Nicorandil
JF-Expert Member
- Aug 9, 2022
- 258
- 749
Habari za usiku ndugu?
Natumai mu wazima wa afya.
Nimekuwa nikiwaza namna nzuri ya kuwekeza pesa yangu niliyoipata hivi karibuni, 3m. Nikataka kuiweka katika fixed account lakini kila nikiwaza benki kukaa na pesa yangu kwa mwaka na zaidi halafu kunipa 9.5percent rate naona ni ndogo.
Hivyo nikawaza kuiweka walau nusu UTT na nusu katika fixed account. Tena nikapata wazo kutembelea bureau de change nakuigeuza dollar ili isishuke thamani. Kama mnavyoona mawazo ni mengi lakini naamini wapo watu watakaonipa mawazo mazuri zaidi au kuboresha ya kwangu.
Katika yote sijaongelea kufanya biashara kwa sababu sina mpango huo kwa sasa kutokana na kuwa na kitu kingine kinachohitaji uwepo wangu muda wote na vile vile sina matumizi nayo kwa sasa ila nataka kulinda thamani yake au iongezeke. Asanteni na karibuni.