzania tusije jikuta tunakimbilia Pete iliyopakwa rangi ya dhahabu huku tukikanyaga dhahabu yenyewe. Sina tatizo na upinzani, ila nataka kusema kwamba unapotaka kubarisha gari uwe na sababu iliyo bora sana. Tusiongozwe na chuki wala mihemuko au ushabiki. Tukumbuke kwamba siasa is about our life and the future of this nation. Wish you uchaguzi mwema. Wakati wote Magufuli alipambambana CCM yake mwenyewe.
CLEMENCE MWANDAMBO MWALIMU WA CHEKECHEA. karibu Mbeya.