Tuuombee Mkutano wa SADC kesho Ili Mgogoro wa DRC uoate suluhu

Tuuombee Mkutano wa SADC kesho Ili Mgogoro wa DRC uoate suluhu

ni muhimu zaidi kuzingatia waakina mama na watoto wanaoteseka na kupoteza maisha bila ya hatia huko DRC,

hakuna haja ya kupepesa macho,
Rais Paul Kagame anastahili kuwajibishwa kimkakati na kikanda mapema iwezekanavyo kabla ya maafa zaidi kutokea DRC na eneo zima la maziwa makuu, kubeba jukumu la kuwalea wakimbizi.

Ni matumaini yangu uamuzi mzito wa maneno na vitendo utatolewa na kuchukuliwa hatua za haraka dhidi ya M23 na Kagame kutoka EAC na SADC 🐒

Yes,maana wahanga wakubwa wa ghasia hii ni wale ambao hata hawana stake.Maana kila anayetaka madaraka kwa nchi za kiafrica ni zaidi kwa ajili yake bonafsi na wala siyo kwa ajili ya wananchi.Ndiyo maana wanaona si kitu wanachi hasa watoto na wanawake kuuawa
 
WaAfrica wote ni vibaraka na wanafiki tu, siku tukiacha hivyo vitu ndio vita na maendeleo yatapatikana Africa.

Huwezi ukawa sio kibaraka kama unategemea misaada kutoka magharibi na hata budget yako inajaziwa na mabeberu, miradi yako inahitaji mabeberu na misaada.

Asiye kibaraka ni yule anayejitegemea kwa kila kitu, yule mwenye technolojia na uwezo wa kutengeneza kila akitakacho akiamua.
Fact
 
Pk ngoma ngumu akili kubwa kawasilo

Ova
 
Kiukweli kabisa ni vyema mno vita kuisha ila kwa uhalisia uliopo tuwe wawazi ile tayari ni WAR zone kupatuliza serious labda weupe waamue.

Moja ya simulizi nzuri sana japo ilikuwa ni tukio la kweli ila likafanywa filamu ni Rambo IV kuhusu ishu iliyokuwa Burma ndo maana ilifunza si kila kitu kitaisha kwa maombi ila kuna muda binadamu anaamua hatma yake yeye mwenyewe.
RIP Juvenal Habyarimana
 
Kesho moja ya agenda,kimsingi agenda kubwa ambayo masikio ya wengi yanasubiri kuona maridhiano ya mgogolo wa huko DRC unafikiwa muafaka.Tuendelee kuwaombea afya njema wahusika wote wakuu ikiwa ni pamoja wa maraisi wa DRC na Rwanda.Pia wawe na moyo wa huruma kuhurumia mamia ya wanawake na watoto wanao teseka huko ikiwa wao wanaishi kwenye viyoyozi.

Kibaya zaidi muafrica anamua mwafrica mwenzake halafu wazungu wanaendelea kuchota rasilimali za nchi yao.Nataka niwakumbushe tuu hawa wakuu wa nchi hasa hizi za maziwa makuuu.suluhu ya migogoro yetu haiwezi kuamliwa na wadau nje ya maziwa makuu.ni wakati pia wa kuonyesha kwamba mataifa yetu yanaweza maliza baadhi ya migogolo wao wenyewe bila mzungu.

Halafu pia misada kwa wakimbizi imepungua sasa baada ya marekani kusitisha huo ujinga wa kuendelea kusaidia nchi ambazo hazi graduate toka kwenye umasikini.ikiwa wanaograduate toka kwenye umasikini ni viongozi wanaojilimbikizia mali na kutumiwa na vibaraka wa huko magharibi
wanasiasa hao wanaokutana ni debe tupu tu the real players ni big corporations kama apple,microsoft na kampuni za magari ya umeme majuu!Tshisekedi hana chaguo zaidi ya kuwapa waasi KIVU nzima na kuwapa mamlaka ya kujitawala.Sion option nyingine hapo.Makampuni ya magharibi hayawezi kujitia kamba shingoni(kumwachia mchina a-stretch influence yake mahali kwenye strategic mineral reserve).Mind you kwasasa kuna mashindano makubwa baina ya nchi za magharibi na China kwenye production ya magari ya umeme na vifaa vya kielectronic.
So wanasiasa wanakutana kwa ufadhili wa big corporations kujadili interest za big corporations and nothing else.Hapo Kagame ataibuka kidedea😂
 
Kesho moja ya agenda,kimsingi agenda kubwa ambayo masikio ya wengi yanasubiri kuona maridhiano ya mgogolo wa huko DRC unafikiwa muafaka.Tuendelee kuwaombea afya njema wahusika wote wakuu ikiwa ni pamoja wa maraisi wa DRC na Rwanda.Pia wawe na moyo wa huruma kuhurumia mamia ya wanawake na watoto wanao teseka huko ikiwa wao wanaishi kwenye viyoyozi.

Kibaya zaidi muafrica anamua mwafrica mwenzake halafu wazungu wanaendelea kuchota rasilimali za nchi yao.Nataka niwakumbushe tuu hawa wakuu wa nchi hasa hizi za maziwa makuuu.suluhu ya migogoro yetu haiwezi kuamliwa na wadau nje ya maziwa makuu.ni wakati pia wa kuonyesha kwamba mataifa yetu yanaweza maliza baadhi ya migogolo wao wenyewe bila mzungu.

Halafu pia misada kwa wakimbizi imepungua sasa baada ya marekani kusitisha huo ujinga wa kuendelea kusaidia nchi ambazo hazi graduate toka kwenye umasikini.ikiwa wanaograduate toka kwenye umasikini ni viongozi wanaojilimbikizia mali na kutumiwa na vibaraka wa huko magharibi

Mgogoro wa huko DRC (Zaire) kati ya Serikali ya huko na Waasi hautapatiwa suluhisho kwa njia za maombi bali kwa njia za KUTENDA HAKI KWA WANANCHI WOTE BILA YA UBAGUZI WA AINA YOYOTE ILE. Suluhisho pekee kwa Mgogoro huo ni kuanzisha Utawala wa nchi ambao utazingatia HAKI na DEMOKRASIA.
Hii ndio suluhisho pekee lililopo.

Kumbuka:

"Njia pekee ambayo Wananchi wataitumia katika kuzungumza au kujadiliana na Watawala wao ambao ni Madikteta ili kufikia muafaka wenye maslahi kwa pande zote mbili ni kwa kupitia mtutu wa bunduki."

Jeffs O'Brien.
 
Back
Top Bottom