Uchaguzi 2020 Tuungane kwa umoja wetu kama Taifa tuikatae CCM, miaka 59 imetosha

Hakuna sababu ya kuendelea kung'ang'ania kitu kisichokuwa na faida 50+ yrs inatosha.
Na hata wakiendelea kuongoza hii nchi miaka elfu ijayo hakuna jipya litakalofanyika la tofauti na hapa uwezo wao ulipoishia.Wakae pembeni wajivue gamba walilokaa nalo toka uhuru labda watapata akili mpya.
 
Ingependeza ungesema ni Operation vunja Jiwe....Au Operation Mwaga Pombe.
Au ungesema ni TAL v. Jiwe, ukisema CCM hapo utaleta uchama. Watu wengi wanapigia chama kuliko mtu.
 
Mabadiliko ni muhimu.Lazima kuje akili mpya ili ifanye mabadiliko ya hali na mifumo iliyokwisha haribika.Haijalishi itatumika muda gani kulingana na aina ya maboresho yanayohitajika na waliopo wameshakaa vyakutosha na uwezo umeshaisha.Lakini pia lazima ijulikane kua yoyote anaweza kuongoza kwahiyo ukipewa nafasi ukazingua unakaa pembeni anakuja mwingine.
 
Na hata wakiendelea kuongoza hii nchi miaka elfu ijayo hakuna jipya litakalofanyika la tofauti na hapa uwezo wao ulipoishia.Wakae pembeni wajivue gamba walilokaa nalo toka uhuru labda watapata akili mpya.
They have reached their capacity limit. Hawana jipya.
 
Na hata wakiendelea kuongoza hii nchi miaka elfu ijayo hakuna jipya litakalofanyika la tofauti na hapa uwezo wao ulipoishia.Wakae pembeni wajivue gamba walilokaa nalo toka uhuru labda watapata akili mpya.
They have reached their capacity limit. Hawana jipya.
 
Ninamuona Magufuli aliyepambana na CCM yake mwenyewe kwa machozi. Haikuwa kazi rahisi kupambana na watu wa nyumbani mwake mwenyewe. CCM kama familia ndio waliofukuza machinga na mama ntilie kama mbwa katika nchi yao wenyewe, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake.
Madereva walikunywa viloba, ajali zikaua sana, tukasema Freemason wanatoa sadaka, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Yaliuzwa majenereta kwà kila duka, na wenyewe majereta wakauziwa mafuta, umeme ukachezewa, yakaundwa makampuni ya kuiuzia umeme TANESCO. Watu walipiga ela, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Wanasiasa waligawana maeneo mahekali kwa mahekali, waligawana maeneo ya madini, maeneo ya mbuga za wanyama, vyura walisafirishwa, walishindana kumiliki fukwe za bahari. Masikini hawakuwa na thamani. Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Mafuta yalipita bandarini bila kulipiwa kodi, makampuni yakabinafsishwa kwa bei chee. Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Leo hospitali za serikali zinajaa vijana wanaotibiwa baada ya kuathirika na madawa ya kulevya, kutokana tabia za watawala, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Sarafu za shilingi mia tano mia tano zilisafirishwa kwenda china, na biashara ilifanywa na watanzania, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Nchi nyingi zilipata sifa ya kuuza madini ya Tanzania, Magufuli akasema hapana, leo anaonekana hafai kwa sababu ya usisiem wake. Mema yake yanayeyushwa na wapenda madaraka.
Ndugu watanzania tusije jikuta tunakimbilia Pete iliyopakwa rangi ya dhahabu huku tukikanyaga dhahabu yenyewe. Sina tatizo na upinzani, ila nataka kusema kwamba unapotaka kubarisha gari uwe na sababu iliyo bora sana. Tusiongozwe na chuki wala mihemuko au ushabiki. Tukumbuke kwamba siasa is about our life and the future of this nation. Wish you uchaguzi mwema. Wakati wote Magufuli alipambambana CCM yake mwenyewe.


CLEMENCE MWANDAMBO MWALIMU WA CHEKECHEA. karibu Mbeya.
 
Rubbish..
Tz ilipopata uhuru Nyerere alipata wapi hao??
 

Kwahiyo hizo nafasi zikijazwa na watu wapya itatoa Ajira mpya kwa wengine wenye mawazo na mbinu mpya za maendeleo...
 
CCM kuendelea kutawala Tanzania ni aibu, kashfa isiyo na mfano. Kazi ni moja tu oktoba kuitosa 'baharini ' itokomee kusikojulikana daima milele.
 
Kuyapata uliyoorodhesha tunahitaji mgombea jasiri mwenye uthubutu huu:

View attachment 1527407
Huo ndiyo ulio ukweli.

Huyo ndiye ambaye atakaye tuvusha.
Vyote hivyo Mh.Lissu anavyo na zaidi,lakini huko CCM mpya hayo hayajadiliki maana wametekwa na Uncle Meko na timu yake.Bila kuiondoa madarakani hatuwezi kuota mambo ya haki za binadamu.
 
Magu ni Hadi atacha kuwatumikia wananchi, hajawahi kushindwa na hatoshindwa kamwe na mpinzani awaye yote, hii yote ni Kwa sababu historia yake ya utendaji na uthubutu wake, Unambeba, huwezi kushindana na mtu ambaye historia yake inamzungumza Kwa mengi mazuri, na Watanzania sidhani kama wanaweza kumwachia huyu mtu kizembe kizembe kiasi hiki, kisa tu kuna mtu anayebebwa na tukio la kuumizwa katka maisha yake

Wapinzani sio kwamba ni wabaya, hapana, ni watu wazuri, wanajua wanataka nini, Nia zao ni njema Kwa ajili ya nchi yetu!

Na mawazo na hotuba ya Mh Lisu Jana, ni hotuba moja nzuri na mpya masikioni mwa wengi, inaacha maswali na kiukweli inapaswa ishughurikiwe na KUFANYIWA KAZI sasa!

Ila,kumwacha Magufuli, itakuwa ni bonge la Ujinga nchini, Kwa vitu vingi vikuubwa alivyothubutu kuvianzisha na kuvifanya Kwa kipindi hiki kifupi, Dunia na washindani wa nchi yetu hasa majirani zetu watatucheka

Nchi yetu inawatu wengi mahiri na wazuri, Lisu ni mtu mahiri na mzuri Kwa vitu vingi, ika Kwa sasa! Hapana, angojee Kwanza, sababu, ni wetu, kakutana na mtu mwingine mzuuri zaidi basi
 
Mfumo ndio unaokwenda kubadirishwa jipe muda kusikiliza mipango ya baadhi ya wagombea wanazungumzia tatizo la mfumo mbovu wa utawala ndiyo msingi wa umasikini wetu na huo ndiyo kubadilishwa CCM haiwezi kuubadilisha sababu unainufaisha. Kama wanavyokataa katiba mpya na tume huru.
 
Daah dish limeyumba
 
Ila utamu wa madaraka wa awamu ya 5 umezidi hadi figisufigisu kwa wagombea kumbe wagombea wanatakiwa wajue karate na kutumia silaha?
 

sore but ccm is here to stay 2100 ndo wnaweza kufikiria vyama vingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…